Somaliland waihonga bandari Ethiopia kutambuliwa kama nchi.

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,681
46,362
Eneo la Somaliland liliojitenga kutoka Somalia tangu mwaka 1991 limekuwa likijiendesha kama taifa bila kutambuliwia rasmi na nchi yoyote duniani.

Hali hii ya kutotambulika sasa inaonekana kuelekea mwisho baada ya kuingia katika makubaliano ya awali na Ethiopia yalipo makao makuu ya AU kuipatia Ethiopia sehemu ya bandari yake kwa miaka 50 kwa mashariti ya Ethiopia kuitambua Somaliland kama nchi rasmi.

Ethiopia ni taifa kubwa zaidi duniani lisilo na bandari tangu Eritrea kujitenga na taifa hilo miaka 30 iliyopita. Tangu waziri mkuu Abiy Ahmed kuingia madarakani amekuwa akitoa kauli za mara kwa mara kwamba Ethiopia itafanya lolote linalowezekana chini ya utawala wake kujipatia bandari na kuwa na jeshi la majini.
 
Huyo Abiy Ahmed tunamuhitaji huku,haogopi chochote yeye Ethiopia mbele,mikwara yote ya Misri wamesanda Kwa huyo Jamaa.
Abiy mwanzo nilikua simuelewi kabisa yule jamaaa
Ila jamaa hasikilizi la mtu bwawa lile misri walipiga kelele kwa bwawa lile mwisho wakaufyata
Tigray na amhara watu wamepiga kelele jamaa anabonda tuuu
Kwahakika Ethiopia ipo kwa mtu mwenye fikra sahihi juu ya Ethiopia
 
Back
Top Bottom