Singida: Godbless Lema afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, asomewa mashtaka 15

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,322
219,647
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless J Lema amefikishwa Mahakamani Singida leo Tarehe 25/03/2020 na kusomewa Mashitaka Kumi na Tano (15).
===

- NoHateNoFear ( 606 X 640 ).jpg

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida na kusomewa mashtaka 15 yanayomkabili.

Kati ya mashtaka hayo moja ni la kusababisha taharuki kwa jamii na 14 ya kupotosha jamii.

Amesomewa mashtaka hayo leo Jumatano Machi 25, 2020 na mawakili wa Serikali, Monica Mbogo, Rose Cholongola, Michael Ng’hoboko na Caren Malando mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Consolata Singano.

Imeelezwa kuwa Lema alitenda kosa hilo Februari 29, 2020 mjini Manyoni mkoani Singida katika mazishi ya kiongozi wa Chadema.

Anadaiwa siku hiyo na katika mitandao ya kijamii alisambaza taarifa za uongo kwa nia ya kupotosha jamii kuwa watu 14 wameuawa kwa kupigwa mkoani Singida.

Lema alikana mashtaka yote yanayomkabili na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 15, 2020 huku mbunge huyo akiachiwa kwa dhamana.

Pia soma >
Lema: Nimepewa orodha ya viongozi wa CHADEMA waliouliwa Manyoni na Polisi kutofanya uchunguzi

DPP Biswalo Mganga: Lema kuchukuliwa hatua kwa kupotosha vifo vya watu 14 Manyoni
 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema

Singida. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida na kusomewa mashtaka 15 yanayomkabili.

Kati ya mashtaka hayo moja ni la kusababisha taharuki kwa jamii na 14 ya kupotosha jamii.

Amesomewa mashtaka hayo leo Jumatano Machi 25, 2020 na mawakili wa Serikali, Monica Mbogo, Rose Cholongola, Michael Ng’hoboko na Caren Malando mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Consolata Singano.

Imeelezwa kuwa Lema alitenda kosa hilo Februari 29, 2020 mjini Manyoni mkoani Singida katika mazishi ya kiongozi wa Chadema.

Anadaiwa siku hiyo na katika mitandao ya kijamii alisambaza taarifa za uongo kwa nia ya kupotosha jamii kuwa watu 14 wameuawa kwa kupigwa mkoani Singida.

Lema alikana mashtaka yote yanayomkabili na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 15, 2020 huku mbunge huyo akiachiwa kwa dhamana.
 
Upelelezi umekamilika?
Haya mambo ndio huwa yanafanya mkuu wa nchi kila siku anashangaa juu ya wapelezi wetu na waendesha mashitaka. Mtu alichapisha orodha ya watu aliodai wamechinjwa kwa ishu zinazohusiana na siasa. Polisi wanasema sio kweli mauaji hayo yana mambo mengi ikiwemo wivu wa mapenzi na uhalifu ,sasa bado wanapeleza nini?
 
Yale maelezo aliyokuwa akitupa kwenye press sasa yamepata sehemu husika kuyapeleka.
 
Swali la msingi ni kweli ama siyo ukweli hicho alichoitaarifu jamii. Kama alisikia sikia tuu na hana uthibitisho apewe adhabu hata ya kunyukwa viboko (faru) 12 akiwa na kanga pekee iliyoloana maji ya pilipili na chumvi na video irushwe mtandaoni ili kukomesha uongo mambo ya kufungana ni msongamano
 
Na Bunge linafungwa leo
Hali si hali hakuna kutoka nje
Miji imekuwa kama ghost towns

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
CHADEMA wangekuwa na makambi ya kufunza na kutayarishi wanachama wake kuwa viongozi bora na wanaofuata siasa Safi kama ilivyo kwa CCM, matatizo haya ya mashtaka ya Mara kwa Mara kwa wapinzani yangekwisha. Ni mtazamo wangu.
Kama alivyofundwa makonda na kuwa kiongozi bora!kweli wasingekuwa wanafikishwa mahakamani kila kukicha.
Wakifanya kile alichofanya Makonda pale ubongo Jana leo wangekuwa kisutu wakisomewa mashitaka yasiyopungua 30 likiwemo la kupuuza Amri ya Rais kuhusu mikusanyiko na wasemaji wa janga la CORONA bahati mbaya akili hainunuliwi ninge..........
 
CHADEMA wangekuwa na makambi ya kufunza na kutayarishi wanachama wake kuwa viongozi bora na wanaofuata siasa Safi kama ilivyo kwa CCM, matatizo haya ya mashtaka ya Mara kwa Mara kwa wapinzani yangekwisha. Ni mtazamo wangu.

Ccm sio chama cha siasa bali ni kikundi cha dola kilichojivika koti la chama cha siasa. Ccm huwa tunaona ikitumia makundi ya wahalifu kufanya ukatili na uhayawani wa wazi kwa wapinzani, kwa uratibu wa vyombo vya dola. Haya wananchi huwa wanayaona na wanayajua, ila wanaogopa kuongea kuhofia usalama wao. Usidhani haya hayafahamiki. Siku ccm inatoka madarakani, nusu ya viongozi wake walio hai wataishia jela.
 
CHADEMA wangekuwa na makambi ya kufunza na kutayarishi wanachama wake kuwa viongozi bora na wanaofuata siasa Safi kama ilivyo kwa CCM, matatizo haya ya mashtaka ya Mara kwa Mara kwa wapinzani yangekwisha. Ni mtazamo wangu.
Hukusikia maneno ya katibu wako mkuu wa chama kule kilimanjaro kwenye mazishi ya Mengi?Au ni kujitoa ufahamu?Alisema Makonda ni zao la mfumo mbovu wa kuandaa viongozi vijana CCM!Sasa wewe unaropoka nini?
Awamu hii hakuna mpinzani haswa anaweza kufanya siasa bila kubambikiziwa kesi zisizo na msingi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom