Kajuni
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 486
- 186
Wana JF kwanza kabisa shalom. Ni jumamosi tulivu pande za hapa Dar na hali ya hewa ni manyunyu manyunyu! Nikiwa katika harakati za kumalizia vipolo vya kazini mara napokea simu kutoka kwa baba mkwe. Namsalimia kwa heshima na tahadhima kwani ndiye mzaa chema (mke wangu). Ama baada ya salamu baba mkwe ana anza kunishutumu kwamba sisi pamoja na binti yake hatuwaheshimu na hatuwajali kwa sababu jana tulishindwa kupeleka japo ua kwa mama mkwe kama zawadi ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa. Baba mkwe aliendelea kutiririka kwamba sisisi tumekuwa na mkono wa birika! Na hata siku moja hatujawahi kuwapa zawadi japokuwa wao wamekuwa mstari wa mbele katika hilo.
Kikubwa ni kwamba mimi nimezaliwa na kuishi na kusomea kwenye hizi shule zetu za kayumba! Uaratibu huu wa kushelekea siku za kuzaliwa nilianza kukuana nao nikiwa chuo kikuu. Sikuwahi kushelekea katika kukua kwangu wala sikumuona baba na mama yangu wakitunulia zawadi wakati wa hii siku nyeti. Sina nia mbaya ya kutopeleka zawadi kwa mama mzaa chema lakini mazingira niliyokulia yanachangia sana mimi kutokuwa sensitive na hizi ishu!
Sasa wandugu nifanyeje kwani Jumamosi leo nimeambulia lawama na shutuma.