Soka la Tanzania limekua au soka la Afrika limeshuka?

Marcovicsavic

Senior Member
Nov 14, 2020
130
298
Kwa miaka mingi sana vilabu kutoka Tanzania vimekua si lolote si chochote kwenye soka la Afrika mpaka pale Simba SC walipo kata utepe kwa ku Qualify Group stage, kwa umri wangu ndio mara ya kwanza niliona klabu ya Tanzania kuingia group stage licha ya kwamba miaka yote alikuwepo bingwa alie enda kushiriki.

Baanda ya miaka kadhaa kwa Simba SC kuendelea kutamba huko kumataifa tumewaona Yanga Sc na wao waki anzisha utawala wao kiasi cha kutinga mpaka fainali shirikisho barani Africa.

Msimu huu timu zote mbili zinawania tiketi ya kwenda clabu bingwa makundi, ila tayari Yanga kasha weka mtaji wa ushindi wa goli mbili igenini huku simba wao wakitoka sare na goli mbili za away.

Kwa hesabu za kawaida ni kama Yanga amesha fuzu na simba wana zaidi ya nusu ya asilimia kufuzu makundio.

Kwa mantiki hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Tanzania inapeleka vilabu viwili makundi ya clabu bingwa Afrika.

Wengi wanachukulia wepesi hili jambo ila sio jambo la kuchukulia wepesi kabisa. Hii ni zaidi ya achievement.

Swali ambalo nime jiuliza na kukosa majibu haya yanayo endelea ni kwasbabu ya kukua kwa soka la Tanzania au, soka la Afrika limeshuka so na watanzania wana serereka huko?

Kuna siku Yanga na Simba watakutana huko clabu bingwa kwenye mtoano, iwe robo au nusu, au fainali, na hapo ndio patakapo chimbika bila jembe.
 
Soka limekua,Timu znasajiri wachezaji wazuri sio kama miaka ile tunasajiri wachezaji kwa majaribio yote kwa yote mpira pesa na vilabu vimewekewa pesa na wadhamini pamoja na wamiliki

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
Upo sahihi mzee, inataka kusema mataifa kama kenya, uganda, rwanda hawa wekezi. Vya kutosha?
 
Mpira bongo kipindi ndio kulikuwa na mpira wa juu. Ila hakukuwa na wawekezaji, na hakukuwa na TV, Nyerere aliharamisha.

Siku hizi kuna uwekezaji timu zinanunua wachazaji kutoka nje
1692837056519.jpg
 
Upo sahihi mzee, inataka kusema mataifa kama kenya, uganda, rwanda hawa wekezi. Vya kutosha?
Hawawekezi vya kutosha ligi zao ni dhaifu timu zenye misuli ya fedha ni chache kusini mwa jangwa la sahara Tanzania ni ligi ya pili kwa kulipa vizuri baada ya Africa kusini,angalia singida ina profesheno 12 sio wakuokoteza ni wa maana yule Rupia aliyefunga goli jana alikua mfungaji bora kenye msimu uliopita,kuna mnigeria kiungo pale kati kacheza ribo final caf cc akiwa na Rivers msimu uliopita hayo hayajatokea kwa bahati mbaya ukiona wachezaji wwnhe profile kubwa kama wakina kazadi,onyango,wawa,kagere,Gyan, wanang'ania kubaki bongo ujue hela ipo

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa miaka mingi sana vilabu kutoka Tanzania vime kua si lolote si chochote kwenye soka la Africa mpaka pale Simba sc walipo kata utepe kwa ku Qualify Group stage, kwa umri wangu ndio mara ya kwanza niliona klabu ya Tanzania kuingia group stage licha ya kwamba miaka yote alikuwepo bingwa alie enda kushiriki

Baanda ya miaka kadhaa kwa Simba sc kuendelea kutamba huko kumataifa tumewaona Yanga Sc na wao waki anzisha utawala wao kiasi cha kutinga mpaka fainali shirikisho barani Africa

Msimu huu timu zote mbili zinawania tiketi ya kwenda clabu bingwa makundi, ila tayari Yanga kasha weka mtaji wa ushindi wa goli mbili igenini huku simba wao wakitoka sare na goli mbili za away

Kwa hesabu za kawaida ni kama Yanga amesha fuzu na simba wana zaidi ya nusu ya asilimia kufuzu makundio

Kwa mantiki hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Tanzania inapeleka vilabu viwili makundi ya clabu bingwa Afrika,

Wengi wana chukulia wepesi hili jambo ila sio jambo la kuchukulia wepesi kabisa.
Hii ni zaidi ya achievement,

Swali ambalo nime jiuliza na kukosa majibu haya yanayo endelea ni kwasbabu ya kukua kwa soka la Tanzania au, soka la Afrika limeshuka so na watanzania wana serereka huko,?

Kuna siku Yanga na Simba watakutana huko clabu bingwa kwenye mtoano, iwe robo au nusu, au fainali, na hapo ndio patakapo chimbika bila jembe,

Amini na penda vya kwako. Angalia:

  • Thaman ya usajili.
  • Thaman ya mauzo ya players.
  • Uwekezaji wa wazamani.
  • Hamasa ya washabiki.....

Soka la Tanzania limekua sana.
 
Kwa mantiki hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Tanzania inapeleka vilabu viwili makundi ya clabu bingwa Afrika,

Moja, Watanzania tujifunze kuwa na subira hadi pale tunapokuwa tumehakikisha jambo, hii ni moja ya tabia inayoturudisha nyuma kinoma...

Hakuna timu iliyofuzu bado, na hakuna sababu ya kurelax kwa sababu hizo mechi zimechezwa mkondo mmoja na bado mwingine...

Kama timu zenu zimeweza kudraw au kushinda ugenini, hata hao wageni wanaweza kushinda kwenu...

Mbili, sishangai kwa Simba au Yanga kufanya vizuri wakati unaona kabisa kwamba viongozi wao wamewekeza kwa kuleta wachezaji na wakufunzi wazuri...

Mathalani itazame safari ya Yanga ilipoamua kujenga timu yao tangu wakati ule Zahera anapewa timu, wakaja na kampeni kibao za kupitisha bakuli ili wanachama na mashabiki wao waji attach na timu yao, hivyo mafanikio unayoyaona kwa Yanga yametengenezewa njia kwa muda wa miaka 4, 5
 
Mpira unaendeshwa kwa hela nyingi sana,hivyo kwa miaka ya hivi karibuni kumekua na uwekezaji mkubwa kwa team kubwa kama Simba na Yanga,

Kingine ujio wa social media umewezesha watu wengi kufuatilia mpira wa nchi yao na kuwapa presha wachezaji wa team zao,hivyo wachezaji hujihisi kua wana deni la kulipa kwa shabiki zao na hivyo hijituma wanapokua uwanjani.
 
Upo sahihi mzee, inataka kusema mataifa kama kenya, uganda, rwanda hawa wekezi. Vya kutosha?
Mataifa uliyoyataja hayajawekeza vya kutosha, ukitaka kujua hilo tembelea mataifa hayo utakuta wachezaji wao wanatamani kuja NBCPL (au hata Championship) kufuata malisho bora. Kiufupi haya ni matunda ya uwekezaji. Singida FG nao kuna uwezekano wakaongeza idadi ya team za Tz zitazoingia makundi.
 
nON OF THE ABOVE. kama taifa stars inayumba yumba basi soka letu bado dogo saaaana Hivi vilabu sio vigezo vya soka letu kukua maana vina wachezaji karibia wote kutoka nje. sasa kama yanga kumshinda al merikh sio sifa ya kujivunia kukuwa kwa soka la nchi bali ni kulitangaza taifa letu ya kuwa na sissi wamo.
Taifa Stars inayumbaje wakati ndo team pekee ya Taifa kutoka EA iliyofuzu Afcon!?
 
nON OF THE ABOVE. kama taifa stars inayumba yumba basi soka letu bado dogo saaaana Hivi vilabu sio vigezo vya soka letu kukua maana vina wachezaji karibia wote kutoka nje. sasa kama yanga kumshinda al merikh sio sifa ya kujivunia kukuwa kwa soka la nchi bali ni kulitangaza taifa letu ya kuwa na sissi wamo.
Unaona Sasa umekosea Ungekaa kimya,sio kila kitu unakitolea maoni.
 
Kwa miaka mingi sana vilabu kutoka Tanzania vime kua si lolote si chochote kwenye soka la Africa mpaka pale Simba sc walipo kata utepe kwa ku Qualify Group stage, kwa umri wangu ndio mara ya kwanza niliona klabu ya Tanzania kuingia group stage licha ya kwamba miaka yote alikuwepo bingwa alie enda kushiriki

Baanda ya miaka kadhaa kwa Simba sc kuendelea kutamba huko kumataifa tumewaona Yanga Sc na wao waki anzisha utawala wao kiasi cha kutinga mpaka fainali shirikisho barani Africa

Msimu huu timu zote mbili zinawania tiketi ya kwenda clabu bingwa makundi, ila tayari Yanga kasha weka mtaji wa ushindi wa goli mbili igenini huku simba wao wakitoka sare na goli mbili za away

Kwa hesabu za kawaida ni kama Yanga amesha fuzu na simba wana zaidi ya nusu ya asilimia kufuzu makundio

Kwa mantiki hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Tanzania inapeleka vilabu viwili makundi ya clabu bingwa Afrika,

Wengi wana chukulia wepesi hili jambo ila sio jambo la kuchukulia wepesi kabisa.
Hii ni zaidi ya achievement,

Swali ambalo nime jiuliza na kukosa majibu haya yanayo endelea ni kwasbabu ya kukua kwa soka la Tanzania au, soka la Afrika limeshuka so na watanzania wana serereka huko,?

Kuna siku Yanga na Simba watakutana huko clabu bingwa kwenye mtoano, iwe robo au nusu, au fainali, na hapo ndio patakapo chimbika bila jembe,
Soka la clubs limekua sababu husajili mpaka wageni wenye viwango vizuri. Soka la Taifa Stars nalo linakua kutokana na wachezaji wanaocheza nje ya nchi.

Zamani hatukua na wageni wengi, pia hatukupeleka wachezaji wengi nje zaidi ya Oman labda.
 
Back
Top Bottom