Special Thread ya Dar Mpya: Paul Makonda afanya Ziara Jijini la Dar kusikiliza kero za wananchi

Iringa wanalima Chai,

Tabora wanalima Tumbaku,

Mbeya wanalima Mpunga.

Morogoro wanalima Miwa,

Tanga wanalima matunda na Mkonge,

Dar es Salaam wanalima nini?

Makonda nakubaliana na wewe, ifute tu maana ipo sehemu kimakosa.
Asilimia 80% ya maafisa kilimo wako mkoa wa Dar es Salaam. Mkoa wa wa Dar es Salaam eneo lake ni mji wa Dar es Salaam tu. Sheria za nchi haziruhusu watu kulima mjini. Cha ajabu maafisa kilimo wako mijini tu.

Makonda kauona ukweli huu. Hivyo wizara husika iwahamishe watalaam hawa wakilimo kwenye mikoa inayolima hasa ile big 5: Sumbawanga, Ruvuma, Tabora, Mtwara, Songea na Kahama.
 
Asilimia 80% ya maafisa kilimo wako mkoa wa Dar es Salaam. Mkoa wa wa Dar es Salaam eneo lake ni mji wa Dar es Salaam tu. Sheria za nchi haziruhusu watu kulima mjini. Cha ajabu maafisa kilimo wako mijini tu.

Makonda kauona ukweli huu. Hivyo wizara husika iwahamishe watalaam hawa wakilimo kwenye mikoa inayolima hasa ile big 5: Sumbawanga, Ruvuma, Tabora, Mtwara, Songea na Kahama.
Mkuu hicho ndio kitu nilichobishania muda si mrefu uliopita.
Watu wanang'ang'ania wabaki Dar ilhali hakuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Idara za kilimo zilizopo Dar zote zihamishiwe mikoani.
 
Kuwa na wataalamu ni jambo moja, kuwaajari wataalamu ni jambo lingine. Serikali imebana ajira kwahiyo kwao kukaa mitaani ni jambo lisilokwepeka bila kujalisha wanahitajika kwa kiasi gani.

Lakini kwa hawa waliopo kwenye mfumo wa ajira, wapelekwe penye uhitaji zaidi.Wakishatosheleza mikoani basi wanaweza kufanya kazi popote hata pale K/koo.
Ukishasema hivyo rejea sasa kauli ya mkuu wa mkoa. Hebu soma heading... yeye anasema anafuta kabisa idara hiyo na kuwafukuza kazi waliopo. Nadhani utakuwa umeshanielewa sasa...
 
Mh makonda na ziara zake za jiji la dar es salaam ni kutaka kuurudisha mkoa kwa chama cha tawala 2020 na ni siasa dhahili.... Kutaka kuwaaminisha wana dar es salaam kwamba walifanya makosa kukiondoa madarakani
Angalia maeneo ambayo ametembelea yaliyowachagua wapinzani Kama si mwenyekiti wa mtaa au diwani cha moto wamekiona viongozi
Lakini sehemu ambazo ccm imeshinda huwa wanafanya vikao kwanza na serikali ya mtaa au kata mfano alipokuja kata ya mburahati mh alikutana na viongozi kwanza alafu jioni ndo mkutano ili iweje sasa
 
Ni kweli mkuu, mara shisha, mara mashoga, mara madanguro, mkuu Makonda, ungeanza na tatizo la maji, dar ni shida,sio leo hiki, Kesho kile, kwenye vyombo vya habari mkuu.
 
hoyooooooooooo hawa jamaa wanazani watu wapo wapo tu ee ? Hata hawajui kuna sheria zinazomlinda mfanyakazi asee trip hii sijui watapata wapi pesa za kuwalipa watu kwa ku sitisha mikataba kichwa kichwa
 
Hili jamaa na akili zake zilizokaa kushoto kama matege yake na domo kubwa kama bakuli, halijitambui, nipeni Cv yake
 
Wakuu wa mikoa nchi nzima wakianza kutoa matamko ya kipuuzi hama haya, hii nchi itaeleweka kweli? Halafu kwa nini agenda kubwa safari hii ni watumishi wa serikali, wamewafanya nini hawa watu mpaka mkawachukia kiasi hiki..
 
Tatizo kubwa ninaloliona kwa watz wengi ni kulinganisha uongozi mmoja na mwingine. Hakuna uongozi duniani unaofanana. Siku zote rais mpya akiingia kutakuwa na tofauti ya maelekezo.
Mzee mwinyi aliwahi kusema kila kitabu na enzi yake.
Ni vema tukakubali haya yanayoyendeka sasa kwa kuwa wataalamu wa menejimenti wanasema hakuna njia moja ya kuongoza.
eea8e0395f27c4653587702b232d4d32.jpg
 
Binafsi ninaona mtindo anaoufanya Makonda atatumia gharama kubwa sana za uendeshaji mfano kuilipa Clouds, kununua mafuta ya gari na kuyafanyia service magari, wakati kuna kazi anatakiwa kuzifanya mfano kudhibiti Shisha (akimaliza aufikirie ujambazi).

Akiwa King'azi ametoa namba ya simu ya kuripoti utendaji mbovu wa wenyeviti wa serikali za mitaa, hiki ndicho kilitakiwa kufanywa tangu mwanzo, kuwe na vyombo ambavyo vitakua na kazi ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi mfano email, fax, namba za simu, dawati la huduma kwa mwananchi n.k.
Hzo namba au mawasiliano ya kupokea malalamiko yawe yanafanyiwa kazi, kuna kpnd nlienda amana hosptal kwenye sanduku la maoni pamejaa, mhudumu wa usafi akasema kaka usijisumbue huwa wanafungua wanachukua chache nyngne wanatupa
 
Shida iko hapa, Makonda kampigia Magufuli simu live wakaongea kuhusu hizo kero na maelekezo yakatolewa kwa simu kupitia hicho kituo binafsi cha redio
Ukiwa na chuki na mtu au Chama unapoteza umakini, utakua na ushahuri zaidi ya kulalamika, je makonda ndio aliepiga simu au umeamua binafsi tu ili upate uhalali wa kushutumu
 
Ukiwa na chuki na mtu au Chama unapoteza umakini, utakua na ushahuri zaidi ya kulalamika, je makonda ndio aliepiga simu au umeamua binafsi tu ili upate uhalali wa kushutumu
Adharusi rafiki tafuta ile clip iko mitandaoni isikilize, yasikilize yale mazungumzo kisha rejea hapa tafadhali nitakuwa nakusubiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom