Siri ya pesa ya madini na hali halisi ya Mererani (Swali na Hoja)

Nasakadoo

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
343
169
Mapema mwaka huu nilifunga safari mpaka Mererani iliyopo Wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara, zamani Mererani ilikuwa sehemu ya Mkoa wa Arusha.

Mererani nilifanikiwa kwenda mpaka maeneo ya machimbo ya madini, kumbuka Madini ya Tanzanite yanapatikana Mererani na ni madini pekee Duniani yanayopatikana/yanayochimbwa Tz tu.

Kwa nilivyoitazama Mererani nzima,wakazi wake kwa asilimia kubwa ni maskini saana,yaani mtu ukiambiwa hapa ndo Mererani ambapo Madini ghali yanapatikana huwezi kuamini

Huduma za Afya mbovu,maji wanakunywa ya Chumvi,ukitaka maji baridi/safi ya kunywa unauziwa kipimo glasi Sh 100 mpaka 300sh kwa Lita moja,na hayo maji safi huwa yanatoka Bomang'ombe na kupelekwa Mererani kuna umbali sana.

Hata hayo maji Chumvi sio kwamba unapata bure,bado nayo wanauziwa kwa Sh 100 kwa ndoo kubwa(Lita 20). Watu wanaishi maisha duni saana,wakazi wengi wa Mererani ni Wajaluo,Wamasai na mchanganyiko wa makabila ya Kanda ya kasikazini.
Wamasai na Wajaluo kila siku hubebesha punda viroba ya mahindi kwenda kuuza kuona kama watapata angalau pesa ya kujikimu. Unawakuta Punda wapo kwenye jua kali huku mizigo ya mahindi ikiwa juu yao wakisubiri wanunuzi wa Mahindi.

Huko Mererani nimegundua kuwa kuna Baa nyingi sana naweza kusema Baa ni nyingi utadhani makazi ya watu kumbe Baa…
Huduma za usafiri bado ni tabu sana, kuna usafiri wa magari aina ya Defender/Land Rover za Zamani zile ambazo huwa zinatumiwa na Polisi… kwa huko haya magari wanaiyaita Mando na hayo magari ni kwa usafiri wa kutoka Mererani kwenda KIA…

Halafu kama unaenda Arusha kwa kupitia Wilaya ya Arumeru kuna usafiri wa magari aina ya DCM…
Nauli zao ni Tsh 2500 mpaka 3000/-Mererani kwa kiasi kikubwa saana barabara zake ni vumbi tupu…

Kwa kifupi Mererani ni moja kati ya Maeneo duni saana wakati hapo hapo kunachimbwa Madini ghali (Tanzanite).

Zinakwenda wapi Pesa za Madini?
Hili ni swali ambalo nilijiuliza saana… nilidadisi saana…

Kuna habari ambazo zinachanganya kuhusu Pesa za Madini na Madini yenyewe…
Ukipewa story na watu wa huko,utaambiwa huyu alikuwa na bilioni moja,
Mara yule aliyepita alikuwa na milioni 600, mara unamuona huyo mwenye pikipiki alikuwa na gari la 200m, ana Ghorofa Arusha, na vitu kama hivyo lakini wote hao kwa sasa eti hawana kitu tena.

Yaani shughuli kubwa Mererani Ni Uchimbaji wa Madini ndo shughuli kubwa ambayo wengi wanaitegemea…wachimbaji na wasiochimba.
Nikauliza kwa nini naambiwa watu wengi hupata hela nyiingi saana lakini ukiwaangalia kwa sasa hawana hela?
Sababu zinazotolewa ni nyiingi saana.

Nikaambiwa,kule mtu akipata pesa ya madini hata 200m au 150m au yoyoye ile,huwa anakula toka Day One mpaka pesa inaisha… halafu unaambiwa pesa ya madini huwezi kula peke yako yaani huwezi kuitumia peke yako…

Kwanza ni nyiingi, fikiria hujawahi kukamata hata milioni 2 ya kwako, leo hii unapata jiwe la Tanzanite unaenda kuuza unapewa 70m,au hata 20, kuna wengine unaambiwa anapiga mpaka 150 hadi 700m… so niliambiwa eti mtu akizipata huwa kama anapata mchecheto, halali nyumbani, ananunua magari, anaenda kulala Hotelini town… na raha zote za dunia… wengine mpaka eti huwa wanagawa hela… yaani anakuja na Bunda labda la 10m… na kuanza kuwapa washikaji ambao hajapata kitu… anagawa tu… na hizo hela wala hata halipi kodi TRA… yaani akiuza jiwe la milioni 50… anapokea yoote bila kukatwa chochote.

Sasa nikataka kujua kuna siri gani migodini inayowafanya watu wapate hela nyiingi lakini baadae zinaisha kabisa kabisaaa… mpaka mtu anatia huruma hana hata mia?

Jibu unalopewa ni eti,hiyo ni akili ya mtu tu…lakini sasa kwa nini wachimbaji woote wawe na akili ile ile? Yaani wote wapate mawe,wauze na pesa walewee,wahonge vimada,wacheze kamari?
Lakini niliona kama kuna kitu behind the scene kwenye pesa inayotokana na Madini ya Tanzanite…
Huenda hata wao wanajua ama hawajui,… kinachomfanya mtu atumie zaidi ya m 100 mpaka inaisha kabisaaa… je hashtuki? Na unakuta kuna wengine walienda wakaambiwa vile vile kuwa bwana huyu hapa alipata m 70 akala zoote… huyo huyo aliyeambiwa vile,bado naye akizipata anakuwa vile vile…

Ni akili ya mtu kweli kuamua matumizi ya pesa ya Madini yawe Negative ama Positive? Au kuna mambo ya giza ambayo labda hata wao hawajui ndo yanayopelekea pesa ya Madini ipukutike kabisaa?

Lakini ukiangalia wale wawekezaji yaani wanaomiliki vitalu/migodi ya madini ndo wanakaa na hela… ila wale waenda shimoni kuyatafuta,kule wanaitwa Wana-Apolo hao hawakai na hela! Kuna nini haswa?
Na kwa nini eneo la Madini liwe masikini saana wakati madini yapo?.
ila siri moja tu ya hawa wachimbaji madini,wakipata hela eti huwa hawana roho mbaya… yaani kukupa Milioni 5 bure sio issue. Story za matumizi ya pesa za madini zinachekesha nyingine, mtu ananunua Smartphone na anaajili mtu wa ikiita apokee na kumuwekea sikioni ili aongee… akimaliza kuongea,mwajiliwa anakata na kumuwekea mfukoni… jamani pesa hizi…

Kuna mambo mengi huwezi kuyamaliza ukianza kutafakari juu ya matumizi ya pesa ya Tanzanite…
Labda wenye uelewa zaidi juu ya pesa ya madini waweza kuongezea hapa!
ila issue kubwa kwangu kwa nini Wachimbaji wengi wakipata hela huishia kuzigawa,kuzitumia kiholela,na kurudi katika hali ile ile?

Na unakuta eti mtu unaweza kuanza kuchimba leo,ukaja kupata jiwe mwaka kesho,wengine wanamaliza miaka hadi mitatu eti,mpaka mitano hajapata Jiwe… ila kuna wengine wanakuwa na bahati yao,miezi minne au sita tu anapata!
ila hata uwe na bahati vipi huwezi kwenda leo ukayapata kesho… Lazima usote na ujitoe kabisa… yaani ni kama upo Sayari nyingine kule unavoambiwa!

Na kule mtu kufa sio issue… ni kawaida saana! Unaweza kusikia mtu fulani kafa mgodini… wala hawashtuki hata! Wanachofanya ni kusafirisha mwili na shughuli kuendelea…
Ni hayo tu niliyoyaona huko Mererani Simanjiro Manyara…

Lakini Serikali pia basi na yenywewe iwabane hawa wawekezaji, waiboreshe Mererani. Wanaoishi karibu na madini wana maisha duni halafu wanaonufaika ni nje ya eneo hilo… haki iko wapi?
ndiyo maana Hata Wana Ntwala hawataki gesi itoke huko…
 
Tatizo la mererani ni uchawi, mchimbaji analoga, nwenye mgodi analoga, mnunuzi analoga, Mererani ni sehemu waganga wa kienyeji wanavuna pesa sana.
Story nyingi za mererani ni uongo. Utakuta mtu akipata milioni 5 utaambiwa amepata milioni 100 ! uongo mtupu
 
Tatizo la mererani ni uchawi, mchimbaji analoga, nwenye mgodi analoga, mnunuzi analoga, Mererani ni sehemu waganga wa kienyeji wanavuna pesa sana.
Story nyingi za mererani ni uongo. Utakuta mtu akipata milioni 5 utaambiwa amepata milioni 100 ! uongo mtupu

Si ndo hapo… ndo maana nikataka kujua inakuwaje mtu unaanza kutafuna milion 200 mpaka unabaki na ndala? Hijishtukio?
Au milioni 2 wanaongeza zero nyuma?
Lakini sasa hizi story ni kila mtu atakwambia hivo
 
ngoja nimalizie kusoma confessions of an Economic hitman halafu nije kuchangia maana naona yote yamo humu kitabuni...Nahisi viongozi wetu hawasomi vitabu
 
Si ndo hapo… ndo maana nikataka kujua inakuwaje mtu unaanza kutafuna milion 200 mpaka unabaki na ndala? Hijishtukio?
Au milioni 2 wanaongeza zero nyuma?
Lakini sasa hizi story ni kila mtu atakwambia hivo
Tatizo la mererani ni uchawi, mchimbaji analoga, nwenye mgodi analoga, mnunuzi analoga, Mererani ni sehemu waganga wa kienyeji wanavuna pesa sana.
Story nyingi za mererani ni uongo. Utakuta mtu akipata milioni 5 utaambiwa amepata milioni 100 ! uongo mtupu
thread imeeleza kila kitu kwa ukweli mimi nipo maeneo karbu sana na mereran, wapo watu nawafaham walikua na pesa nyingi sana kuliko hata hzo M200 lkn sasa hv wanaomba soda
 
Tunaamini sana majaliwa.

Mfano. Huko Mererani kulitokea janga, watu wakafukiwa shimoni,akaenda Kikwete akasema "ni kazi ya mungu".

Huyo rais wa nchi. Ametembea dunia nzima.

Badala ya kusema tuangalie vipi tutaboresha miundombinu, anakwambia ni kazi ya mungu.

Kwa hiyo sishangai.

Wasomi wanalalamika kazi hamna. Wakati hata kuandika tu kuhusu hii sehemu ni kazi.
 
Mkuu hakuna tajiri mwenye mgodi anaweza kuwekeza mererani.....sanasana wana apolo ndio wanajenga pale ni wachache...wengi wakipata hela wanajenga arusha na kwingneko.....matajiri wengi wamewekeza arusha mjini mahoteli na apartments za kupangisha
 
Mkuu unayosema ni kweli kabisa mimi nimesota Mererani toka mwaka 2000 had 2004 nimezama migod mingi tu' opec nimezama kwa marandu njia ya chini kwa sunda kwa mawaya kwa onesmo kwa kirika kwa six' block d' nimezama kwa askofu na kwa abas marenj lakini pesa kubwa niliopata haikuzid lak 5 nikaona huu ni ujinga nikaondoka zangu alaf mkuu maji ya kule sio ya chumv ni magadi nna story nying sana za kule zakutisha kweli kule hakufai jamani kwa sasa nipo kibaha.
 
Hivi pakijengwa pakawa kama darslam hayo madini yatachimbwa wapi??nenda south africa kaangalie vijumba vya machimbo yao hata mererani afadhali.
 
Mkuu unayosema ni kweli kabisa mimi nimesota Mererani toka mwaka 2000 had 2004 nimezama migod mingi tu' opec nimezama kwa marandu njia ya chini kwa sunda kwa mawaya kwa onesmo kwa kirika kwa six' block d' nimezama kwa askofu na kwa abas marenj lakini pesa kubwa niliopata haikuzid lak 5 nikaona huu ni ujinga nikaondoka zangu alaf mkuu maji ya kule sio ya chumv ni magadi nna story nying sana za kule zakutisha kweli kule hakufai jamani kwa sasa nipo kibaha.
Mkuu hiyo migodi yote umezama kipindi rizki ipo au.....mana kama uko mbele dashboard huwezi kosa hela.....hata kma ulikua kwenye mfuko
 
Mkuu unayosema ni kweli kabisa mimi nimesota Mererani toka mwaka 2000 had 2004 nimezama migod mingi tu' opec nimezama kwa marandu njia ya chini kwa sunda kwa mawaya kwa onesmo kwa kirika kwa six' block d' nimezama kwa askofu na kwa abas marenj lakini pesa kubwa niliopata haikuzid lak 5 nikaona huu ni ujinga nikaondoka zangu alaf mkuu maji ya kule sio ya chumv ni magadi nna story nying sana za kule zakutisha kweli kule hakufai jamani kwa sasa nipo kibaha.
ongezea hizo story hapa bhas tujue
 
Mkuu uliyosema yote ni kweli coz mm nafanya kazi huko, but kwa swali ulilouliza kuhusu watu kuishiwa tatizo kubwa ni ushirikina. Trust me kama ni uchawi umelala mererani unakuta apolo analoga, broker analoga, mwenye mgodi haishiwi kutoa kafara yani ni tabu tupu ndo mana hizo pesa zikipatikana zinaisha kimiujiza. Hizo story za mtu kushika milioni 100 200 ni kawaida ila zinaisha kimiujiza hutaamini
 
Sasa wewe mleta thread kama una akili nzuri,hata ukipata hela unaweza jenga/kuwekeza mirerani kweli?ambako source ya income ni moja tu?Na kama unafikiri hawapati mawe ya mamilioni na mabilioni,hayo majumba ya kifahari na maghorofa yaliyojaa boma ng'ome na arusha yamejengwa kwa hela zipi?
 
Hiyo stori ni mererani ya zamani, sasa hivi huo ujinga wa kutapanya pesa hawafanyi tena sasa hivi wanawekeza sana kwenye nyumba, viwanja na biashara. Ninao marafiki kama 10 hivi ni wana appolo wako vzr sana kimaisha
 
Back
Top Bottom