Sitasahau siku pombe zilitaka kunitoa roho

Mr mutuu

JF-Expert Member
Jan 27, 2023
2,201
10,830
Leo Kuna mtu kanipigia simu nikakumbuka tukio Moja miaka kama 10 imepita

Kipindi hicho ujana mwingi+ tulikua wajanja wajanja tumeshika shika vipesa si haba, npo dsm Kuna jamaa yangu ye hata tungi hapigi ananicheki hewani kuniuliza upo wapi, namwambia npo geto ila naenda bulls park(karibu na chuo Cha ardhi pale juu kidogo ya mlimani city) kupata chakula, jamaa ananiambia poa ntakukuta hapo

Natoka na jamaa yangu mmoja tumefika pale tukala, Kisha tukaingia ndani Kule kwenye vinywaji... agiza grants kubwa na drostdyhoff ya kuchanganyia( hii combination ni ya kipuuzi sikuwahi kurudia tena)... Basi bana piga mitungi pale sana kichwa kikaanza kuwaka, Anza kutoa ofa kwa wahudumu.... Ongeza vinywaji... Hapo mfukoni Nina kama 300k.. inafika jioni tushalewa hapo nauliza bili ni inakaribia 200k(kipindi hicho bado vinywaji bei sio sana) nikaona hapa nilipe bili tuhamishie vita geto tupige za mwisho tupumzike

Jamaa aliyenicheki mchana ndo anafika sasa ananiambia twende nje kuongea, tunafika parking jamaa ananipa 1M ananiambia weka mbali Hio kwanza, sasa huyu jamaa yangu aliyekua amekuja alikua anamiliki printing company kipindi hiko sio nyingi kama sasa ivi, kama mwezi uliopita alikuja rafiki yangu mmoja anafundisha eckenford ile ya Tanga,alikua anatafuta mahali pa kuprint t-shirt za shule Kila mwanafunzi t shirt 3 so ulikua mzigo wa kama t shirt 3000+ ndo bila hiyana nikamuunganisha na huyu mwenye printing company wapige kazi, mi sikufatilia hata walipana vipi,baada ya kazi kuisha huyu jamaa angu huyu kama kama alikua kanifata kunipa shukrani kwa kazi niliomconnect

Jamaa akanipa 1M nikaiweka kwenye carpet ya chini ya gari pale kwa dreva, tukaingia ndani... Kufika ndani jamaa akaomba ile bili akalipa afu akanipa kama 100k tena ya kutumia pale akaniasa ile M nisiiguse ye akaondoka zake maana hata hanywi pombe, badae sana jamaa alikuja niambie ile dili ilimpa kama 6M faida so kunitoa vile ni kama alikua analipa fadhila japo sikuwahi kumdai

Balaa ndo likawa limeanzia hapo, aisee acha tuanze kuagiza upya sasa, grants drostdyhoff na ofa kwa wahudumu, jamaa yangu niliyekuja nae akazima akawa amelala kwenye kochi, ikafika muda na Mimi sioni kabisa Yale mataa ya ndani naona maruwe ruwe tu

Nikalipa Hio bili mpya nikamnyanyua jamaa tuondoke, nakumbuka Kuna dada akawa kaja parking ananiambia usiendeshe gari we kaka, mmelewa sana! Nikaona anatania huyu Mimi huyo nikasepa, sikumbuki hata nilipita njia Gani nashangaa tu npo sinza hoteli Moja nilikua napenda kulala hapo,nikafika nikachukua vyumba viwili tukampeleka jamaa yangu aliyezima akaingia chumbani Yani hata kufunga mlango hawezi, hangaika nae sana tukaamua kumfungia kwa nje, funguo nikampa receiptionist...

Akili za kijinga zikaanza sasa, nawaza kwenda kangaroo au corner bar pale nikasafishe macho, ila nishalewa macho mazito balaa, nikaacha gari nikachukua bajaji mpaka pale kangaroo, kufika nikamwambia jamaa wa bajaji aagize chochote ntalipa, tukae pale anipe company afu atanirudisha, akaniambia 30k mi nikamwambia poa tu

Aisee muda unaenda nishavuta mdada yupo meza yetu pombe ndo zinamiminika, hapo naanza kuigusa sasa ile 300k nilikua nayo awali, pombeka Sana badae jamaa katurudisha na yule dada hotelini, kufika namlipa jamaa akaondoka zake tukaingia room, sasa akili za pombe nazo sasa, hapo Nina kama laki 2 ila sijui nikapata akili Gani aisee nikaenda kwenye gari nikachukua ile M nikaja nayo chumbani

Kufika ndani tukaagiza bia, mhudumu kuleta namlipa nimetoa vibunda vyote nikalipa, yule dada npo nae akaona kibunda akaanza kunipet pet kwa ukaribu kuliko awali nikaanza pata instincts tu kua hapa Leo huyu lazima anipige huu mzigo, nikamwambia kaoge kwanza wewe, akawa anasisitiza tukaoge wote nikakataa, akaenda akaoga, muda wa kuoga mi nikaenda kuoga ila sikuacha pesa, nafika bafuni nawaza hii pesa naficha wapi, aisee ila pombe hizi, nikachukua ile M nikaiweka chini ya kama kiuvungu ya choo Cha kukalia, nikabaki ni ile hela nyingine nikarudi nayo

Mtoto wa watu akaanza kujituma kwenye shoo ila mi hapo akili inawaza huyu Leo ataniibia tu, baada ya round 1 tu akili ikasema usinitanie, nikamwambia yule dada, si tumepatana 40, nikatoa 60 nikampa nikamwambia hii 20 ya usafiri we nenda nataka kulala mwenyewe, akaanza kulalamika mara baby mbona unakua ivo, mara tuagize bia bana mi bado sijalewa, nikilewa ndo ntakupa vizuri na maneno mengine mengi tu...

Hapo Hio 60 kashaivuta, nikampa 10 nikamwambia kaongeze bia, akavaa haraka haraka akaenda mapokezi, nikaamka nikafunga mlango nikatulia, kurudi kugonga nikamwambia we nenda tu kama hizo bia kunywa mi nalala, aisee alisumbua pale mpaka mtu wa mapokezi akaja, nikamwambia mi hanidai huyo ye anywe bia aondoke

Nikarudi fakamia bia zilizobaki pale nikaenda kuoga hata kufunga maji nilisahau nikaenda kulala, aisee kesho naamka hata kuvaa suruali siwezi, sijui ndo sukari imefika yaani hata kushika simu natetemeka, nikajivuta vuta kama nusu saa hivi ndo nikavaa suruali akili ya kwanza nitafute fanta orange ntakuja kufa, nikaamka nikafunga maji bafuni nikatoka nikafunga chumba kwa nje kwenda mapokezi sioni mtu

Nikatoka kutafuta duka, njiani nguvu zikaisha nikakaa barabarani npo hoi, akaja dada mmoja anapita kajitinda kiislam ananiuliza we kaka unaumwa, hapo hata kumjibu siwezi Yani npo hoi, nikajikaza nikatoa elf 10 mfukoni nikamwambia naomba niletee fanta orange na maji, akaenda bado ananishangaa, kurudi nakunywa ye yupo busy kaka unaumwa Nini, au uende hospitali mi nabaki kumshangaa tu

Soda haipandi, nikawa namsumbua tu, mara niletee maziwa, mara juice yaani vurugu mechi, badae yule dada ananiaga Kuna mahali anawahi basi nikamuomba namba bila hiyana akanipa akaniambia utaniambia unaendeleaje

Nikajivuta nikarudi hotelini na ma vinywaji yangu, kufika ndo nikakumbuka M nilitoa kwenye gari mbona siioni, aisee tafuta sana wapi, baada ya kama nusu saa ndo nakumbuka nilipoficha, kumbuka sikufunga shower nakuta hela zimelowa tu, nikazitandika kitandani pale, jikaza sana pale nikarudi mapokezi ulizia jamaa yangu naambiwa hajaamka, sikutaka kelele nikavilipia vyumba tena Hio siku nikarudi kulala, kuja kushtuka naamshwa na jamaa yangu Hio sa 10 jioni, kuja Kuonana tukaanza kuchekana tu wote..... Mwili haufai nahisi kufa kufa tu

Aisee ila vijana enzi hizo ni wabishi sana, tukashauriana ujinga tukaenda kupiga supu, kurudi tukaendeleza gambe tu, ushungi badae alinichek na slices zikalika kibishi tu, we went on a drinking spree ya kama siku 4 straight, ile M zaidi ya kuweka mafuta hakuna la maana nilichofanya, shkamoo pombe!!
 
Party muhimu ya Ushungi umepotezea.

Umetumia muda mwingi kutuhadithia mipombe yako ambayo hata hivyo haikutaka kukutoa roho. Maana kama kweli roho ilitaka kutoka usingerudia kunywa tena siku hiyo, sasa wewe umeendeleza siku nne.

Hebu futa, tunaomba story ya Ushungi. Dada yake na Malaria 2.
 
Dah matukio ya pombe na pesa hayafai kabisa unaweza kuwa umetembea na ada ya mtoto wako ukajikuta umetumia kwenye pombe afu kesho inabidi ulipe ada unaanza kuwaza kuwapiga ujanja wakuu wa shule huku ukijuta sana kumamae nyingi nyingi tu ka uliitwa
 
Mimi huwa na hofu ya Maisha ujinga mwingi 😊 wa ujana sijafanya...

Nilikua naogopa Sana kuja kua MTU wa ovyo ovyo so Mimi Ni ICON kwenye familia..

Mdogo angu ndio msumbufu wa familia mpaka Sasa..

NB.
Kama haujawai kutumia vilevi au kilevi chochote Basi jua hujawai kuishi 😊😊
 
Dah matukio ya pombe na pesa hayafai kabisa unaweza kuwa umetembea na ada ya mtoto wako ukajikuta umetumia kwenye pombe afu kesho inabidi ulipe ada unaanza kuwaza kuwapiga ujanja wakuu wa shule huku ukijuta sana kumamae nyingi nyingi tu ka uliitwa
Unakunywa responsible unaacha offer na shobo na WATU

Mimi nilikataaga kua mtu wa ovyo ovyo tangu udogoni mwangu

Kwanza unatakiwa ujue alcohol persistent yako na uweze kui control ukisha ijua ukiifikia acha kunywa hata ushikiwe mtutu
Mbona easy TU
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom