Elections 2010 Sitakua mmoja wao

Negotiator

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
303
44
Itakapofika October 31 mimi na familia yangu na jamaa zangu wa karibu hatutakua mmoja wa;
  • wale watakaopigia kura wala kuunga mkono chama kilekile kinachokumbatia ufisadi.
  • wale watakounga mkono wadogo zetu ndugu na jamaa kendelea kununua elimu kama bidhaa kutoka shule za serikali
  • wale watakao unga mkono serikali iliyoshindwa kujenga uchumi imara na kulinda thamani ya shillingi yetu
  • wale watakaomtukuza mgombea aliyedharau wafanyakazi, kuwabeza watoto wanaopata mimba wakiwa mashuleni na kunyanyapaa wenye VVU
  • wale watakaoendeleza serikali iliyopelekea upatikanaji duni wa huduma za afya
  • wale watakaoirejesha madarakani serikali iliyokubuhu katika matumizi holela ya kodi za wavujajasho wazalendo
  • watakao ipa ushindi serikali ile ile isiyoheshimu katiba na sheria za nchi
  • watakao ipa mwanya serikali isiyoheshimu uhuru wa vyombo vya habari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom