Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,723
Nafikiri kwa timu yoyote itayovuka kati ya hizi kukutana na yanga basi itatakiwa ifanye kazi ya ziada mara 2 kuizuia yanga, naangalia mechi yao hapa inayoendelea sijaona timu ya kuisumbua yanga, Al Hilal wanao wachezaji wazuri lakini wanakosa muunganiko kila mchezaji anacheza kwa uwezo binafsi na sio kitimu, na ndicho kilichowagharimu mpaka sasa wako nyuma kwa goli 2 bila, St George tuliyoiona ikicheza na Simba hapa Tanzania mechi ya kirafiki naiona ni ile ile akuna kilichobadilika wamefanikiwa kuwaduwaza Al hilal kwa kutumia mapungufu waliyonayo ya kutokuwa na muunganiko, Nawaona st george awana washambuliaji hatari aina ya mayele kitu ambacho safu ya ulinzi ya yanga haitokuwa na kazi ngumu ya kufanya, yote kwa yote najua tiyali kuna shushushu wa yanga ndani ya dimba pale ethiopia akifuatilia kwa ukaribu mechi hii na ninamuona kocha Nabi akifanya home work yake vizuri sana kuelekea mechi dhidi ya wapinzani wake hawa