Simba sc: Mshusheni shipa mbuyu twite

mwakitundilo

Member
Aug 15, 2012
28
7
Nimeudhishwa sana na kitendo cha kitapeli na kisichokuwa cha kiuanamichezo kilichofanywa na mchezaji MBUYU TWITE wa APR ya Rwanda. Mchezaji huyu alisajiliwa na Simba SC kutoka APR, lakini katika hali ya kustaajabisha mchezaji huyu akiwa kishalipwa kitita cha USD 30,000 kaamua kusajili pia YANGA. Nawashauri wanachama, viongozi, mashabiki na "wazee" wa Simba kumtia adabu mkongoman huyu ili awe fundisho kwa wachezaji wengine wenye tabia kama hiyo. Adhabu ninayopendekeza ni kumshusha shipa naamini "wazee" wangu wa Simba hili liko ndani ya uwezo wenu. NAWASILISHA​
 
Though! what he did is not acceptable anywhere, but that is not punishment and remedy he deserve.
 
Acheni kupiga mayowe,yapo mambo matatu ambayo yamemfanya beki Mbuyu Twite wa APR ya Rwanda, aachane na Simba SC na kuamua kujiunga na YANGA.

Mambo hayo ambayo kwa mjumuisho unaweza kuyaita ‘Ujanja ujanja wa mjini’ wa viongozi wa klabu hiyo ndio leo, yanaiponza klabu hiyo kumpoteza aina ya mchezaji ambaye walimuhitaji sana kwenye kikosi chao ili kujiimarisha.

Mosi; Namna ambavyo ‘walimuenzi’ kiungo Patrick Mutesa Mafisango (sasa marehemu), pili; desturi ya kuwaacha wachezaji wa kigeni baada ya kuwasajili, hata kabla hawajaitumikia timu mfano Lino Masombo, Derrick Walullya na wengineo na tatu hadhi ya klabu yao kwa sasa ukilinganisha Yanga na Azam FC.
Habari za kiuchunguzi zinasema kwamba Mbuyu alilishwa ‘sumu’ za kutosha ili aichukie Simba, kwanza klabu hiyo ilivyoutelekeza mwili wa marehemu Mafisango baada ya kifo chake, ambao hakuna kiongozi mkuu wa klabu hjiyo hata mmoja aliyekwenda kumzika DRC, zaidi ya Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji na mchezaji mmoja.
Pamoja na namna ambavyo Simba hawakujali kabisa mambo mengine muhimu kuhusu marehemu Mafisango, kama arobaini yake na kadhalika, Wakongo wameichukulia hiyo kama ni dharaua na ulipotokea mjadala Mbuyu aende wapi, watu wa Kongo wakamnyooshea kidole kinachoelekeza Jangwani.
Ikumbukwe, Mafisango aliyejiunga na Simba akitokea Azam FC, iliyomsajili kutoka APR ya Rwanda, alifariki akiwa mchezaji muhimu ndani ya Simba akiongoza kwa kufunga mabao na mwenye mchango mkubwa kwenye timu.
Simba, hivi karibuni ilimsajili mchezaji Lino Masombo kutoka DRC, lakini baada ya mwezi mmoja na ushei ikamtema kama ilivyofanya kwa Mganda, Derrick Walullya msimu uliopita, hilo limetajwa kumsitisha Mbuyu kuangukia Msimbazi na kuamua kurudisha fedha zote alizochukua kwa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage (dola za kimarekani 30,000 kwa mujibu wa Simba).
Lakini pia, wakati Mbuyu anasaini Simba kuchukua fedha, alikuwa hajui kwamba katika soka ya Tanzania hivi sasa, klabu ambazo zinachuana kwa ‘utajiri’ ni Yanga, ambao Mwenyekiti wao Yussuf Manji ni mfanyaiashara mkubwa na Azam FC ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara mwingine, Said Salim Bakhresa.
Yanga imemsajili Twite, wakati tayari akiwa amekwishaini Simba SC, baada ya kumrudisha kwenye uraia wake wa asili, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), badala ya Rwanda aliopewa wakati akicheza nchini humo na kumbadili jina pia.
Kwa kumbadili uraia, Yanga walipata na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji huyo, kutoka Shirikisho la Soka (DRC), na kuwaacha Simba wakihangaika bila mafanikio kupata ITC ya mchezaji huyo kutoka FERWAFA, Shirikisho la Soka la Rwanda.
Yanga inamsajili Twite kama mchezaji kutoka St Eloi Lupopo, klabu ambayo aliichezea kabla ya kutua APR mwaka 2006 kwa pamoja na ndugu yake, Kabange. Lakini mchezo uliochezwa hapa ni kwamba Twite alikuwa anacheza kwa mkopoAPR.
Habari zaidi zinasema, Yanga inamsajili pia na pacha wake Mbutu (pacha wa kuzaliwa kabisa), Kabange, kwa sababu wachezaji hao kawaida yao kucheza timu moja daima.
 
nimeudhishwa sana na kitendo cha kitapeli na kisichokuwa cha kiuanamichezo kilichofanywa na mchezaji mbuyu twite wa apr ya rwanda. Mchezaji huyu alisajiliwa na simba sc kutoka apr, lakini katika hali ya kustaajabisha mchezaji huyu akiwa kishalipwa kitita cha usd 30,000 kaamua kusajili pia yanga. Nawashauri wanachama, viongozi, mashabiki na "wazee" wa simba kumtia adabu mkongoman huyu ili awe fundisho kwa wachezaji wengine wenye tabia kama hiyo. Adhabu ninayopendekeza ni kumshusha shipa naamini "wazee" wangu wa simba hili liko ndani ya uwezo wenu. Nawasilisha​

mbona povu limekujaa, nasi tutamuotesha busha bw mwakitundilo kwa wivu
 
tusilipe baya kwa baya bali tunamtakia mafanikio mema huko kwenye yeboyebo na arudishe pesa zetu za usajili ili siku tukiwafunga wasiseme kwamba amehujuma timu kwakulipa fadhila kwa simba
 
unacheza wewe!!uchawi wa ki-congo uko juu kuliko wa kibongo,au unataka kumuona mwenyekiti wenu akiwa na mashipa!!!!ha ha ha ha ha!!
 
unacheza wewe!!uchawi wa ki-congo uko juu kuliko wa kibongo,au unataka kumuona mwenyekiti wenu akiwa na mashipa!!!!ha ha ha ha ha!!

Ni sawa na kutisha vita Syria mkuu, kiukweli uchawi wa kibongo haupandi kwa wanigeria na wacongo.
 
kwa taarifa yako katika vilabu hivi viwili yanga na simba uchawi wa kweli ni 1% kwani kila mechi wanazocheza ziwe za kirafiki au ligi ya aina yoyote ndani na nje ya nchi lazima waende kwa babu (kuloga) hii ndio jadi yao lakini katika huko kutafuta uchawi hawafanyi lolote bali kuchukua fedha za uchawi pasipo kuwa na uhakika wa uchawi huo. mwanachama anaweza akamchukua mjomba wake kutoka kijijini kwao mwenye sura mbaya au barakashia akamleta klabu na kuwaambia viongozi kwamba huyu ni mchawi + mganga bahu kubwa kutoka Liwale au Rufiji na viongozi hao wanaamini na kutoa fedha, kwa kuwa wao pia wana bili kubwa ya uchawi wanayoiandikia pesa kibao katika kila mechi, kwa maana hiyo wanaoweza kumshusha MSHIPA Twite siku hizi hawapo bali utapeli na kujinufaisha fanya uchunguzi utaambiwa kuna akaunti ya kamati ya ufundi sio ufundi wa kiwanjani tu bali ufundi uchawi feki
 
MBU HUYU ATUITE!! atakiona chamtema kuni, ajue kuwa sisi hapa ni nyumbani na yeye ni mgeni hapa. cdhani kama atakuwa huru kucheza soka la kiwango kinachokubalika maana tutamzomea kila akigusa mpila maka achanganyikiwe ki saikolojia.
 
Sio kishipa tu, na kumuotesha ugonjwa wa matende. Haijuwi simba huyo kwan mafisango hakuwa mkongo? Mbona alikufa kama kuku wa mdondo.
 
Sikujua kuwa kumbe simba inayo taaluma ya mambo ya jinsi ya uchawi? Hii inaogopesha kwenye masuala ya soka!
 
Mkuu mbona ni kama unatabiri kifo cha Mbuyu Twite!!!!!??????
Acheni kupiga mayowe,yapo mambo matatu ambayo yamemfanya beki Mbuyu Twite wa APR ya Rwanda, aachane na Simba SC na kuamua kujiunga na YANGA.

Mambo hayo ambayo kwa mjumuisho unaweza kuyaita ‘Ujanja ujanja wa mjini' wa viongozi wa klabu hiyo ndio leo, yanaiponza klabu hiyo kumpoteza aina ya mchezaji ambaye walimuhitaji sana kwenye kikosi chao ili kujiimarisha.

Mosi; Namna ambavyo ‘walimuenzi' kiungo Patrick Mutesa Mafisango (sasa marehemu), pili; desturi ya kuwaacha wachezaji wa kigeni baada ya kuwasajili, hata kabla hawajaitumikia timu mfano Lino Masombo, Derrick Walullya na wengineo na tatu hadhi ya klabu yao kwa sasa ukilinganisha Yanga na Azam FC.
Habari za kiuchunguzi zinasema kwamba Mbuyu alilishwa ‘sumu' za kutosha ili aichukie Simba, kwanza klabu hiyo ilivyoutelekeza mwili wa marehemu Mafisango baada ya kifo chake, ambao hakuna kiongozi mkuu wa klabu hjiyo hata mmoja aliyekwenda kumzika DRC, zaidi ya Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji na mchezaji mmoja.
Pamoja na namna ambavyo Simba hawakujali kabisa mambo mengine muhimu kuhusu marehemu Mafisango, kama arobaini yake na kadhalika, Wakongo wameichukulia hiyo kama ni dharaua na ulipotokea mjadala Mbuyu aende wapi, watu wa Kongo wakamnyooshea kidole kinachoelekeza Jangwani.
Ikumbukwe, Mafisango aliyejiunga na Simba akitokea Azam FC, iliyomsajili kutoka APR ya Rwanda, alifariki akiwa mchezaji muhimu ndani ya Simba akiongoza kwa kufunga mabao na mwenye mchango mkubwa kwenye timu.
Simba, hivi karibuni ilimsajili mchezaji Lino Masombo kutoka DRC, lakini baada ya mwezi mmoja na ushei ikamtema kama ilivyofanya kwa Mganda, Derrick Walullya msimu uliopita, hilo limetajwa kumsitisha Mbuyu kuangukia Msimbazi na kuamua kurudisha fedha zote alizochukua kwa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage (dola za kimarekani 30,000 kwa mujibu wa Simba).
Lakini pia, wakati Mbuyu anasaini Simba kuchukua fedha, alikuwa hajui kwamba katika soka ya Tanzania hivi sasa, klabu ambazo zinachuana kwa ‘utajiri' ni Yanga, ambao Mwenyekiti wao Yussuf Manji ni mfanyaiashara mkubwa na Azam FC ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara mwingine, Said Salim Bakhresa.

Back
Top Bottom