JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Mbali na adhabu hiyo, Mshtakiwa ametakiwa na Mahakama hiyo kumlipa Mwathirika kiasi cha Sh. 300,000 (Laki tatu) kama fidia kutokana na kitendo alichomfanyia.
Hakimu wa Mahakama hiyo Robert Kaanwa, wakati akitoa hukumu hiyo ameamuru Mshitakiwa kupimwa kwanza Afya yake na Daktari kama anaweza kuhimili adhabu hiyo ya viboko.
Awali, kabla ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Wilaya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Jaston Mhule alielezea Mahakama kuwa Mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130(1)(2)e na 131(2) vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo Mwaka 2022.
Mhule ameeleza kuwa Mshtakiwa akiwa katika msiba wa Babu yake mnamo tarehe 10/07/2023 huko Kijiji cha Mahembe ndani ya Wilaya Itilima alimbaka mhanga mwenye umri wa Miaka 17 na kumsababishia maumivu.
Mhule amesema Sheria inaweza isizungume moja kwa moja muathirika kupewa fidia lakini Mahakama inaweza kuamua hivyo kutokana na kusikiliza pande, ndipo inaweza kuamua fidia au la.
Kifungu cha 131 Kifungu Kidogo cha Pili cha Sheria Kanuni ya Adhabu inaeleza kama mshtakiwa wa kesi ya ubakaji akiwa na umri wa miaka 18 kushuka chini adhabu yake ni viboko tu, idadi ya itategemea na afya ya mhusika.
Mshtakiwa kabla ya kuchapwa viboko inatakiwa afanyiwe vipimo vya afya na Daktari atoe cheti cha kuonesha kuwa kwa idadi vya viboko ambayo amehukumiwa na Mahakama inaweza kumfaa au inatakiwa kupunguziwa adhabu.
Sheria inaeleza mshtakiwa wa ubakaji akiwa na umri wa miaka 19 kuendelea akikutw ana hatia kifungo cha chini ni miaka 30 na inaweza kwenda mbele zaidi ya hapo hadi kuwa kifungo cha maisha.