Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Hii ni kwa hasara yako mwenyewe.
Hakuna aliyewahi kufunguliwa mashtaka
kwamba hajatoa sada kanisani/msikitini na ndo maana
inaitwa sadaka.Jitahidi ulipe kodi,hiyo usipolipa utakumbana
na vyombo vya dola.Ila ukumbuke serikali haina mbingu
ya kukupeleka ukiisha kufa. Wala hutakutana na mtu huko
mbele ya safari yako ukamuonyesha TIN namba yako.
ukitafakari haya utaelewa sadaka ni nini?

Si lazima kama umemuona yatima
au mjane upeleke sadaka kanisani afu ndo uwaambie wampe
unaweza kumpatia huyo mjane/yatima sadaka yako
na mbinguni ikahesabika.Saidia yatima walipie ada
wape nguo n.k na kanisani peleka sadaka kwa maendeleo
ya kanisa na kutunza watumishi. period.
 
Malaki 3:10 nakuendelea inaeleza vizuri sana. "Leteni zaka kamili gharani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo..... zaka ni fungu la kumi.
 
Sasa hivi hatuko kwenye sheria za Musa bali za Kristo.
Nioneshe sehemu iliyoandikwa maneno hayo ndugu! Yesu alimshinda shetani kwa kutumia agano la kale, na agano la kale ndo ina ahadi za parqdiso ya milele (Isaya 58-66)
 
kweli kabisa wachungaji wengi ni wasanii tu wanataka sadaka ,mimi tokea 2010 niliacha kutoa sadaka najikusanya kila wiki naenda kutoa kwawazee wasiojiweza na mayatima
Hayo unayofanya si maagizo ya Mungu (Malaki 3:8-10). tatizo ni kutojua ukweli, tafuta maarifa ya Mungu utapata neema yako, kutoa Sadaka na Zaka ni agizo la Mungu kurudi kwake aliyekupa, hutumika kulipa wachungaji (walawi kiBiblia) na kueneza injili ya Kristo na kusaidia wahitaji. karibu Seventh Day Adventist Church (the bride of Jesus Christ)
 
That's why i will remain a Roman Catholic for life!
Unamkuta pastor ana hummer complete with security detail (bodyguards) plus a helicopter wakati ata jengo la kanisa hana waumini mvua yao jua lao!
KWELI JAMANI???!!!!
soma Biblia ndugu, RC wamechakachua AMRI za Mungu, wameodhi mamlaka za Mungu (kusamehe dhambi), kubadili majira ya Mungu, kufundisha mapokeo ya wanadam badala ya neno la Mungu! RC HAWANA TOFAUTI NA WALA ZAKA NA SADAKA za wanyonge hawa wanaolalamika humu!
 
Hahaaah unanikumbusha sikumoja nilienda kwa mzee wa upakoroko ,daaaa nililojionea !!!!nikastaajabu huyu Mungu wakweli kwanini anachezewa?kwanini asimuadhibu tapeli yule?
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
Yaaani ww na umri huo ulidhani pesa hizo za sadaka anafanyia nn? Ulijua anampa mungu kwa njia gani? Endelea kumnufaisha tuu na ww baki maskini.
 
Kusomewa mapato na matumizi kanisani kwako iwe rc au kwingineko hautakuwA na maaba yoyote kama hakuna Usafi na utakatifu watakusomea mapato na matumizi sawa ni vizuri he utapata nini zaidi ya kwenda motoni kwa ajili ya kuongozwa na kipofu?
 
Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki, tukiwa watoto mapadri wengi walikua raia wa kigeni. Mapato ya J2 yalikuwa yanatangazwa na kama mleta mada alivyosema pesa nyingi ilisaidia wazee, yatima, na wasiojiweza. Padri aliwahimiza vijana kuweka akiba na pia aliyekua na nidhamu na akiba yake aliongezewa mtaji, kuna sehemu watu wengi walihamia kutoka sehemu mbali mbali kwa kwenda kukata mkonge au ukuli bandarini, kwa mungozo wa mapadri watu wale wengi walinunua mashamba na kujenga nyumba sasa wameloea kabisa. Pale nilielewa maana ya lile neno baba paroko. Sijaelewa kwakua walikua wakipata misaada kutoka Vatcan au ilikuaje.

Makanisa mengi ya Pentekoste yanajitegemea yenyewe, sadaka ndiyo mshahara wa mchungaji na huo ndio umwezeshe kuendeleza kanisa, kutangaza injili, kulipa bills za umeme, maji, huduma za internet, nguo za wanakwaya, vifaa vya kanisa. Pia dini ni imani, kuna watu wanaimani kubwa sana na wako tayari kutoa nusu ya mali walionaya kwa Mungu kupitia kanisa fulani, unapomuona mchungaji anaendesha gari jipya si maajabu sana ikawa gari ile amepewa kama zawadi na mmoja wa waumini au msamaria mwema mwingine.

Ur truly a great thinker
 
Wana kila mbinu ya kuhakikisha sadaka lazma utoe tu.
Kwanza kutoa kwa kila bench, ivo utaona aibu mwenyewe kukaa tu wakati wenzako wameinuka.
Pili michango ya kinanda, ujenzi wa ofisi etc
Tatu siku izi wameanzisha utaratibu wa kutunzwa madhabahuni.
Mama Rwakatale kwake fungu la kumi la mwaka mzima unatoa mwanzoni mwa mwaka, ili hata ukihama mji, hatakua na cha kupoteza etc.
 
Hayo unayofanya si maagizo ya Mungu (Malaki 3:8-10). tatizo ni kutojua ukweli, tafuta maarifa ya Mungu utapata neema yako, kutoa Sadaka na Zaka ni agizo la Mungu kurudi kwake aliyekupa, hutumika kulipa wachungaji (walawi kiBiblia) na kueneza injili ya Kristo na kusaidia wahitaji. karibu Seventh Day Adventist Church (the bride of Jesus Christ)

Yesu amesema watu watangaze neno bila kutaka ujira
 
Back
Top Bottom