Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,707
- 5,111
Mimi kama muhaya, nshomile kutoka Uhayani Republic, imenibidi niingie chimbo kuleta maelezo kamili juu ya hii vita ya Israel na palestina ambayo kuna watu wanadhani Gaza inapigwa kwa bahati mbaya. Ukisoma maandiko ya agano la Kale (Old Testament) katika biblia na vitabu vya kiyahudi Torah na Tanakh. Utagundua kuwa Gaza ilitakiwa kubondwa tangu enzi na enzi kwa mujibu wa maandiko. Vita vya Israel na Palestina, vinaanza tangu enzi za zama za Wafilisti na Wana wa Israel, na chanzo kikuu cha vita ya waisraeli na wafilisti kugombana ilikuwa ni kwa sababu ya Ardhi, Rasilimali, na Ngome, na vita hivyo havikuwa na chanzo maalumu bali kugombania Ardhi na rasilimali. Vita vya hawa jamaa vimeorodheshwa kama ifuatavyo;
1. Vita ya Israel na Wafilisti ikiongozwa na Eli na watoto wake.
Ukisoma 1 Samwel 4:1-3, utaona namna vita vilipigwa baina ya wafilisti na waisraeli.
English
2. MFALME SAULI, MWANAE JONATHAN na WAFILISTI
Baada ya muda mrefu, utawala wa Mfalme Sauli ukaingia. Vita bado vikaendelea kupigwa balabala baina ya waisraeli na Wafilisti; katika kitabu cha 1 Samwel mlango wa 14-15 tunaona.
1 Samwel 14:47-52
3. DAUDI, GOLIATH na WAFILISTI
Katika kitabu cha 1 Samwel 17:1-53 Daudi ambaye alikuwa mchungaji wa mifugo anaonekana kwenda vitani kuwasalimia kaka zake, ndipo akamuoka Goliath ambaye ni mfilisti akiwadhiaki ndugu zake katika uwanja huo wa vita.
4. UNABII WA AMOS dhidi ya GAZA na NCHI JIRANI.
Angalia maandiko ya Biblia hapo chini namna Nabii Amos anavyoishutumu Gaza kwa udhalimu wake na kuitabiria kuwa Gaza na Jirani yeyote atakaye endelea na ujinga ujinga basi atapokea kichapo kikali.
Ukisoma kitabu cha Amosi 1:6-8 (Amos 1:6-8)
English
Kiswahili
UFAFANUZI: Amosi analaani mji wa Gaza kwa vitendo vyake vya zamani, hususani kwa kuteka jamii nzima na kuziuza kwa Edomu. Unabii huo unatabiri adhabu ya Mungu kwa namna ya adhabu ya moto (sijui ndio haya mabomu) juu ya kuta na ngome za jiji hilo kama adhabu matendo yao. Hii ni sehemu ya mfululizo wa unabii katika Amosi 1 unaozungumzia mataifa mbalimbali jirani, ukigusia udhalimu na vitendo vyao viovu na kadhia watakayokumbana nayo kutokana na mipango yao dhidi ya Israel. Ndio maana mwaka 1948 Israel ilizikunguta nchi zote za kiarabu zilizoungana kumshambulia hapa nazungumzia Misri, Lebanon, Syria, na zote zilizoshiriki katika vita hile ya mwaka 1948 inayoitwa Israel-Arab war. Unabii bado unaendelea.
5. MFALME HEZEKIA kuwatandika wafilisti na kuchukua eneo la GAZA
Vile vile ukisoma tena kitabu cha; 2 Wafalme 18:8 (2 Kings 18:8)
English
Kiswahili
UFAFANUZI: Mstari huu ni sehemu ya simulizi la kihistoria la Mfalme Hezekia wa utawala wa Yuda na kampeni zake za kijeshi. Inataja kutekwa kwa eneo la Wafilisti, na eneo la mji wa Gaza, na Mfalme Hezekia. Muktadha mpana wa tukio hili ni kwamba Mfalme Hezekia wa Yuda alitafuta kuimarisha na kulinda ufalme wake. Gaza ulikuwa mji katika eneo la Wafilisti, ambao walikuwa adui wa muda mrefu wa Waisraeli na Wayuda. Kampeni ya kijeshi ya Mfalme Hezekia katika eneo hilo, ambayo ilijumuisha Gaza, inaweza kuwa sehemu ya juhudi pana za kulinda mipaka ya ufalme wake na kudhibiti udhibiti wa eneo hilo. Sababu maalum au vitendo vilivyosababisha kampeni hii hazijaelezewa kwa kina katika maandishi ya kibiblia.
