SIMBA - Sitamuonea haya fisadi hata aje na bilioni

Kauli yake inatia kichefu chefu hana maadili wala hana moral authority ya kuongea maswala ya ufisadi. Inatia kinyaa na inachukiza kuwafanya watanzania (wanawake) wajinga. anathibitisha yaliyosemwa na Macelecela aende akapime kichaa. dodoma alikuwa anshambulia wapambanaji an kukumbatia mafisadi sasa hivi anapambana na mafisadi. yote haya yanasababishwa na wananchi kutojua haki za uraia pia ujinga uliokisiri kwenye jamii zetu. ndo maana naongea vitu kwa kujiamini bila kuzomewa
 
Kwa hiyo tuseme anatuambia kwamba kuna waliomfuata na hesabu pungufu ya hiyo bilioni? Ni kama vile alishafuatwa na labda tuseme milioni kadhaa akawatolea nje.....mawazo yangu tu.
 
Yaani katika mawaziri waliofilisika kisera ambao sijui kwanini rais hawashushi ni huyu Sophia Simba, hivi hana uhusiano na yule Iddi?? maana Simba wamezidi sasa kutajwa kwenye ufisadi (Nicol)

Kitwana kondo huyo
 
Hata aje na bilioni? Vipi bilioni mbili?

The Mafia says every man (and presumably woman) has a price, so are you advertising your price range minister Simba? What is your price?
 
Sielewi ni vigezo gani Raisi anatumia katika kuwachagua mawaziri na hasa wale wanaoshika wizara nyeti kama ya huyu Mama Sophia Simba.

Tokana na kuchambua maelezo ya mama huyu mama inaonesha wazi kwamba hapaswi kuwa katika baraza la mawaziri achilia mbali kuwa mkuu wa wilaya. Kama Raisi anataka kuwashirisha wanawake wa Tanzania katika baraza la mawaziri kuna wanawake wana akili timamu na uwezo wa kuongoza vyema kabisa kuzidi huyu mama.

Kuna wanawake kama Dr Suma Kaare ambaye amebobea vyema kabisa katika fani ya Utawala (hili linaweza kuthibitishwa kama mta - google na kuangalia kazi zake alizofanya), na pia kuna Mwanadada kama Rosemary Mwakitwange ambaye naye amebobea vyema katika masula ya utawala. Kwanini tuwe na mawaziri bomu na vilaza kama Sophia Simba?

wako tayari kukubali masharti ?. Usifikiri wanawekwa burebure.
Nina imani wanawake makini hawatakubali masharti kama kina sofia.
 
jamani huyu mh Simba nimeambiwa kaokoka kampa yesu maisha yake,na ansali kwa mama rwakatare ni kweli?
 
mama kwa nini unaangalia Kibanzi ndani ya jicho la mwenzio ? ondoa kwanza Boliti linalokutesa wewe kisha ndo uendelee na harakati zako
 
Huyu mama inaelekea mla rushwa kulinganisha thamani ya uadilifu na hela! Je tujiulize what if ze fisadi anakuja na billioni 2 atamwonea haya? Hivi serikali huwa inawazowa hawa watu wapi kupewa madaraka makubwa namna hii? :confused:
 
Nafikiri Sofia ni kweli anatakiwa aende Mirembe yaani uropokaji wake ni wa kiwango kingingine cha kutisha! Imagine kina mama hao wasio mjua wanaona "Maskini we huyu mama anajitahidi kupambana na mafisadi ya kiume" wasijue kuwa loh yeye ndio mamalao mafisadi! Mdaku, hafai, lakini wananchi walimkataa kwenye kura! JK kamteua ubunge, halafu kampa uwaziri, full ministerial position, halafu ofisi nyeti kama hiyo?? hivi kuna nini????????!!!!!!!:eek:
 
Sophia Simba hafai kuwa Waziri wa Utawala Bora
ban.mtazamo.jpg

Irene Mark

amka2.gif

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Mnyambi Simba, kwa mara nyingine tena amezua mjadala na kuamsha hisia za waliosinzia kuhusu utata wa utumishi wake ndani ya Serikali ya Awamu ya Nne chini ya mwamvuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ni mara nyingine kwa sababu huko nyuma amewahi pia kutoa kauli zenye ukakasi akimshambulia mfanyabiashara na mmoja wa wafadhili wa chama tawala kilichomweka waziri huyo madarakani.
Ni huyu huyu Sophia ambaye chama chake kimekanusha matamshi aliyotatoa mbele ya kadamnasi kuwashambulia wabunge wa kuchaguliwa walio mume na mke – John Malecela na Anne Kilango Malecela.
Ni huyu Sophia mwenye dhamana ndani ya wizara nyeti ya Utawala Bora, yenye wajibu wa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma, iliyo chini ya Ofisi ya Rais.
Ni Sophia ndiye anayewajibika katika kusimamia na kutekeleza kiapo chake cha utii na kumshauri vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa, bila migogoro yoyote.
Ni huyu Sophia, ambaye ndani ya chama chake, amekabidhiwa dhamana ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) - wanaokiamini, kukipenda na kukitumikia chama tawala, yaani CCM.
Ni huyu Sophia aliyedaiwa kumwangushia kipigo, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Janeth Kahama, wakati wa mchakato na kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa wanawake hao kwa njia ya kura.
Ni Sophia huyu huyu, aliyewahi kukaririwa na vyombo vya habari akiwatetea wafanyabiashara wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kuzua gumzo na kuharibu upepo wa nchi wakati huo.
Sophia Simba, kwangu ni mwanamama anayekurupuka. Ni Waziri asiyejipa muda wa kutafakari na kueleza anachokifahamu. Wakati mwingine nahisi anatumika ama kwa nia ovu au kwa maslahi ya taifa ili kuharibu mwelekeo ama kuwasahaulisha walalahoi kero zinazowakabili.
Ni Sophia, aliyejaribu kucheza ngoma tofauti ya vita dhidi ya ufisadi iliyoanzishwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kupokelewa kwa shangwe wa wakuu wa chama chake, akiwemo rais aliyemteua kushika nafasi ya uwaziri.
Ni Sophia aliyewashangaza wasomi na wasio wasomi, pale alipojiinua na kuishambulia familia ya wanasiasa, akiwemo mkongwe, Mzee Malecela.
Ni huyu Waziri Sophia aliyewaacha vinywa wazi wachambuzi, wajuzi na wananchi wa kawaida pale alipowashambulia kwa tuhuma mbalimbali wanasiasa wenzake.
Ni wapi alipokuwa Sophia kiasi cha kuzikalia tuhuma nzito za wanasiasa hao na kujinasibu kwamba ndani ya chama chao cha CCM hakuna msafi, wote ni mafisadi?
Ni imani yangu kwamba Sophia anahitaji kubanwa ili aanike tuhuma zote anazozifahamu, pengine atalisaidia taifa na kulirejesha kwenye mstari ili walalahoi waone raha na faida ya kuzaliwa juu ya ardhi ya Tanzania.
Pamoja na yote, nina ushauri kwa mkuu wake wa kazi. Kwanza amfukuze kwa sababu amejidhihirisha kwamba hafai kuwa kiongozi wa wanyonge kwa sababu ameshindwa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma. Sophia aanze kufuatiliwa, ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Polisi na Usalama wa Taifa. Ni Imani yangu kwamba kuondolewa kwa waziri huyu katika nafasi aliyonayo, kutabadili fikira zangu kwamba analipwa fadhila za mema machache aliyoyatenda wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
 
.
Sophia Simba hafai kuwa Waziri wa Utawala Bora
ban.mtazamo.jpg

pdidy.swi

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Mnyambi Simba, kwa mara nyingine tena amezua mjadala na kuamsha hisia za waliosinzia kuhusu utata wa utumishi wake ndani ya Serikali ya Awamu ya Nne chini ya mwamvuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ni mara nyingine kwa sababu huko nyuma amewahi pia kutoa kauli zenye ukakasi akimshambulia mfanyabiashara na mmoja wa wafadhili wa chama tawala kilichomweka waziri huyo madarakani.
Ni huyu huyu Sophia ambaye chama chake kimekanusha matamshi aliyotatoa mbele ya kadamnasi kuwashambulia wabunge wa kuchaguliwa walio mume na mke – John Malecela na Anne Kilango Malecela.
Ni huyu Sophia mwenye dhamana ndani ya wizara nyeti ya Utawala Bora, yenye wajibu wa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma, iliyo chini ya Ofisi ya Rais.
Ni Sophia ndiye anayewajibika katika kusimamia na kutekeleza kiapo chake cha utii na kumshauri vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa, bila migogoro yoyote.
Ni huyu Sophia, ambaye ndani ya chama chake, amekabidhiwa dhamana ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) - wanaokiamini, kukipenda na kukitumikia chama tawala, yaani CCM.
Ni huyu Sophia aliyedaiwa kumwangushia kipigo, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Janeth Kahama, wakati wa mchakato na kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa wanawake hao kwa njia ya kura.
Ni Sophia huyu huyu, aliyewahi kukaririwa na vyombo vya habari akiwatetea wafanyabiashara wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kuzua gumzo na kuharibu upepo wa nchi wakati huo.
Sophia Simba, kwangu ni mwanamama anayekurupuka. Ni Waziri asiyejipa muda wa kutafakari na kueleza anachokifahamu. Wakati mwingine nahisi anatumika ama kwa nia ovu au kwa maslahi ya taifa ili kuharibu mwelekeo ama kuwasahaulisha walalahoi kero zinazowakabili.
Ni Sophia, aliyejaribu kucheza ngoma tofauti ya vita dhidi ya ufisadi iliyoanzishwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kupokelewa kwa shangwe wa wakuu wa chama chake, akiwemo rais aliyemteua kushika nafasi ya uwaziri.
Ni Sophia aliyewashangaza wasomi na wasio wasomi, pale alipojiinua na kuishambulia familia ya wanasiasa, akiwemo mkongwe, Mzee Malecela.
Ni huyu Waziri Sophia aliyewaacha vinywa wazi wachambuzi, wajuzi na wananchi wa kawaida pale alipowashambulia kwa tuhuma mbalimbali wanasiasa wenzake.
Ni wapi alipokuwa Sophia kiasi cha kuzikalia tuhuma nzito za wanasiasa hao na kujinasibu kwamba ndani ya chama chao cha CCM hakuna msafi, wote ni mafisadi?
Ni imani yangu kwamba Sophia anahitaji kubanwa ili aanike tuhuma zote anazozifahamu, pengine atalisaidia taifa na kulirejesha kwenye mstari ili walalahoi waone raha na faida ya kuzaliwa juu ya ardhi ya Tanzania.
Pamoja na yote, nina ushauri kwa mkuu wake wa kazi. Kwanza amfukuze kwa sababu amejidhihirisha kwamba hafai kuwa kiongozi wa wanyonge kwa sababu ameshindwa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma. Sophia aanze kufuatiliwa, ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Polisi na Usalama wa Taifa. Ni Imani yangu kwamba kuondolewa kwa waziri huyu katika nafasi aliyonayo, kutabadili fikira zangu kwamba analipwa fadhila za mema machache aliyoyatenda wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005
 
Sielewi ni vigezo gani Raisi anatumia katika kuwachagua mawaziri na hasa wale wanaoshika wizara nyeti kama ya huyu Mama Sophia Simba.

Tokana na kuchambua maelezo ya mama huyu mama inaonesha wazi kwamba hapaswi kuwa katika baraza la mawaziri achilia mbali kuwa mkuu wa wilaya. Kama Raisi anataka kuwashirisha wanawake wa Tanzania katika baraza la mawaziri kuna wanawake wana akili timamu na uwezo wa kuongoza vyema kabisa kuzidi huyu mama.

Kuna wanawake kama Dr Suma Kaare ambaye amebobea vyema kabisa katika fani ya Utawala (hili linaweza kuthibitishwa kama mta - google na kuangalia kazi zake alizofanya), na pia kuna Mwanadada kama Rosemary Mwakitwange ambaye naye amebobea vyema katika masula ya utawala. Kwanini tuwe na mawaziri bomu na vilaza kama Sophia Simba?

kweli wapo vizuri.afu hawa wote ni mtu na dada yake
 
Ha! Ha! Haaaa! Sofia simba unatamani maneno haya yarudi kinywani , lakini wapi !
 
sielewi ni vigezo gani raisi anatumia katika kuwachagua mawaziri na hasa wale wanaoshika wizara nyeti kama ya huyu mama sophia simba.

Tokana na kuchambua maelezo ya mama huyu mama inaonesha wazi kwamba hapaswi kuwa katika baraza la mawaziri achilia mbali kuwa mkuu wa wilaya. Kama raisi anataka kuwashirisha wanawake wa tanzania katika baraza la mawaziri kuna wanawake wana akili timamu na uwezo wa kuongoza vyema kabisa kuzidi huyu mama.

Kuna wanawake kama dr suma kaare ambaye amebobea vyema kabisa katika fani ya utawala (hili linaweza kuthibitishwa kama mta - google na kuangalia kazi zake alizofanya), na pia kuna mwanadada kama rosemary mwakitwange ambaye naye amebobea vyema katika masula ya utawala. Kwanini tuwe na mawaziri bomu na vilaza kama sophia simba?

swali dogo , je hao ni wenzetu ?
 
Hivi jameni Watanzania tunaelekea wapi? Hizi lawama zetu za mafisadi zinaishia humu kwenye JF au zinawagusa wahusika. We need to get rid of these mafisadi!!!! Hivi ile E-mail ya muulizerais@yahoo.com bado inatumika? if yes we need to use it!!!

Thubutu yake ! Tovuti ya tume ya warioba imefungwa , sembuse hiyo ?
 
Back
Top Bottom