Songwe: RC Dkt. Francis Michael, ameviagiza vyombo vya ulinzi kuanza kuwachukulia kwa waliotafuna Mil 400 za Machinga Tunduma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
RC SONGWE AAGIZA WALIOTAFUNA MILIONI 400 ZA MRADI WA MACHINGA TUNDUMA KUKAMATWA.

TUNDUMA: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael ameviagiza vyombo vya ulinzi kuanza kuwachukulia hatua kali watu wote ambao wamejihusisha na usimamizi wa ujenzi wa soko la machinga Tunduma ambalo Serikali kuu ilileta fedha milioni 380 za awali na Halmashauri ya mji Tunduma ikaongeza milioni 20 za kuchimba kisima cha maji.

Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Francis Michael amechukua hatua hiyo baada kukuta mradi wa soko la machinga ukiwa ujenzi umesimama na fedha milioni 400 za ujenzi zikiwa zimeisha uku miundombinu iliyopo haiendani na thamani ya fedha ya milioni 400.

"Haiwezdkani Mheshiniwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan analeta fedha kwa ajili ya wamachinga alafu wanatokea watu wachache wanakula fedha izi hii haikubariki lazima sheria ichukue hatua kali dhidi ya watu hawa" Mhe. Dkt. Francis Michael Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Mji Tunduma imeteja kuwa matumizi ya fedha ambazo zimekuwa na shaka kubwa ni Manunuzi ya mchanga na kokoto milioni 114 kiasi ambacho hakiendani na uhalisia, malipo ya bidhaa ambazo hazikupokelewa katika eneo la ujenzi wa soko milioni 113 na malipo ya fundi milioni 62 kabla ya shughuli za ujenzi kuanza, malipo ya milioni 203 bila kuwepo kwa mitasari ya Kamati mbalimbali pamoja na vifaa vya milioni 18 vilivyonunuliwa bila kuingizwa kwenye daftari ya kumbukumbu.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael ameagiza vyombo vya ulinzi kuchukua hatua dhidi ya watu wote ambao wamesimamia ujenzi wa soko la machinga Tunduma.

"Fedha zote za miradi ya maendeleo tunatakiwa kuzisimamia ipasavyo na mtu yeyote awe mtumishi wa umma au mwananchi wa kawaida atakayehusika na ubadhilifu wa fedha lazima hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake" Mhe. Dkt. Francis Michael.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanamlinda mkaguzi wa ndani, Bwn. Thomas Mzee aliyebaini changamoto za mradi huo ili asizuruke na jambo lolote.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Bwn. Philemon Magesa amesema baada ya kuona mradi huo unachangamoto alichukua hatua ya kuwasimamisha kazi mtalamu wa Manunuzi na Mhandisi wa Halmashauri kwa ajili ya uchunguzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Fakii Lulandala amesema tayari Kamati ya Ulinzi na Usalama imeanza kufanya mahojiano maalumu kwa watu wote ambao wametakiwa au kuhusika na mradi huo.
IMG-20230511-WA0015.jpg
 
Wizi wa kwenye makaratasi ni mbaya sana aisee.

Kelele zinaweza kuwa nyingi kama hivi ila matokeo yake yasiwe vile inavyotakiwa maana kuthibitisha wizi Huwa ni kazi hasa kama tayari majengo yapo.

Mwisho kama ni kweli hakuna nyaraka za manunuzi hao watu wapandishwe kizimbani haraka sana.
 
Hivi kuna kiongozi yeyote ambaye hajawahi kushiriki wizi na ufisadi kwa namna yoyote ile?
 
Nadhani ifike wakati watanzania kwa pamoja kuamka na kuanza kupinga vitu kama hivi ikiwezekana kwa maandamano. Kuonyesha hisia kwa pamoja kwa walio madarakani kuwa kodi zetu tunazochanga sio pesa zao binafsi. Maana imeshazoeleka watu wanaiba pesa na kusema takukuru fanyeni uchunguzi. Na baada ya hapo hamna kinachoendelea.

Hii inafanya tuamini kuwa wapigaji wanacheza michezo kama hiii wakishirikiana na takukuru.
Na ndio maana hamna kinachoendelea na wapigaji wanaendelea kupiga bila kuchukuliwa
hatua au hata kufilisiwa.

Ebu angalia hivyo vyumba viliwi sijui vitatu vimejengwa kwa Shiling Milioni 441. Na anayeulizwa anajibu kwa confidence kuwa kuna wizi na takukuru wanasema ndio tuko kwenye uchunguzi mwezi wa pili unakwenda wa tatu . Hii inaashiria na wao wanakitu nyuma ya pazia au?

Hizi pesa ni nyingi sanaa na ni kodi zinakatwa kwenye miamala, kodi za masoko, kodi za mafuta, kodi za makato kwenye benki , kodi za simu nk. Na watu wachache wanakula bila huruma.

Mimi naona watanzania inabidi tupinge kwa pamoja upigaji kwa huu. Kodi zetu zitumike kuleta maendeleo na sio blah blah za wamekala, takukuru mwisho ndio wamekula na wanaendelea na kazi.

Inasikitisha sanaaa .....!! Au wadau mna mtazamo gani?
 
"Fedha zote za miradi ya maendeleo tunatakiwa kuzisimamia ipasavyo na mtu yeyote awe mtumishi wa umma au mwananchi wa kawaida atakayehusika na ubadhilifu wa fedha lazima hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake" Mhe. Dkt. Francis Michael.
Wongo mtupu, mbona waliodalalia ndege bado wapo wanakula kiyoyozi humo maofisini.
 
Back
Top Bottom