Spika wa Mombasa akamatwa na Polisi katika Maandamano

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
rajwayi.jpg


SPIKA wa Bunge la Kaunti ya Mombasa, Thadeus Rajwayi (pichani) na memba wa kaunti hiyo anayewakilisha Junda, Paul Onje ni baadhi ya watu takribani 10 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia kushiriki maandamano ya kupinga tume huru ya uchaguzi ya Kenya (IEBC), yaliyofanyika asubuhi ya leo mjini Mombasa.

Wawili hao walitiwa nguvuni baada ya Polisi kupiga mabomu ya machozi katika jaribio la kuwatawanya waandamaji kutoka muungano wa Upinzani wa CORD ambao wanapinga uwepo wa maafisa wa IEBC ofisini kwa madai kwamba hawana sia ya kuendelea kukaa ofisini.

Kabla ya kukamatwa kwao kulitokea purukushani kati ya waandamaji na Polisi huku kukiwa na taarifa za awali kuwa zoezi hilo lingefanyika bila kuwepo kwa aina yoyote ya ghasia.

Mamia ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Uhuru Gardens mjini Mombasa kuanzia majira ya saa 1:00 asubuhi tayari kwa ajili ya maandamano ya kuishinikiza Serikali kuridhia kuivunjilia mbali IEBC au kulazimisha maafisa wa tume hiyo kujiuzulu. Polisi nao walikuwa chonjo kukabiliana na matukio yoyote ya uvunjifu wa amani.

Hata hivyo, Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho, Wabunge Abdulswamad Shariff Nassir (Mvita), William Kamoti (Rabai) na Rashid Bedzimba (Kisauni), walifanikiwa kuongoza kile kilichoonekana kuwa ni maandamano ya amani kutoka Bustani ya Uhuru (Uhuru Gardens) kuelekea hadi kwenye ofisi za IEBC zilizoko maeneo ya Barabara ya Nkurumah (Nkurumah Road).

Ameandika Fadhili - Spika wa Mombasa akamatwa na Polisi katika Maandamano « SAUTI KUU l The Voice of East Africa
 
Back
Top Bottom