Elections 2010 Sita atumia ma-komandoo wa serikali kulinda rushwa ya uchaguzi

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,171
Wana JF,
Asubuhi ya leo nimepata taarifa toka jimbo la Mh Sita kwamba Walinzi wake wamejeruhi watu wa PCCB na baadhi ya wajumbe wa CCM.

Jana jioni vijana wa PCCB wakiwa na mwenyekiti wa kitongoji ambacho leo hii kingetembelewa na wagombea wote, walivamia mkutano uliokuwa ukifanyika usiku kwa lengo la kuwaweka sawa wana-CCM kabla ya siku ya kampeni. Bila kutegemea Mh Sita pia alikuwepo na walinzi wake.

Bila kutegemewa wafuatiliaji hawa waliambulia kipigo. Mh. Sita bado ana walinzi toka serikalini aliopewa akiwa spika.

Nadhani magazeti yatakuwa yatapata undani huu maana nasikia wengine wamelazwa.
 
Sijuwi pahala gani nilisoma kuhusu hili tatizo la hawa incumbets kutumia mali za umma baada ya mda wao wa uongozi kumalizika, kwa kujipigia kampeni za kurudi madarakani. Ilitakiwa wakati rais, wabunge na madiwani mda wao wa uongozi umemaliza walitakiwa waache kutumia ushawishiwa nafasi zao, mali za umma katika shughuli zao za siasa za kutafuta nafasi ya kurudi tena. Hapa nashangaa Mh.Sitta anadaiwa kutumia walinzi toka serikalini sijuwi akiwa kama nani?

Ipo haja kuwe na sheria kurekebisha hii ili kuwa na mazingira sawa ya ushindani na kuzuia ufisadi huu wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom