SIRA 31:25-31, Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana.

WeedLiquorz

JF-Expert Member
May 30, 2022
3,287
5,466
Salaam Wakuu,....

SIRA 31​

Pombe iliumbwa kumfurahisha mtu

25Usijioneshe kuwa hodari wa kunywa pombe,
maana pombe imewaangamiza wengi.
26Tanuri hupima ugumu wa chuma,
na pombe hupima mioyo katika shindano la wenye kiburi.
27Pombe ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi.
Maisha yafaa nini bila pombe?
Imeumbwa iwafurahishe watu.
28Kunywa pombe wakati wake na kwa kiasi,
kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
29Lakini kunywa pombe kupita kiasi,
kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha.
30Ulevi huongeza hasira ya mpumbavu akajiumiza mwenyewe;
humdhoofisha na kumwongezea majeraha.
31Usimkaripie jirani yako kwenye pombe,
wala usimdharau anapofurahia karamu.
Usimwambie neno la kumwonya,
wala usimsumbue kwa kumtaka alipe deni.

Najua wataomba Picha, hii hapa.
 

Attachments

  • IMG-20240217-WA0007.jpg
    IMG-20240217-WA0007.jpg
    43.7 KB · Views: 3

Uzi tayari
 

Uzi tayari
Aaah Alooh🤣 Ahsante kwa kunifumbua macho.
 
Safi sana pombe kwa kiasi ni tiba ya mwili na akili,hata peponi tutakunywa pombe acha tuanzie huku.
 
Hichi kitabu Cha sira nakitafuta sana... Ni biblia ipi kinapatikana?? Mwenye pdf yake atuwekee tafadhali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom