SPIKA: Tumesitisha kufanya kazi na CAG. Panga pangua Kamati za Bunge yaanza

Wakati tukisubiri tarehe 21.01.2019 kuripoti kuhojiwa, Spika amesitisha kufanya kazi na CAG!

Tutafakari:
-Je, Spika hajakiuka katiba na sheria?
-Je, CAG ataenda kuhojiwa na nani wakati Spika amesitisha kufanya kazi naye?
-Je, CAG ameshajibu kuwa hatoenda?
-Ripoti za ukaguzi za CAG zitakuwa zinawasilishwa wapi?
-Kwanini kamati zipanguliwe?
View attachment 995809
View attachment 995810
Jibu sasa ni wazi.Mheshimiwa hsmaki take ilikuwa in Ku implement mpango ambao ulishapangwa.Sad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wakati Escrow inatokea CAG alikuwepo? Au alikuwa likizo? Mbona ofisi ya CAG ikishirikiana na NAO wanaomba na kupokea rushwa wakati wa kuandaa taarifa zao kila Mwaka?
Braza tunajua unatetea ulaji hufanyi haya kwa mapenzi yako lakini kuna muda inabidi usimame na Taifa haya MaCCM Machadema yatapita ila Tanzania itaendelea kuwepo. Je, tutakuwa na nchi ya namna gani huko mbele ikiwa tu ofisi ya CAG ilipewa ushirikiano na mafisadi wakafanya yao.Serikali hii unayoitetea inawafahamu vyema lakini ni nani aliyeshughulikiwa hadi sasa?! Sasa imagine Maishs bila ushirikiano wa CAG?! Kama una akili timamu utagundua tunaenda kuweka rekodi ya ufisadi ambayo haijawahi tokea tangu uhuru wa Nchi hii.
 
Msitishike na tangazo la Spika kutishia kusitisha kufanya kazi na ofisi ya CAG, zile kanuni za Bunge zinamdanganya, hana uwezo huo anaodhani anao. Ofisi ya GAG ipo kwa mujibu wa katiba, ukaguzi utaendelea na ripoti ya CAG itawasilishwa Bungeni na lazima ipokelewe.
P

Umejiuliza uthubutu huo wa Job wa kuvunja katiba anautoa wapi? big malicious hidden behind?
 
Watanzania baadhi ni wapumbavu sana na haya majizi na mafisadi yanautumia upumbavu wao kufanya maovu wayatakayo hawana hata chembe ya woga.

Hatuna wabunge katika nchi hii. Tuna mfano wa wabunge. Ni aibu kwa wananchi wa Tanzania kwa kuchagua wabunge wa aina hii. AIBU KUBWA SANA WABUNGE WANAOTAKIWA WASEMEE WANANCHI, WAO WANASEMEA SERIKALI.
 
Msitishike na tangazo la Spika kutishia kusitisha kufanya kazi na ofisi ya CAG, zile kanuni za Bunge zinamdanganya, hana uwezo huo anaodhani anao. Ofisi ya GAG ipo kwa mujibu wa katiba, ukaguzi utaendelea na ripoti ya CAG itawasilishwa kwanza kwa rais Kisha ndani ya siku saba za kikao cha mwezi April, itawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba ya nchi na lazima ipokelewe, wether Spika anapenda au hapendi.

CAG anakuwa amemaliza kazi yake na ametimiza majukumu yake, sasa kama Bunge litaamua kuijadili au kuikalia, sasa hili sio la CAG, ikitokea Bunge likaamua lisijadili huo sasa ndio utakuwa uthibitisho wa alichokisema CAG.

P
 

Attachments

  • images(3).jpg
    images(3).jpg
    19.7 KB · Views: 34
Kama kuna wakati muhimu sana wa Watanzania kuonyesha kwamba hatuukubali ujinga na maovu yanayoendelea nchini basi wakati huo ni huu.

Hawa wahuni wakiweza kulifanya hili huku Watanzania especially wale wapumbavu kuendelea kumuunga mkono huyo dikteta basi nchi yetu itaingia kwenye giza nene sana katika miaka iliyo mbele yetu.
 
Back
Top Bottom