6. SAMSON na GAZA
Vilevile tunaona kwenye kitabu cha waamuzi wafilisti wa mji wa Gaza wakipokea kichapo kutoka kwa Samson, baada ya kupata mwanamke katika mji huo.
Waamuzi 16:1-4 (Judges 16:1-4)
English
Kiswahili
UFAFANUZI: Mstari huu ni sehemu ya hadithi ya Samsoni, mmoja wa Waamuzi wa Israeli, na inasimulia ziara yake katika jiji la Gaza. Waamuzi 16, inatajwa kwamba Samsoni alienda Gaza, na huko akamwona kahaba. Akiwa Gaza, alijihusisha na matukio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubeba milango ya jiji hadi juu ya kilima. Matendo yake huko Gaza ni sehemu ya simulizi kubwa zaidi la maisha ya Samsoni na kukutana kwake na Wafilisti, ambao walikuwa maadui wa Waisraeli wakati huo. Safari ya mwisho ya Samsoni lilifanyika huko Gaza. Alifia huko Gaza, karibu na mahali alipokuwa ametekwa na Wafilisti. Kifo cha Samsoni kinafafanuliwa katika Waamuzi 16:21-30, ambapo aliangusha hekalu la mungu wa Wafilisti Dagoni, akiwaua Wafilisti wengi, akiwemo na yeye mwenyewe, katika mchakato huo.
HITIMISHO: Mji wa kale wa Gaza ulikuwa katika eneo linalolingana na sehemu ya Gaza ya hivi leo. Kwa maelfu ya miaka, jiji na mazingira yake yamekumbwa na mabadiliko na maendeleo mengi, lakini marejeo ya kibiblia ya Gaza kwa ujumla yanarejelea mji wa kihistoria na eneo pana zaidi la mji huo mkongwe. Gaza ya leo iko katika eneo la linalosemekana ndio lililokuwa jiji la kale la Gaza, na miunganisho ya kihistoria na maandiko ya Biblia inasalia katika muktadha huo wa kijiografia kuwa Gaza ya leo ndio Gaza ya Kale.
Wafilisti wa nyakati za kale si sawa na Wapalestina wa leo. Neno "Wafilisti" linarejelea watu wa kale walioishi katika eneo la Kanaani, ambalo liko karibu na eneo la Israeli ya kisasa na maeneo ya Palestina, na vile vile sehemu za Gaza ya leo, maeneo haya waliishi wafilisti. Walitajwa katika Biblia ya Kiebrania na walijulikana kwa migogoro yao ya muda mrefu na Waisraeli wa kale.
Wapalestina wa kisasa ni wakazi wenye asilimia ya Kiarabu wanaoishi katika eneo hilo linalojumuisha Ukingo wa Magharibi (West Bank), Ukanda wa Gaza (Gaza strip), na sehemu za Israeli. Neno "Wapalestina" kimsingi linamaanisha wakazi wa Kiarabu wa maeneo haya. Ingawa majina yanafanana kwa kiasi fulani kutokana na eneo la kijiografia, mazingira ya kihistoria na kiutamaduni ya Wafilisti na Wapalestina wa kisasa ni tofauti. Wafilisti walikoma kuwepo kama watu wanaotambulika zamani, jamii yao ilipotea, wakati Wapalestina wa kisasa ni watu tofauti wenye historia na utambulisho wao wa kiarabu.
1. Vita ya Israel na Wafilisti ikiongozwa na Eli na watoto wake.
Ukisoma 1 Samwel 4:1-3, utaona namna vita vilipigwa baina ya wafilisti na waisraeli.
English
Kiswahili1. And the word of Samuel came to all Israel. Now Israel went out against the Philistines to battle, and pitched beside Ebenezer: and the Philistines pitched in Aphek.
2 And the Philistines put themselves in array against Israel: and when they joined battle, Israel was smitten before the Philistines: and they slew of the army in the field about four thousand men.
