Simu za wanandoa nyingi ni chafu, hawaingii majumbani mwao mpaka wazisafishe

twijuke

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
547
252
Je! Ndoa ni utwamwa? Nini chanzo cha yote haya? Jana usiku nikiwa na jamaa yangu, ilinilazimu nipite kwake kuna ka mzigo kangu kaliachwa kwake. Kabla hatujaingia ndani aliniambia subiri kwanza nisafishe sim yangu ni chafu nikiingia nayo ndani kitanuka.

Nikiwa kwenye hali ya bumbuwazi nisijue anamaanisha nini, ilinilazimu niulize kwani ni ya mama ulidondosha chini? Akacheka sana, akasema hapana! Kuna ma sms nayafuta na mamiss call, bila aibu jamaa alipigia watu si chini ya 7 kuwajulisha wasimtafute amefika nyumbani. Ebu tafakari mtu ana michepuko zaidi ya 7 na kila mchepuko unapiga mnyonyo.
 
J

..... Ebu tafakari mtu ana michepuko zaidi ya 7 na kila mchepuko unapiga mnyonyo....

Duuuu, hiyo sentensi juu imenishanga kidogo, watu 7? Labda inawezekana siyo michepuko kwa maana ya michepuko huenda ni meseji za utani wa ndani zinazosababishwa na kuzoeana na watu kupitiliza.
Huwa nashauri kila siku, ni vyema wapenzi na wanandoa kuwa na mipaka ya utani na mawasiliano na watu wasio wapenzi wao, vinginevyo, iko siku kitanuka!

HP
 
we unashangaa hao saba tu? watu wanamsululu wakiwapanga barabani wanaweza kuanza kariakoo hadi mwanjelwa mbeya.......yaani hadi vifanyio vinaomba poo

Uliza wababa wenye ndoa hapa, aliyemo kwenye ndoa ya miaka mi5 kwenda juu ametembea na wangapi? Ikiwa watu ni wakweli tutashuhudia maajabu hapa.
 
Sasa ina maana hujui kiswahili fasaha, mtu mmoja ni mwanandoa so ungetuambia "simu ya mwanandoa ni chafu" sio simu za wanandoa. Uchafu na usafi ni mambo binafsi acha ku generalize
 
mmmhhh kwel kaz ipo kuna haja ya kuwa tunazitoa risasi,atembee na bastola tupu
 
Sasa ina maana hujui kiswahili fasaha, mtu mmoja ni mwanandoa so ungetuambia "simu ya mwanandoa ni chafu" sio simu za wanandoa. Uchafu na usafi ni mambo binafsi acha ku generalize

Nimesema nyingi ni chafu, maana yake sipo chache safi ikiwemo yako, kweli kiswahili sijui waweza nielekaza au tungoje wajuzi.
 
Nimesema nyingi ni chafu, maana yake sipo chache safi ikiwemo yako, kweli kiswahili sijui waweza nielekaza au tungoje wajuzi.

Kichwa cha habari wanandoa wengi, mfano uliotoa ni mwanandoa mmoja. Inawezekana unachosema ni kweli lakini hapa bado hauja justify, na hivyo kutusababishia wanandoa wengi pressure zisizo za lazima.
 
usafi sio wa mazingira tu hata simu inatakiwa kuwa safi so nafuta kila kisichostahili kwa simu yangu kulingana na muktadha hahahaaaaa
 
Je! Ndoa ni utwamwa? Nini chanzo cha yote haya? Jana usiku nikiwa na jamaa yangu, ilinilazimu nipite kwake kuna ka mzigo kangu kaliachwa kwake. Kabla hatujaingia ndani aliniambia subiri kwanza nisafishe sim yangu ni chafu nikiingia nayo ndani kitanuka.

Nikiwa kwenye hali ya bumbuwazi nisijue anamaanisha nini, ilinilazimu niulize kwani ni ya mama ulidondosha chini? Akacheka sana, akasema hapana! Kuna ma sms nayafuta na mamiss call, bila aibu jamaa alipigia watu si chini ya 7 kuwajulisha wasimtafute amefika nyumbani. Ebu tafakari mtu ana michepuko zaidi ya 7 na kila mchepuko unapiga mnyonyo.

Unatudhalilisha wenye ndoa zetu bana, we ukutane na mtu mmoja tu ndiyo useme wenye ndoa wengi?? Kwa nini usiseme wachache kwa sababu uliyekutana nae ni mmoja?? Method yako uliyotumia kupata sample si sahihi kabisaaa
 
Back
Top Bottom