Siku ya tano leo wife kaninunia kisa nilimchana ukweli kuwa hajapendeza

Habari za leo watanganyika wenzangu?

Jumamosi iliyopita tulikuwa na mwaliko wa harusi,sasa basi my wife akaniambia nikimaliza mizunguko yangu nimpitie ofisini kwake ili twende wote home tukajiandae, well me kwenye saa 10 hivi jioni nikawa nimemaliza mizunguko yangu, nikasema ngoja nimpitie wife kama tulivyokubaliana nilivyofika akaniambia nimdrop kwanza saloon akafanye make up akaniambia hapo saloon angetumia dakika 10 tu, so me nikampeleka hapo saloon then nikawa niko kwenye gari namsubiri,matokeo yake akatumia zaidi ya lisaa limoja humo ndani, ofcoz me niliudhika sana coz alijua leo tutatoka kwa nini hayo mambo ya saloon hakuyafanya mapema?

Alivyomaliza mambo yake akaja kwenye gari me nikaamua kumuudhi makusudi tu, nikamwambia hiyo make up aliyofanya haijampendeza kabisa, bora awe anabaki na sura yake ya kawaida tu.alikasirika sana baada ya kumuambia hivyo,akaniuliza kama mimi sitomsifia nani mwingine wa kumsifia aliongea mengi sana me nikampuuza tu so tangu Jumamosi Hadi leo kaninunia,hanisemeshi chochote.

Kuna haja ya kumuomba msamaha au nami niendelee kukaza buti wakuu?
"Mwamme ishi na mkeo kwa akili na mwanamke mpende mmeo" - Vitabu vya dini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom