Smz yakataa maeneo yake kuchimbwa mafuta

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Mohammed-Aboud-400x272.jpg

Waziri wa nchi ofisi makamo wapili wa Rais Mh Mohammed Abuod

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imezuwia maeneo yake kufanyiwa utafiti wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kufuatia utafiti kama huo kufanyika katika maeno ya Tanzania bara.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta litafanywa na wanzazibari wenyewe wakati utakapofika na sio kampuni za kigeni.

Amesema serikali imeshatoa raarifa hiyo kwa serikali ya muungano kutoyaruhusu maeneo yake kufanyiwa utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia

Waziri Aboud serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria ya kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.

Amesema katika kikao kilichofanyika hivi karibuni suala la mafuta na gesi asilia lilikuwa ni miongoni mwa agenda zilizojadiliwa na ilikubaliwa suala hilo lipatiwe ufumbuzi wa haraka.

Hata hivyo waziri Aboud amesema serikali haitambuli mikataba yoyote iliyosainiwa awali ya upande wa pili wa muungano kuyaruhusu makampuni ya kigeni kutafuta mafuta katika maeneo ya Zanzibar.

Tamko hilo la waziri Aboud katika baraza la wawakilishi kumefuatia madai yaliotolewa na mwakilishi wa jimbo la mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu aliedai kampuni ya Petro Brass imeruhusiwa kufanya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar
 
Msaada definition ya maeneo ya zanzibar.

ni lile eneo lote la visiwa vya unguja na pemba, pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka na bahari yake, ambapo kabla ya muungano wa tanganyika na zanaibar likijulikana kama jamuhuri ya watu wa zanzibar. hii ni kutoka katika katiba ya zanzibar
 
Baada ya kujua hamna chochote katika eneo hilo la Tanzania-Zanzibar mnajifanya mnakataa, hamna uwezo kikatiba wa kuamua mambo ya nchi kwa ikiwa Shein ni Waziri tu je huyo Abud si hewa tu? Serikali ya Zanzibar ni kujifurahisha tu
 
Mheshimiwa Mohamed Aboud, una uhakika na uyasemayo? Mbona Zanzibar ni Tanzania?
 
Wed, Jun 20th, 2012

Wed,June 20th, 2012 / Tanzania |


Zanzibar has restricted foreign companies from exploring for oil and gas, Minister of State Mohammed Aboud Mohammed told the House of Representatives on Tuesday.


Aboud-Mohammed.jpg

State Minister in the Second Vice-President's Office Aboud Mohammed


He said this after some legislators had demanded for immediate removal of oil and natural gas from the list of Union matters. He assured the law makers that the issue would soon be solved.


During questions and answer session, legislators Ismail Jussa Ladu (CUF-Mjimkongwe), and Salmin Awadhi Salmin (CCM-Magomeni), expressed their concerns over delaying the process of removing the oil and natural gas matters from Union list in accordance with 2009 House of Representatives resolution.


"The Government of National Unity (GNU) promised that it will solve the problem within four months. But we are in fifth month and nothing has been done. What is the problem?" wondered Mr Ladu. Responding to the concerns, the minister said that the
Zanzibar government had sent a notification letter to the Union Government, informing it that any contract with a foreign company to explore oil and natural gas in Zanzibar territory would not be accepted.


"I would like to assure members of the House and Zanzibaris in general that we, officers in the government, will do all it takes to safeguard the interest of Zanzibaris. We cannot act contrary to your wishes," said Mr Mohammed. The minister said: "On several occasions President
Jakaya Kikwete has acknowledged that there is a problem in connection with Zanzibar's demands for oil and natural gas autonomy. This is an indication that Zanzibar's demands will be considered.


By ISSA YUSSUF
, Tanzania Daily News
 
Why they keep on repeating this? I believe this has been stopped no one is exploiting and exploring Gas or Oil around sovereign boundaries of Zanzibar...

Ninavyojua ndio Maana hata Tanga ambako wanasema kuna Mafuta na GAS hawajaamuka kuchimba kwasababu Tanga na

Pemba ziko karibu sana, lazima kuwe na uelewano kati ya Tanganyika na Zanzibar kuhusu suala hilo
 
Kwa hili nawapongeza Wazanzibari. Ingawa wanamchukia Nyerere lakini ulikuwa ni msimamo wa Nyerere kuwa tusiruhusu wageni waje kuchimba madini na mafuta yetu mpaka hapo Watanzania watakapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo wenyewe. Lakini viongozi wetu waroho wa kutajirika upesi wakakimbilia kusaini mikataba ya ajabu ajabu na sasa tunaangalia tu wakati dhahabu yetu inasafirishwa nje ya nchi kila kukicha wakati shule zetu za kata hazina madawati.
 
Hawa vilaza washaanza kelele zao. Nikiambiwa nichague kwenda kuishi Jehanamu au Zanzibar, nitachagua Jehanamu maana kuna uwezekano wa kukutana na watu wenye akili timamu kuliko Wazenji.
 
Zanzibar sio nchi! Kwanza hata ukubwa wake ni sawa na wilaya ya Tarime!

wacha longo longo zako hizo mkuu unatudharaulisha watanganyika wenzako kwa wazanzibari ukiongea :blah:

kuna nchi nyingi tu duniani ambazo ni ndogo kuliko zanzibar...
Zanzibar ni kubwa ki eneo kuliko nchi hizi zote
kwa bara la Africa
1. Mauritus
2.Seychelles
3.Comoros
4. São Tomé and Príncipe
kwa bara la nchi za ulaya
1. Monaco
2. Malta
3. San Marino
4.Liechtenstein
5.Andorra
na kuna nchi nyingi tu kule upande wa Caribbean na majirani wa Australia ambazo ni ndogo sana kuliko Zanzibar

Tuiwache Zanzibar iende salama na tuwe majirani wao wema haina haja ya kupotezeana muda kwa kitu tunachokijua kuwa Muungano wetu hauna n guvu tena ni mivutano tu ndio iliyobaki....mie naona bora wasepe kinyao:yo:
 
Back
Top Bottom