baraka bb
JF-Expert Member
- Mar 20, 2016
- 2,691
- 3,862
weeeAaah wapi mimi huyu huyu
We piga tena tufanye yetu,maisha yenyewe mafupi haya,mara pap nikufe na sukari yangu ikaliwe na nyeyere si bora nikuonjeshe tu

ndo imeishaInaendelea
Nilifika Songea na kuanza kufanya biashara ya kununua na kuuza mahindi nilijichanganya na wazoefu biashara ikawa inaenda poa, pale nilipokuwa nimepanga kulikuwa na nyumba kama nne kwenye eneo moja kulikuwa kama kota,walipanga wafanyakazi na kuna jamaa wengine nao wafanyabishara wa mahindi na dili nyingine nyingi nyingi,dili chafu na safi walikuwa wamepanga pale pale.Nikaibiwa walivunja chumba changu na kikasafishwa kila kitu tene waliiba mchana,kuna vijana wawili walikuwa wamepigwa marufuku kuingia maeneo yale nilivyowaambia jamaa zangu wakawahisi wale vijana,wakaniambia nenda kwa Binti Ndembo ukawakomeshe,kipindi hiko Ruvuma kulikuwa na mganga anaitwa binti Ndembo alikuwa mashuhuri sana alikuwa anapatikana wilaya ya Namtumbo.
Sikwenda kwa binti Ndembo nilienda kwa mganga mmoja alikuwa anaishi karibu na msikiti wa mkoa nilifika kwake muda wa saa moja giza likiwa limeanza kuingia,nikaingia kwenye chumba cha uganga na kumuona mganga nikamueleza shida yangu akanisikiliza na kunitajia kiasi kidogo cha fedha ambacho aliniambia nitampa mara tu nitakavyopata vitu vyangu nikamuambia sawa,mganga akafanya uganga wake na alivyomaliza alianza kujaza upepo kwenye tyubu ya baiskeli aliniambia kadri anavyojaza na matumbo ya wale wezi nayo yatakuwa yanajaa
Duuuuuh maskhara hayaNinaandika lakini nakuta imefutika ilikuwa inaisha sasa naanza tena
kutamka tu yanga umetukwaza wengine, inaonekana hii story Ni ya Simba tu, hivyo kwaheri ndugu yangu, machungu ninmengi Sina mda wa kuhangaika naweWaungwana habari ya leo fuatana nami kwenye simulizi yangu hii ambapo niliwahi kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi baada ya kukutana na changamoto mbalimbali za kimaisha.
Kiukweli ni vigumu kumjua yupi ni mganga wa kweli na yupi ni mganga feki ni kama vile ambavyo huwezi kumjua yupi ni mtumishi wa Mungu wa ukweli na yupi ni feki.Hali hiyo ilinifanya nihangaike kwa waganga mbalimbali ili kutatua changamoto zangu.
Wale ndugu zangu Walokole na Watakatifu wengine msiokuwa na dhambi mtanisamehe kwa hii simulizi.
Baada ya kumaliza masomo mwaka 2008 niliamua kurudi nyumbani kwetu Chunya na kujiajiri,sikupenda kuajiriwa kwa sababu kwetu Chunya marafiki zangu ambao nilisoma nao shule ya Msingi walikuwa wameishia darasa la saba walikuwa na pesa kushinda wasomi waliokuwa wameajiriwa na Serikali.
Hao marafiki zangu walikuwa machimboni kwa kuchimba au kununua dhahabu.Na Mimi nikajikita kwenye kuchimba lakini kabla ya hapo wakati nilipokuwa nasoma nilipokuwa napata nafasi nilikuwa naenda mgodini,ilikuwa rahisi kwenda machimboni kwa sababu kulikuwa na watu wengi niliokuwa nafahamiana nao.
Baada ya kuanza rasmi kuchimba madini niligundua machimboni kumetawaliwa na ushirikina wa hali ya juu,ndipo na mimi nikaanza kwenda kwa waganga wa kienyeji na kama ilivyo ada ukienda Roma ishi kama Waroma.Safari yangu ya kwenda kwa waganga ilianza kama ifuatavyo:
Mganga wa Ziwa Rukwa
Sikumbuki jina la kijiji ila kilikuwa karibu na ziwa Rukwa,nilienda kupitia Tunduma, naikumbuka barabara ilikuwa ya vumbi, milima, mabonde, miamba na yenye kona nyingi kali nilienda kwa kutumia fuso. Kijiji kilikuwa na Wafugaji wa Kisukuma wengi waliokuwa na mifugo mingi pamoja na wenyeji waliokuwa wakulima hodari wa mpunga kwenye bonde la ziwa Rukwa.
Niliipenda sana lugha ya Wenyeji kwani walikuwa wanaongea kama wanaimba au wanavuta maneno ,aina yao ya uongeaji ilinivutia sana.
Nilifika asubuhi na kumuona mganga,mganga mzee wa zaidi ya miaka sitini alikuwa hana vitu vingi vya kumtambulisha kama ni mganga wa kienyeji, nilimueleza sababu ya kwenda kwake akafanya uganga wake akaniambi usiku wa saa nane tutaenda kumalizia kufanyia uganga wake ziwani kwani huko ndiko kwenye mizimu yake, kutoka kwake hadi ziwa Rukwa kwa miguu ni saa mbili kwahiyo tulitoka kwake saa sita usiku ili tuweze kufika ziwani saa nane.
Tulitoka kwake watu wanne yaani mimi, mganga na watu wengine wawili, tulifika ziwani saa nane kasoro wakati tunaenda ilikuwa rahisi kwa sababu ilikuwa tunashuka tu kasheshe ilikuwa wakati wa kurudi kwani tulikuwa tunapandisha milima, usiku ule nilichoka sana.
Tulivyofika kwenye ufukwe wa ziwa mganga alituambia tugeuge tuangalie tulikotoka kisha alivua nguo zote akasisitiza tusimuangalie,wakati yeye anafanya uganga wake huku anaonge ongea maneno ambayo sikuyajua maana yake sisi wote watatu tulikuwa tunangalia pembeni.
Baada ya muda kidogo kukawa kimya, baada ya kama dakika tano nikasikia naitwa kwa kutajwa jina, sauti ilikuwa kubwa na yenye muungurumo, muda huo sehemu ile ya ziwa tulikuwa watu wanne tu sauti ile iliendelea kuniita lakini mtu aliyekuwa ananiita nilikuwa simuoni ila ilikuwa sauti ya mganga.
Sauti ilinitaka nielekee usawa wa ziwa, mimi kuogelea sijui ila sauti ilikuwa inanitaka niingie ziwani,wale jamaa wakaniambia kwa ukali niingie ziwani maana nilikuwa natembea kwa kusita sita, nilifika ziwani nikaingia kwenye maji nikawa naendelea kutembea kwenye maji kwa kusita sita sikuwa namuona mganga ila sauti nilikuwa naisikia ikiniambia niendelee kumfuta.
Niliendelea kutembea maji yalivyofika usawa wa magoti sauti ikanitaka nisimame nisiendelee kumfuata na mimi nikatii.
Itaendelea.
Sasa hivi najiandaa kwenda Mkwakwani kuwaona watani Yanga dhidi ya Coastal kwenye mechi yao itakayo chezwa saa kumi leo,nawatakia sare tu.
Nielekezeni jinsi ya kuipost hapa maana niliiandika yote imekamilika na ipo kwenye flash.
ila mi Ni Simba dam dam, sijapenda tu ulivyohusisha ushabiki na story yako, hkukuwa na sababu Wala maanaWaungwana habari ya leo fuatana nami kwenye simulizi yangu hii ambapo niliwahi kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi baada ya kukutana na changamoto mbalimbali za kimaisha.

kweli jamani, Mimi pia mnitag, Mana uyu fala anajiona tuna shida Sana na story yake, Yani imekua trend Sasa jf, kwamba itaendeleaaa, naomba muwaambie mods kwamba hi Ni trend inatusumbua Sana wateja wao waipige ban, yaani unasema tu itaendeleaaa inakuwa ban ya miezi sita, Kuna wale wanaweka mwendelezo kwa link kwenye post yao ya Kwanza, wapewe heshima na ulinzi wa jktakiishusha yote naomba nishtue maana huyu mapicha picha kaanza mapema sana
Nenda zako, hujaitwa huku . Vitu vidogo misuli ya shingo inakukakamaa, hovyooo Kwan unamlipa? Mfyuu,ila mi Ni Simba dam dam, sijapenda tu ulivyohusisha ushabiki na story yako, hkukuwa na sababu Wala maana
Mkuu unamlipa nn? Ana kazi zake yaani kuna watu hamjielewagi eti na komandi juu kwani unalipa?kweli jamani, Mimi pia mnitag, Mana uyu fala anajiona tuna shida Sana na story yake, Yani imekua trend Sasa jf, kwamba itaendeleaaa, naomba muwaambie mods kwamba hi Ni trend inatusumbua Sana wateja wao waipige ban, yaani unasema tu itaendeleaaa inakuwa ban ya miezi sita, Kuna wale wanaweka mwendelezo kwa link kwenye post yao ya Kwanza, wapewe heshima na ulinzi wa jkt
Thanks,nilichelewa kuiona,hata hivyo nilitoka mapema goli la pili la wagosi sikuliona.Daraja la miti
Kama upo kweli Mkwawani njoo upande wa jukwaa kuu kulia, tafuta mtu aliyevaa t-shirt ya njano isiyo na maandishi na nimevaa kofia nyeupe, pembeni yangu yupo mwanamsimbazi na jezi yake.
Kama una smartphone nina OTG hapa nitakuwekea story yote kupitia simu yako alafu utapost mwenyewe.
kweli kabisa mkuu, Waganga wameiteka vilivyo jamii yetuBaada ya msimu huu wa stori za nguvu za giza, ufuatiwe na msimu mpya wa NGUVU ZA MUNGU jinsi zilivyonasua wadau katika majanga! Maana Ibilisi katukuzwa sana msimu huu!!
Sawa.Thanks,nilichelewa kuiona,hata hivyo nilitoka mapema goli la pili la wagosi sikuliona.