Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 353
'Would you like to test for HIV too?, we recommend it to people who have lived in Africa and Asia' Aliniuliza Daktari huku akinitazama usoni, nikajikuta nimeropokwa...'Yeah, I wont mind!'. Japokuwa nilikuwa nimeenda hospitali kwa matatizo mengine, nilijikuta nimefanya uamuzi mkubwa sana kiafya kwa mara ya kwanza katika maisha yangu na to be honest- I suffered for a good one week hadi nilipopata matokeo yangu.
Nilitamani sana majibu yangekuwa yanatoka papo kwa papo lakini niliambiwa ingebidi nisubiri kwa wiki nzima. Nikaanza kukumbuka vimeo vyoooote nilivyowahi kuvipitia, usiku nilikuwa silali bila kupiga mbili tatu ili nipate usingizi, nikaona haitoshi nikanunua kadi ya simu nikaanza kuwapigia washkaji bongo. 'I see hivi yule demu wangu flani wa zamani yuko wapi siku hizi' ndo lilikuwa swali kuu. Mara nyongo ikantumbukia katika ulizia ulizia yangu, moja ya mademu niliopitia nikaskia kavuta, moyo ukaanza kwenda mbio, nikamuuliza mshkaji ' Nini kilimsibu jamani?', akajibu 'Alifariki kwenye ajali ya gari'....nikashusha pumzi mhhhh....huku moyoni nikijisemea 'aah...hiyo poa!!'
Katika wazawaza yangu nikaanza kuwakumbuka ndugu zangu wote ambao ukimwi umewachukua. Mwaka 94 bado nakumbuka, Binamu yangu ndo kwanza kazi alikuwa kaipata TRA wakamuweka kwenye Road tolls, hela akazikamata kwa sana na mabinti nao wakaongezeka, hakutaka kusubiri watu wambadilishe nepi na kuuguza madonda- alijiua punde tu baada ya kugundua kuwa ana ngoma.
Mtoto wa mama mkubwa, mi nilikua namuita dada, sura na maumbile alikuwa kajaliwa. Ndoa yake ilipovunjika, akaanza kufanya biashara za kusafiri, mara leo Tanga kesho Boarder Taveta. Naskia alikuwa hana hiyana katika safari zake, I guess alikuwa concerned zaidi na 'cost cutting and profit maximisation' kuliko uhai wake, akiwa safarini akipata atakayemnunulia chakula na kumpa malazi- twende kazini! Akapata bwana ambaye naye alikuwa ni mfanyabiashara wa kusafiri, walikuwa wanaonana mara mojamoja kwa kuwa wote walikuwa ni watu wa kusafiri, akaamua kumzalia!Mara ya mwisho nilipomuona 2006 machozi yalinitiririka, siku sio nyingi baada ya kuondoka Bongo nikaskia wamemzika, mtoto aliyeachwa ana kila dalili za uathirika.
Binamu yangu huyu, nilimpenda sana, alikuwa ni mrembo haswa lakini nahisi alifika mahali akawa desperate kuingia kwenye relationship. Sijui hata alikutania wapi na huyu mwanajeshi!! jamaa akamuoa na chapchap akampiga mimba- baada tu ya kuzaa, binamu afya yake ikadhoofika na mauti yakamchukua. She was so innocent, huyu mjeshi alikuwa akienda kwenye kituo chake cha kazi anakaa huko for 3-6 months ndo anarudi kumuona mkewe na hadi leo sijui ni kwanini alikuwa haendi naye.
Kwakweli nilipata nafasi ya kuwaza mengi, nikawakumbuka pia marafiki zangu ambao wametangua mbele ya haki kwa sababu zinazohisiwa kuwa ni UKIMWI, siwezi kuwapa story zao hapa kwa kuwa am not sure na watu hawasemi hadi leo hii kama ndugu zao wakifa kwa UKIMWI, utaskia 'shinikizo la damu' au 'marehemu amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu'!
Majibu niliambiwa nigeyapata kwa text jumanne iliyopita kati ya saa 3 asubuhi na 11 jioni, basi siku hiyo hadi napata majibu yangu kila text iliyokuwa ikiingia ilikuwa kama hivi mtu kanichoma kisu! Mapigo ya moyo yananiongezeka huku nikitetemeka. Mishale ya saa nane nikakiona kitu kimeingia toka namba ya kiofisi, kufungua 'All results negative'!
Nice weekend, kama unaweza kapime kama mimi japokuwa sishauri kama una moyo mwepesi, its always good to know your status!
Kana-Ka-Nsungu.