Stanbic wamegoma kutoa orodha ya waliochukua

Nchi ikiingia katika RUSHWA system yote huwa inaparanganyika,siyo serikali,bunge na mahakama wote chali.Hivi kwa nini Rais wetu hakuliongelea hili? BOT inajua taratibu sahihi za uchukuaji wa fedha kwa nini Gavana yupo kimya? Najuta kukishuhudia kizazi cha nyoka mapema hivi.Hata akina Kigunge watetezi wa Azimio la Arusha enzi hizo kimya.Wote hao walikuwa wanafiki kwa Mwalimu.Zuma na ANC yake ni aibu sana South Africa mpaka waafrika wenzao wanawashangaa.Rushwa rushwa unatupeleka wapi sasa na viongozi wetu?



TUKO KPINDI KIGUMU,nawaonea huruma watanzania wangu kwa kimya hiki,makaburi yetu yatakuwa MUSEUM ya wajukuu zetu kuangalia jinsi tulivyouza twiga hai,dhahabu,TANZANITE.Itabidi mafufu ya vichwa vyetu yachunguzwe kama yalikuwa na ubongo sahihi.
 
Nasikia tape ya CCTV inayoonesha wababaji wa viroba iko chini ya ulinzi mkali kwa Madiba.

Ila kwa ufupi, haya mambo ya baraka za mtu mmoja tu hapa Bongo...akiamua (jambo ambalo haliwezekani), kila kitu kinaisha ndani ya saa 24!
 
Hatukubali mpaka ishu ya stanbic iwekwe wazi aka sivyo hata hawa akina muhongo
 
Mie najiuliza hivi kumbe kama kuna vikundi vya kigaidi vinafadhiliwa fedha kuhujumu nchi yetu na fedha hizo zikapotia kwenye mabenki yetu kumbe serikali haina uwezo wa kuziamuru benki hizo kutoa taarifa ya nani kalipwa fedha hizo?
Kama sheria zetu haziwezi kupata taarifa hizo toka mabenki yetu basi tuko hatarini sana.
Mkuu Tanzania tunaserikali ya kushughulikia wapinzani tu si kulinda maslahi mapana ya umma.sema tu watanzania tunamoyo otherwise kingekuwa kishanuka
 
Mkuu Tanzania tunaserikali ya kushughulikia wapinzani tu si kulinda maslahi mapana ya umma.sema tu watanzania tunamoyo otherwise kingekuwa kishanuka
Sisi hatuna moyo, sisi ni wabinafsi. Kila mtu anasemea kwake. Aliyeko kwenye system anaitetea, aliyeko nje anaongelea nyumbani. Hakuna Watu ambao wako tayari kulikomboa Taifa hili.
 
Kwenye Orodha ya Stanbic na Mbiwe yumo. Ndo maana hali iko hivyo

Yaani wewe kweli ni MWEHU yaani jina la Mbowe liwemo orodha ifichwe? kama Kikwete siku hizi ndio anaitwa Mbowe ni sawa. je hauoni kama hiyo ndio ilikuwa nafasi ya CCM kujisafisha na suala hili.
 
Hivi bongo hatuna ma-IT experts wanaoweza ku-hark system ya stanbic kweli!!!!!?????

Kiuhalisia kwa jinsi nchi ilivyo huyo IT atakayefanya hivyo sidhani kama ataweza kuishi zaidi ya siku tatu kwani TISS na UWT waliopo hapa nchini wapo kwa ajili ya kulinda mambo ya hovyo kuliko kulinda mamba yaliyo bora kwa maendeleo ya nchi.
 
Hawana uhusiano mkuu...

Ilivyo ni kuwa, Stanbic ni subsidiary company ya Standard Bank ya South Africa, walipokuja bongo tayari Standard Chartered Bank walikuwa wana branches hapa ikabidi ili kujitofautisha, waje na hilo jina la Stanbic.

Okay. Lakini ni South Africa based. Na huu ujio wa Zuma wa ghafla niliutilia shaka.
 
Kilichonoshangaza ni kwamba Tundu Lissu ndo alitamka star TV kwamba stanbic wamegoma kutoa orodha. Nilipatwa na wasiwasi maana alionyesha kama hamna njia vile ya kupata orodha. Lakini hii benk ikishtakiwa hata kwenye mahakama za kimataifa ambazo tunashirikiana nazo wanaweza kutussidia kuwaumbua stanbic.
 
Orodha ipo Mbowe na Slaa walionekana wamebeba viroba vya pesa

Sawa! Mleta mada anasema tunahitaji orodha ya mgao ule. Haijalishi ni majia ya kma Kinana au Slaa kuwa yamo. Tunahitaji orodha ya mgao. Destructor unajiondoa akili unajibu unachoona ni kizuri kwako
 
lizaboni kiongozi, mbona mnakuwa vipofu kiasi hicho nyie waungwana!!! Kila kitu nyie ni siasa za kujadili mtu, hata haya mambo yanayoongelea taifa kazi yenu ni kuleta siasa za vyama tu? Lini mtakuwa kisiaaa jamani...so sad..hili taifa lina tabu kuwa na binadamu wenye weledi wa kuku.

mkuu ndio umaskini wa fikra walio nao wenzetu wao ni sifia sifia ili wapatiwe ujira wao. Bila kuchanganya na akili kidogo ya kupambanua mambo ya msingi na yakishabiki shabiki.mimi wakati mwingine najiuliza hivi hao viongozi wao wa chama wanawacheka kiasi gani? Au wanadhani wanawapenda kwa kushabikia ujinga? Wanawaona kama walemavu wa kifikra wasio jitambua.
 
Kwenye Orodha ya Stanbic na Mbiwe yumo. Ndo maana hali iko hivyo

nakufananisha na mavi kwa kweli,, hata sijui unaakili gani. Mbowe hana mabavu ya kuzuia lolote lile katika hili kuwa mkweli acha unafiki.
 
Back
Top Bottom