Silvester Kasulumbayi, mbunge Maswa Mashariki ni mzigo

GREATTHINKERDAIMA

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
232
46
Mbunge wa Maswa Mashariki Sylvester Kasulumbayi (CHADEMA) kwa kipindi cha miaka mitano ameonekana kuwa mzigo ni afadhali hata ya John Magele Shibuda.

Mosi, uchangiaji wa hoja Bungeni ni sifuri kabisa. Tofauti na wabunge wengine wa CHADEMA tunaona wako mstari wa mbele kutetea hoja zenye maslahi ya nchi lakini jamaa huyu yeye zake bungeni ni kukaa kimya tu.

Pili, tangu amechaguliwa mbunge kuna baadhi ya kata hajawahi kufika na kujua shida za watu wake.

Tatu, hajaonekana katika kazi ya kujenga chama yaanu CHADEMA kama wabunge wengine wanavyofanya.

Je, CHADEMA tunamrudisha tena huyu kugombea ubunge? Hakuna mbadala unaoweza kutetea jimbo hilo libaki maana kwa namna niwajuavyo wasukuma hawatampigia kura tena huyo na hivyo kuipa nafasi CCM kunyakua jimbo la Maswa Mashariki.

CHADEMA maeneo haya inakubalika sana ila mgombea huyu nadhani atatuangusha vibaya.
 
Sio Kweli kuwa mbunge Kasulumbayi ni mzigo kwa sababu yupo pamoja na wapiga kura wake na ana makazi ya kudumu hapa Maswa.Ana chapa sana kazi jimboni kwake na mara nyingi hua anaitisha vikao na mikutano mbali mbali kusikiliza kero za wananchi wake.Mimi ni mkazi wa Maswa na haya niliyoyaandika nina uhakika nayo.
 
Its better to remain silent and let people think you are a stpid than to open your mouth and confirm to everyone that you are one
 
na hapiti CHADEMA wakibugi kumpitisha imekula kwao wotee..CCM watashangilia ushindi wa kishindo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom