Siku ya Mwezi Duniani Julai 20

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Siku kama ya leo 1969 Wanaanga wa Marekani Neil Amstrong na Buzz Aldrin walifanikiwa kutua Mwezini mara baada ya safari ya siku takribani 3 tangu kutokea duniani ambapo walihudumu kwenye misheni ya Apollo 11

Safari ilikuwa ya maswahibi mbalimbali kwa wanaanga hao huku wakiwa na hofu kutokana na makosa ambayo wangeyasababisha yangskuja kuwagharimu pengine misheni nzima kuharibika au kupoteza maisha kabisa

Mara baada ya kutua mwezini wanaanga hao walitumia muda wa masaa 6 mwezini hapo na baadae kuanza safari ya kurudi duniani ambapo walifanikiwa kufika duniani baada ya siku mbili baadae

Safari nzima ilijumuisha wanaanga watatu ambapo wawili walitua mwezini na mmoja ambaye ni Michael Collins yeye alibaki kuzunguka mwezi na chombo cha Columbia command module kwa maana bila ya kuwepo kwa chombo hicho basi wanaanga Neil Amstrong na Buzz Aldrin wasingeweza kurudi nyumbani kabisa .

Tangu kwa safari ya kwanza mwaka 1969 hadi 1972 Marekani walifanikiwa kupeleka wanaanga 12 mwezini katika misheni kadhaa ambazo ni Apollo 11,12,14,15,16,17 .

Pichani ni mwanaanga Neil Amstrong akiwa amesimama pembezoni mwa bendera ya Marekani mara baada ya kumaliza kuichomeka kwenye uso wa Mwezini

Siku ya leo imeitwa siku ya mwezi duniani ili kuenzi siku pekee ambayo mwanadamu aliweza kukanyaga uso wa gimba lengine tofauti kabisa na dunia yetu .

AstronomyKiswahili
 
Back
Top Bottom