Soma hii kama una upungufu wa Damu Mwilini

Dr isaya febu

Member
Jan 17, 2023
25
219
Ikiwa una changamoto ya upungufu wa damu mwilini zingatia mambo yafuatayo.

1) Usitumie Kahawa, chai wakati wa kula chakula au kunywa dawa za kuongeza damu kwa sababu kahawa/chai huzuia ufyonzwaji (absorption) wa madini chuma kuingia ndani ya mwili.

2) Badala yake tumia vyakula vyenye vitamin C kama vile chungwa, limao , chenza kwa sababu husaidia mwili kufyonza (absorb) madini chuma ya kwa urahisi.

Kumbuka:
Unaweza ukawa na ulaji mzuri wa vyakula vyenye madini ya chuma, lakini kwa sababu ya utumiaji wa kahawa/chai madini ya chuma yakashindwa kufyonzwa vyema tumboni, vilevile upungufu wa Vitamin C ukadhoofisha ufyonzwaji wa madini ya chuma mwilini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom