Singida: Mkurugenzi(DED) wa Halmashauri ya Itigi adaiwa kumuua mwananchi kwa risasi

uncle Bk

Senior Member
Apr 20, 2015
165
83
Mkurugenzi wa Halmashauri ya ITIGI amemshambulia na kuua mtu mmoja kisa mgogoro wa shamba.

Mkurugenzi huyo amemuua mtu huyo ndani ya kanisa la sabato kwa bunduki.

UPDATES:
Kamvamia mtu akiwa kanisani ktk kijiji cha kitaraka na kumpiga risasi ya kichwa na kufa papo hapo.

Wananchi wamechachamaa wanamtaka mkurugenzi. RPC wa Singida kaja kupoza fujo...

Huyu DED apimwe akili

VIDEO:


======
Itigi.jpg

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa Itigi, Pius Luhende na askari wawili wa wanyama pori wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa risasi muumini aliyetajwa kwa jina la Isaka Petro akiwa kanisani.

Akizungumza na Mwananchi jana kuhusiana na tukio hilo lililotokea Jumamosi iliyopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo alisema; “Ni kweli kumetokea mauaji hayo na hadi sasa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Itigi na askari wawili wa wanyama pori wapo ndani.

“Kwa kuwa nipo barabarani, sijajua undani wa jambo lenyewe. Siwezi kuzungumza mengi, ila kwa kiufupi ni jambo baya sana lililowahi kutokea, nitatoa kauli baada ya kupata undani wa tukio lenyewe,” alisema Jafo.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi alisema suala la mauaji si la kisiasa wala kiutendaji, hivyo linapaswa kujibiwa na Polisi, “Mtafuteni kamanda wa polisi Mkoa wa Singida anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia.”

Alipotafutwa, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida simu yake iliita bila kupokewa.

Mchungaji wa Kanisa la Adventista Sabato yalikotokea mauaji hayo, Manyigina Manyigina alisema alipata taarifa hizo akiwa Manyoni alikokuwa akiendesha ibada nyingine na alilazimika kukatisha ibada na kurejea Itigi ili kujua kilichosababisha tukio hilo.

Alisema alisimuliwa lilivyokuwa na waumini ambao walidai kabla ya mauaji hayo, kulitokea vurugu kanisani hapo wakati wa mafundisho ya sabato saa saba mchana.

“Waumini walinieleza kuwa baada ya kupata chakula cha mchana kanisani hapo, wengine walikuwa wameingia ndani na wengine walikuwa nje, ndipo waliona gari mbili aina ya Land Cruiser za Serikali zikiingia eneo hilo na mkurugenzi alishuka na maaskari watatu.

“Nje walimkuta mzee mmoja wakampiga kisha wakaingia kanisani na kumkaba shati muumini mmoja kabla ya kumkata ngwala na walikuwa wakiulizana ni huyu... hapana siyo huyu wanaulizana na kujibizana wao kwa wao, kisha ofisa mtendaji waliyeongozana (hakumtaja jina) naye akawaambia watoke nje,” alisema. Alidai kuwa walipotoka nje, waliwafungia waumini mlango kwa nje na baada ya muda walirudi na kumpiga risasi muumini mmoja ambaye alifariki dunia papo hapo.

“Najiuliza kwa nini wamekuja kufanya fujo kanisani tena siku ya sabato na kuua, inashangaza sana,” alisema.




Baadhi ya habari/taarifa kuhusiana na Mkurugenzi huyu:

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi amshukia vikali Waziri Jafo kwa kuupotosha umma!

Hivi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa mauza uza yake yote hajatumbuliwa tu?

Mkurugenzi Halmashauri ya Itigi atishia kuwasweka rumande walimu waliohamishwa kisa madai ya stahiki zao

Eti Meneja wa City Style Hotel naye kawa DED wa Itigi, jamani tuweni serious kama nchi
 
Aisee haya mambo ya kupigana risasi hivi bongo now yanaenda kuwa kawaida aisee
 
Back
Top Bottom