3 And when the people were come into the camp, the elders of Israel said, Wherefore hath the LORD smitten us to day before the Philistines? Let us fetch the ark of the covenant of the LORD out of Shiloh unto us, that, when it cometh among us, it may save us out of the hand of our enemies.
UFAFANUZI: Miaka hiyo Eli na wanawawe, waliingia vitani na wafilisti, vita vikapigwa kweli kweli. Waisraeli wakiongozwa na Eli na wanawawe wawili wakashindwa vita. Watoto wakiume wa Eli ambao walikuwa mashujaa wakauwawa na wafilisti, Sababu za kushindwa kwa Eli ni kutokuwa na Imani thabiti. Vita vikaendelea kwa miaka mingi, waisraeli wakiendelea kuchezea kichapo. Mpaka ufalme wa Sauli.1. kawa siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na Israeli, nao Waisraeli wakatoka juu ya Wafilisti kwenda vitani;wakatua karibu na Ebenezeri ,nao Wafilisti wakatua huko Afeki.
2 Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne.
3 Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona Bwana ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la Bwana toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.
2. MFALME SAULI, MWANAE JONATHAN na WAFILISTI
Baada ya muda mrefu, utawala wa Mfalme Sauli ukaingia. Vita bado vikaendelea kupigwa balabala baina ya waisraeli na Wafilisti; katika kitabu cha 1 Samwel mlango wa 14-15 tunaona.
1 Samwel 14:47-52
UFAFANUZI: Sauli na mwanaye wa kiume Jonathan waliendelea kupigana vita dhidi ya wafilisti. Na wakawa wanashinda kwa sababu walikuwa wanamtumikia Mungu. Vita viliendelea mpaka badae akaibuka Goliath.47 Basi Sauli alipokwisha kuutwaa ufalme juu ya Israeli, alipigana na adui zake zote pande zote, juu ya Moabu, na juu ya wana wa Amoni, na juu ya Edomu, na juu ya wafalme wa Soba, na juu ya Wafilisti; na po pote alipogeukia, akawashinda.
48 Naye akatenda kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli katika mikono yao waliowateka nyara.
49 Basi, wana wa Sauli walikuwa ni hawa, Yonathani, na Ishvi, na Malkishua; na majina ya binti zake wawili yalikuwa haya; jina lake wa kwanza aliitwa Merabu, na jina lake mdogo aliitwa Mikali;
50 na jina lake mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu, binti Ahimaasi. Tena, jina la jemadari wa jeshi lake aliitwa Abneri, mwana wa Neri, aliyekuwa baba mdogo wa Sauli.
51 Na Kishi, babaye Sauli, na Neri, babaye Abneri, walikuwa wana wa Abieli.
52 Tena, kulikuwa na vita vikali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu ye yote aliyekuwa hodari, au mtu ye yote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.
3. DAUDI, GOLIATH na WAFILISTI
Katika kitabu cha 1 Samwel 17:1-53 Daudi ambaye alikuwa mchungaji wa mifugo anaonekana kwenda vitani kuwasalimia kaka zake, ndipo akamuoka Goliath ambaye ni mfilisti akiwadhiaki ndugu zake katika uwanja huo wa vita.
UFAFANUZI: Vita iliisha kwa daudi kuwa mshindi, na badae baada ya kifo cha mfalme Sauli, kwa mujibu wa unabii wa Samwel ilitakiwa Daudi ndio arithi ufalme huo kutokana na watoto wa Sauli wote kuuwawa vitani na wafilisti. David anafanikiwa kuwa mfalme ya Yuda, na badae biblia inaeleza David alikuwa nguli wa Vita, katika enzi za ufalme wake alizikunguta falme za Wafilisti vibaya mno na kufanikiwa kuteka maeneo yote ya Israel na kuziunganisha tawala zote kuwa chini yake, na Yerusalemu ndio ukawa mji mkuu. Tokea hapo wafilisti wakawa wanakula kichapo tu. Baada ya kifo cha Mfalme Daudi, mwanawe Sulemani alimrithi kwenye kiti cha enzi. Sulemani akawa mfalme wa tatu wa Israeli na akatawala kwa muda mrefu. Anajulikana kwa hekima yake, utajiri, na kwa kujenga Hekalu la Kwanza huko Yerusalemu. Utawala wa Sulemani mara nyingi huonekana kama kipindi cha ufanisi mkubwa katika historia ya Israeli.33 Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake.
34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi,
35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua.
36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.
37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe.
38 Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii.
39 Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua.
40 Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti.
41 Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri.
43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.
44 Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.
45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti.
49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.
51 Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia.
4. UNABII WA AMOS dhidi ya GAZA na NCHI JIRANI.
Angalia maandiko ya Biblia hapo chini namna Nabii Amos anavyoishutumu Gaza kwa udhalimu wake na kuitabiria kuwa Gaza na Jirani yeyote atakaye endelea na ujinga ujinga basi atapokea kichapo kikali.
Ukisoma kitabu cha Amosi 1:6-8 (Amos 1:6-8)
English
Kiswahili
6. Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu;
7. lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake.
8. Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU."
UFAFANUZI: Amosi analaani mji wa Gaza kwa vitendo vyake vya zamani, hususani kwa kuteka jamii nzima na kuziuza kwa Edomu. Unabii huo unatabiri adhabu ya Mungu kwa namna ya adhabu ya moto (sijui ndio haya mabomu) juu ya kuta na ngome za jiji hilo kama adhabu matendo yao. Hii ni sehemu ya mfululizo wa unabii katika Amosi 1 unaozungumzia mataifa mbalimbali jirani, ukigusia udhalimu na vitendo vyao viovu na kadhia watakayokumbana nayo kutokana na mipango yao dhidi ya Israel. Ndio maana mwaka 1948 Israel ilizikunguta nchi zote za kiarabu zilizoungana kumshambulia hapa nazungumzia Misri, Lebanon, Syria, na zote zilizoshiriki katika vita hile ya mwaka 1948 inayoitwa Israel-Arab war. Unabii bado unaendelea.
5. MFALME HEZEKIA kuwatandika wafilisti na kuchukua eneo la GAZA
Vile vile ukisoma tena kitabu cha; 2 Wafalme 18:8 (2 Kings 18:8)
English
7. And the LORD was with him; and he prospered whithersoever he went forth: and he rebelled against the king of Assyria, and served him not.
8. He smote the Philistines, even unto Gaza, and the borders thereof, from the tower of the watchmen to the fenced city.
Kiswahili
7. Naye Bwana akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia.
8. Akawapiga Wafilisti mpaka Gaza na mipaka yake, tangu mnara wa walinzi hata mji wenye boma."
UFAFANUZI: Mstari huu ni sehemu ya simulizi la kihistoria la Mfalme Hezekia wa utawala wa Yuda na kampeni zake za kijeshi. Inataja kutekwa kwa eneo la Wafilisti, na eneo la mji wa Gaza, na Mfalme Hezekia. Muktadha mpana wa tukio hili ni kwamba Mfalme Hezekia wa Yuda alitafuta kuimarisha na kulinda ufalme wake. Gaza ulikuwa mji katika eneo la Wafilisti, ambao walikuwa adui wa muda mrefu wa Waisraeli na Wayuda. Kampeni ya kijeshi ya Mfalme Hezekia katika eneo hilo, ambayo ilijumuisha Gaza, inaweza kuwa sehemu ya juhudi pana za kulinda mipaka ya ufalme wake na kudhibiti udhibiti wa eneo hilo. Sababu maalum au vitendo vilivyosababisha kampeni hii hazijaelezewa kwa kina katika maandishi ya kibiblia.
6. SAMSON na GAZA
Vilevile tunaona kwenye kitabu cha waamuzi wafilisti wa mji wa Gaza wakipokea kichapo kutoka kwa Samson, baada ya kupata mwanamke katika mji huo.
Waamuzi 16:1-4 (Judges 16:1-4)
English
1. Then went Samson to Gaza, and saw there an harlot, and went in unto her.
2. And it was told the Gazites, saying, Samson is come hither. And they compassed him in, and laid wait for him all night in the gate of the city, and were quiet all the night, saying, In the morning, when it is day, we shall kill him.
3. And Samson lay till midnight, and arose at midnight, and took the doors of the gate of the city, and the two posts, and went away with them, bar and all, and put them upon his shoulders, and carried them up to the top of an hill that is before Hebron.
4. And it came to pass afterward, that he loved a woman in the valley of Sorek, whose name was Delilah.
Kiswahili
"1. Kisha Samsoni akaenda Gaza, akamwona kahaba, naye akaingia kwake.
2. Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.
3. Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
4. Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila.