Siku ya Kiswahili Duniani: Wamarekani na Kiswahili

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
SIKU YA KISWAHILI DUNIANI: WAMAREKANI NA KISWAHILI

Nimefika Marekani kwa mwaliko wa Chuo Kikuu Cha Iowa, Iowa City mwaka wa 2011 aliyenialika ni Prof. James Giblin Mkuu wa Idara ya Historia ya Afrika hapo chuoni.

Visa ya Marekani ina tabu kidogo na nilipofika Consulate ya Marekani kuomba visa ikawa nimeonekana na dosari kwa kuwa nilikuwa nimefika Iran na Nigeria.

Jibu nililolopewa ni kuwa nahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Nikaondoka kurejea Tanga nilikotokea.

Baada ya siku chache nikapigiwa simu na Prof. James Giblin akiniuliza kwa Kiswahili kilichonyooka kama nimeshapata visa ya kuingia Marekani.

Nikamjibu kuwa bado.

Nikawa nimeshangazwa na ulimi wake katika kukizungumza Kiswahili.

Prof. Giblin si kuwa anasema Kiswahili vizuri na kwa fasaha lakini ameingia ndani ya utamaduni wa Waswahili kiasi anafanya makhara ambayo ukimsikia utajiuliza huyu Mmarekani kajuaje haya ya Kariakoo na Manzese?

Baada ya muda kidogo akanipigia simu kuniambia kuwa yuko Dar es Salaam na jana yake alikwenda Consulate kuuliza kuhusu visa yangu.

''Hawa Wamarekani sijui wana nini nawauliza visa yako wananijibu kwa mkato kuwa wao hawawezi kuzungumza na mimi kuhusu visa yako lakini wamenipa namba ya simu wameniambia nikupe uwapigie.''

Nilipopiga namba ile kwa mastaajabu yangu makubwa jibu nililopewa ni kuwa visa yangu iko tayari niende nikachukue.

Lakini Prof. Giblin hakuwa Mmarekani wa kwanza niliyefahamiananae ambae alikuwa Mswahili.

Katika miaka ya mwishoni 1980 nilifahamiana na Mmarekani Mweusi jina lake John Innis mwenyewe akipenda kujiita, ''John Mtembezi.''

John Innis yeye alikuwa mwalimu wa Kiswahili Marekani na akikijua Kiswahili vizuri mno kiasi mimi tukizungumza alikuwa akinishangaza jinsi alivyokuwa anajua misemo na misamiati ya Kiswahili.

Siku moja tunamzungumza Prof. Tigiti Sengo aliyekuwa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

John Innis akaniambia, ''Mimi namheshimu Dr. Sengo kwani ni nyakanga wangu.''

Siku nyingine katika mazungumzo akaniambia, ''Sikiliza ndugu yangu huwezi wewe kucheza ngoma na mzigo kichwani.''

Lakini katika Wamarekani waliofurtu ada katika Kiswahili na Uswahili nadhani hakuna wa kumshinda Prof. Kelly Askew wa Chuo Kikuu Cha Michigan.

Kelly yeye akiwa katika utafiti Tanga alifika na kuwa mwimbaji wa taarab wa sifa hapo mjini.

Ushapata kumuona au kumsikia Mzungu anaimba taarab?

Kelly baada ya utafiti wake kukamilika na kurejea kwao akaja kuandika kitabu kizuri sana kuhusu taarab, ''Performing The Nation,'' (2002).

Katika miaka ya mwanzoni 2000 nikiwa Tanga nilijiwa na kijana jina lake James Brennan mwanafunzi wa Ph D kaagizwa kwangu na mwalimu wake Jonathon Glassman.

James Brennan tunafahamiana toka miaka ya mwanzoni 2000 anazugumza Kiswahili vizuri na kilichonistaajabisha ni kule kuniambia kuwa yeye kajifunza Kiswahili Marekani.

Jim kama ninavyopenda kumwita leo ni rafiki yangu ndugu.

James Brennan kaandika sana kuhusu Tanzania na ana mapenzi makubwa na nchi yetu.

Hapungui Dar es Salaam na ni mpenzi na mlaji mzuri wa biriani na mishkaki ya mitaani.

Vipi mtu atakuwa Mswahili asipende vitu hivi?

Nimefika Chuo Kikuu Cha Iowa mwenyeji wangu ananitembeza na kunijulisha kwa watu.

Nashangazwa na Wamarekani wanaosema Kiswahili.

Nimeingia maktaba nakuta vitabu tele vya Kiswahili hadi CD za Bi. Kidude.

''Sisi hatuagizi mtu kutununulia CD za Bi. Kidude tunakuja wenyewe Kariakoo kununua upo hapo Mzee wa Tanga?

Namtazama Prof. Giblin naishia kucheka.

Najisema moyoni, ''Hawa Wamarekani wanga hawa vipi utaichimba na kuipenda lugha na utamaduni ambao si wako kwa kiasi hiki kisha ukajinasibu kwa mwenye lugha yake?''

Wamarekani wanaona sifa kuwa wanakijua Kiswahili na wanakisema kwa ufasaha.

''Sisi tunakuja Tanzania si kujifunza Kiswahili, sisi tunatoka huku lugha tunaijua tunakuja Dar es Salaam kukipamba Kiswahili chetu kipendeze.''

Huwezi kushindana na wanga kwani wanga wanakujia nyumbani kwako usiku umelala kuja kukuwangia.

''Nyinyi Waamerika wachawi.''
Sote tunacheka kwani hawa watu wanaujua utamaduni wetu.

Wanacheka kwa kuwa wanashindwa kupata picha ya mwanga wa Kimarekani.

Wamarekani ni taifa kubwa la watu wajanja na wajuzi wa kila fani.
Wanajua njia nyepesi ya kumpata mtu ni kuisema lugha yake.

Nikiwa Chuo Kikuu Cha Iowa Jonathan Glassman akanialika kuzungumza Northwestern University, Chicago.

Nikaenda nimefatana na rafiki yangu James Brennan.

Kanichukua na gari yake tunakwenda Chicago na njia nzima tunazungumza Kiswahili.

Njiani tunasimama kuingia katika mgahawa ndugu zake wanamshangaa kumsikia akizungumza na mimi lugha wasiyoijua.

Niko Ukumbi wa Eduardo Mondlane Northwestern University nasubiri kuzungumza.

Nilikuwa nimejawa na hofu.
Napepesa macho kila upande wa ukumbi.

Ukumbi umepambwa kwa vinyago vya Kimakonde kutoka Msumbiji.

Ukumbi huu umepewa jina la Mondlane kwa kuwa yeye alisoma chuo hicho.

Nimejawa na hofu kwa sababu mwaliko huu wa kuja Northwestern University kuzungumza naamini ulitokana na ubishani uliozuka mwisho wa mada yangu pale Iowa katika kipindi cha maswali na majibu.

Alisimama profesa mmoja wa historia ya Afrika na kusema kuwa Tanzania Waislam ni wachache Wakristo ndiyo wengi.

Jibu nililotoa lilimaliza ubishi na ukumbi ukapwelewa.
Wamarekani hawapendi kushindwa.

Jibu nililowapa liliwatosha.

Hapo ndipo nilipopewa mwaliko na Jonathon Glassman wa kuja kuzungumza chuoni kwake Northwestern University.

Lakini uko uwezekano kuwa zilikuwapo sababu nyingine za mwaliko ule.

Northwestern University ipo Evanston nje kidogo ya Chicago.

Hapo Evaston nikakutana na Mswahili Mmarekani jina lake Nathaniel Mathews.

Huyu ndiye alikuwa mwenyeji wangu na alinipigia simu hotelini anazungumza na mimi Kiswahili.

Anakimwaga Kiswahili kama maji na ananiambia kuwa yeye Kiswahili kasoma Marekani.

Nathaniel ndiye aliyekuja kunichukua hotelini kunipeleka ukumbini.

Ukumbi haukuwa mbali tunatembea njia nzima tunazungumza Kiswahili.

Nikiwa nimekaa pale mbele Ukumbi wa Eduardo Mondlane moyo ukinidunda nikaona labda naweze kujituliza kwa kuiambia kitu ile hadhira yangu.

''Why put me up at the Hilton?''
Hadhira yangu ikacheka.

Nilikuwa kama vile nawalaumu kwa kuniweka katika hoteli kubwa ya kifahari.

Nyuma ya ukumbi ikatoka sauti kwa Kiswahili cha Kariakoo, ''Sikiliza Bwana Mohamed wewe mtu mkubwa sasa unadhania sisi mtu kama wewe tutamweka wapi?''

Hakika nilipigwa na butwaa.

Nimeshangazwa na lile jibu lililoletwa kwangu kwa maskhara yale yale niliyopeleka lakini kuna kitu kikawa kimeongezeka.

Huyu Mmarekani ananijibu mimi kwa mtindo wa watoto wa mjini ambao sikutegemea kuusikia Chicago.

Nashangaa leo kuna Waswahili akizungumza sharti atie na maneno ya Kiingereza.

Watu kama hawa wanatafuta nini?

PICHA: Prof. James Giblin, James Brennan, Kelly Askew na Nathaniel Mathews.
 
Tupe thread ya wa-iran na kiswahili
Mpaji...
Mwaka wa 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza baada ya kureshwa vyama vingi Abdul Fatah Mussa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio Iran, Tehran alikuwa akinifanyia mahojiano mara kwa mara.

Ikatokea mahojiano yetu kupendwa sana kwa wasikilizaji waliokuwa Falme za Kiarabu na kwengineko.

Halikadhalika nikapata umaarufu ndani ya nchi hizo kwani Kiswahili kinasemwa sana nchi hizo pamoja na Muscat.

Kwa ajili hii Idhaa yao ya Kiswahili ikapata wasikilizaji wengi.
Kwa kuonyesha shukurani yao kwangu nikaalikwa Iran mwaka wa 2007.

Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje walifika Uwanja wa Ndege kunipokea na walinipitisha VIP.

Kama hii haikutosha gari niliyopanda kwenda hoteli ilitanguliwa Mercedes Benz iliyokuwa imewashwa kimulimuli.

Hii ilikuwa mara yangu ya pili kupokelewa kama hivi.
Mara ya kwanza ilikuwa Khartoum, Sudan mwaka wa 1989.

Nilipokuwa Tehran niliingia studio na kurekodi vipindi kadhaa kuhusu Tanzania.
Angalia picha hiyo hapo chini nikiwa studio na Abdul Fatah Musa.

1688731613992.jpeg
 
Kumbukumbu nzuri sana, Kelly askew nakumbuka kumuona kwenye matangazo ya kukundi chake kwenye magazeti ya uhuru na mzalendo, enzi hizo tunashangaa mzungu anaimba taarab, kumbe mtu anautafuta uprofesa.
Lhuga ya kiswahili haina mwenyewe, inaunganisha watu wa mataifa mbalimbali, tunapaswa kuienzi na kuieneza ifundishwe nchi zote
 
SIKU YA KISWAHILI DUNIANI: WAMAREKANI NA KISWAHILI

Nimefika Marekani kwa mwaliko wa Chuo Kikuu Cha Iowa, Iowa City mwaka wa 2011 aliyenialika ni Prof. James Giblin Mkuu wa Idara ya Historia ya Afrika hapo chuoni.

Visa ya Marekani ina tabu kidogo na nilipofika Consulate ya Marekani kuomba visa ikawa nimeonekana na dosari kwa kuwa nilikuwa nimefika Iran na Nigeria.

Jibu nililolopewa ni kuwa nahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Nikaondoka kurejea Tanga nilikotokea.

Baada ya siku chache nikapigiwa simu na Prof. James Giblin akiniuliza kwa Kiswahili kilichonyooka kama nimeshapata visa ya kuingia Marekani.

Nikamjibu kuwa bado.

Nikawa nimeshangazwa na ulimi wake katika kukizungumza Kiswahili.

Prof. Giblin si kuwa anasema Kiswahili vizuri na kwa fasaha lakini ameingia ndani ya utamaduni wa Waswahili kiasi anafanya makhara ambayo ukimsikia utajiuliza huyu Mmarekani kajuaje haya ya Kariakoo na Manzese?

Baada ya muda kidogo akanipigia simu kuniambia kuwa yuko Dar es Salaam na jana yake alikwenda Consulate kuuliza kuhusu visa yangu.

''Hawa Wamarekani sijui wana nini nawauliza visa yako wananijibu kwa mkato kuwa wao hawawezi kuzungumza na mimi kuhusu visa yako lakini wamenipa namba ya simu wameniambia nikupe uwapigie.''

Nilipopiga namba ile kwa mastaajabu yangu makubwa jibu nililopewa ni kuwa visa yangu iko tayari niende nikachukue.

Lakini Prof. Giblin hakuwa Mmarekani wa kwanza niliyefahamiananae ambae alikuwa Mswahili.

Katika miaka ya mwishoni 1980 nilifahamiana na Mmarekani Mweusi jina lake John Innis mwenyewe akipenda kujiita, ''John Mtembezi.''

John Innis yeye alikuwa mwalimu wa Kiswahili Marekani na akikijua Kiswahili vizuri mno kiasi mimi tukizungumza alikuwa akinishangaza jinsi alivyokuwa anajua misemo na misamiati ya Kiswahili.

Siku moja tunamzungumza Prof. Tigiti Sengo aliyekuwa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

John Innis akaniambia, ''Mimi namheshimu Dr. Sengo kwani ni nyakanga wangu.''

Siku nyingine katika mazungumzo akaniambia, ''Sikiliza ndugu yangu huwezi wewe kucheza ngoma na mzigo kichwani.''

Lakini katika Wamarekani waliofurtu ada katika Kiswahili na Uswahili nadhani hakuna wa kumshinda Prof. Kelly Askew wa Chuo Kikuu Cha Michigan.

Kelly yeye akiwa katika utafiti Tanga alifika na kuwa mwimbaji wa taarab wa sifa hapo mjini.

Ushapata kumuona au kumsikia Mzungu anaimba taarab?

Kelly baada ya utafiti wake kukamilika na kurejea kwao akaja kuandika kitabu kizuri sana kuhusu taarab, ''Performing The Nation,'' (2002).

Katika miaka ya mwanzoni 2000 nikiwa Tanga nilijiwa na kijana jina lake James Brennan mwanafunzi wa Ph D kaagizwa kwangu na mwalimu wake Jonathon Glassman.

James Brennan tunafahamiana toka miaka ya mwanzoni 2000 anazugumza Kiswahili vizuri na kilichonistaajabisha ni kule kuniambia kuwa yeye kajifunza Kiswahili Marekani.

Jim kama ninavyopenda kumwita leo ni rafiki yangu ndugu.

James Brennan kaandika sana kuhusu Tanzania na ana mapenzi makubwa na nchi yetu.

Hapungui Dar es Salaam na ni mpenzi na mlaji mzuri wa biriani na mishkaki ya mitaani.

Vipi mtu atakuwa Mswahili asipende vitu hivi?

Nimefika Chuo Kikuu Cha Iowa mwenyeji wangu ananitembeza na kunijulisha kwa watu.

Nashangazwa na Wamarekani wanaosema Kiswahili.

Nimeingia maktaba nakuta vitabu tele vya Kiswahili hadi CD za Bi. Kidude.

''Sisi hatuagizi mtu kutununulia CD za Bi. Kidude tunakuja wenyewe Kariakoo kununua upo hapo Mzee wa Tanga?

Namtazama Prof. Giblin naishia kucheka.

Najisema moyoni, ''Hawa Wamarekani wanga hawa vipi utaichimba na kuipenda lugha na utamaduni ambao si wako kwa kiasi hiki kisha ukajinasibu kwa mwenye lugha yake?''

Wamarekani wanaona sifa kuwa wanakijua Kiswahili na wanakisema kwa ufasaha.

''Sisi tunakuja Tanzania si kujifunza Kiswahili, sisi tunatoka huku lugha tunaijua tunakuja Dar es Salaam kukipamba Kiswahili chetu kipendeze.''

Huwezi kushindana na wanga kwani wanga wanakujia nyumbani kwako usiku umelala kuja kukuwangia.

''Nyinyi Waamerika wachawi.''
Sote tunacheka kwani hawa watu wanaujua utamaduni wetu.

Wanacheka kwa kuwa wanashindwa kupata picha ya mwanga wa Kimarekani.

Wamarekani ni taifa kubwa la watu wajanja na wajuzi wa kila fani.
Wanajua njia nyepesi ya kumpata mtu ni kuisema lugha yake.

Nikiwa Chuo Kikuu Cha Iowa Jonathan Glassman akanialika kuzungumza Northwestern University, Chicago.

Nikaenda nimefatana na rafiki yangu James Brennan.

Kanichukua na gari yake tunakwenda Chicago na njia nzima tunazungumza Kiswahili.

Njiani tunasimama kuingia katika mgahawa ndugu zake wanamshangaa kumsikia akizungumza na mimi lugha wasiyoijua.

Niko Ukumbi wa Eduardo Mondlane Northwestern University nasubiri kuzungumza.

Nilikuwa nimejawa na hofu.
Napepesa macho kila upande wa ukumbi.

Ukumbi umepambwa kwa vinyago vya Kimakonde kutoka Msumbiji.

Ukumbi huu umepewa jina la Mondlane kwa kuwa yeye alisoma chuo hicho.

Nimejawa na hofu kwa sababu mwaliko huu wa kuja Northwestern University kuzungumza naamini ulitokana na ubishani uliozuka mwisho wa mada yangu pale Iowa katika kipindi cha maswali na majibu.

Alisimama profesa mmoja wa historia ya Afrika na kusema kuwa Tanzania Waislam ni wachache Wakristo ndiyo wengi.

Jibu nililotoa lilimaliza ubishi na ukumbi ukapwelewa.
Wamarekani hawapendi kushindwa.

Jibu nililowapa liliwatosha.

Hapo ndipo nilipopewa mwaliko na Jonathon Glassman wa kuja kuzungumza chuoni kwake Northwestern University.

Lakini uko uwezekano kuwa zilikuwapo sababu nyingine za mwaliko ule.

Northwestern University ipo Evanston nje kidogo ya Chicago.

Hapo Evaston nikakutana na Mswahili Mmarekani jina lake Nathaniel Mathews.

Huyu ndiye alikuwa mwenyeji wangu na alinipigia simu hotelini anazungumza na mimi Kiswahili.

Anakimwaga Kiswahili kama maji na ananiambia kuwa yeye Kiswahili kasoma Marekani.

Nathaniel ndiye aliyekuja kunichukua hotelini kunipeleka ukumbini.

Ukumbi haukuwa mbali tunatembea njia nzima tunazungumza Kiswahili.

Nikiwa nimekaa pale mbele Ukumbi wa Eduardo Mondlane moyo ukinidunda nikaona labda naweze kujituliza kwa kuiambia kitu ile hadhira yangu.

''Why put me up at the Hilton?''
Hadhira yangu ikacheka.

Nilikuwa kama vile nawalaumu kwa kuniweka katika hoteli kubwa ya kifahari.

Nyuma ya ukumbi ikatoka sauti kwa Kiswahili cha Kariakoo, ''Sikiliza Bwana Mohamed wewe mtu mkubwa sasa unadhania sisi mtu kama wewe tutamweka wapi?''

Hakika nilipigwa na butwaa.

Nimeshangazwa na lile jibu lililoletwa kwangu kwa maskhara yale yale niliyopeleka lakini kuna kitu kikawa kimeongezeka.

Huyu Mmarekani ananijibu mimi kwa mtindo wa watoto wa mjini ambao sikutegemea kuusikia Chicago.

Nashangaa leo kuna Waswahili akizungumza sharti atie na maneno ya Kiingereza.

Watu kama hawa wanatafuta nini?

PICHA: Prof. James Giblin, James Brennan, Kelly Askew na Nathaniel Mathews.
Wewe mzee huwa ni hazina ya Taifa, basi tu unaruhusu udini wako kwenye kazi yako, ungeweza kutenganisha udini wako na kazi yako watu wangekuthamini zaidi. Nilikua Texas siku moja nikaulizwa na mtu mmoja kama nakufahamu, una jina kubwa nje lakini hapa nchini, hasa hasa madogo wa jf wanakuchukulia poa kupitiliza
 
Tes...
Ungenitambulisha kwa "Mzee Mohamed" badala ya "Wewe Mzee."

Nini kipimo chako cha "ukubwa" na "udogo" wa jina la Mohamed Said?
 
Hongera sana mzee wangu kwa bandiko mujarabu. Wewe ni hazina kubwa sana, huko duniani wewe ni maarufu kweli!!! Lakini hapa kwetu sasa!!!!!!Sijajua tatizo ni nini??? Kama mahaba ya dini kila mtu anayo!!!!!!!Au nabii hakubaliki kwao????

Kuna kitu kibaya ulikifanya dhidi ya mfumo (system)???? Mbona huko duniani unajulikana sana kuliko hata hawa wanasiasa wetu!!!!!!! Hapa wanaokufahamu ni wachache sana hasa wa kizazi chako ambacho kinaelekea kupotea!!!!!Au ni siri kubwa???

Samahani kwa kukukera!!!!!!!!!!!!

Nb: Kuna profesa (msimamizi wangu kwenye utafiti) kutoka Marekani alinieleza kuwa wewe ni mtu muhimu na una mchango mkubwa sana lakini mimi nilikuwa sikufahamu.Kwenye utafiti nikagundua kweli!!!!!!!!!!!!
 
Enzo....
Katika kitabu cha Mario Puzo "The Godfather" kuna mtu anaitwa, "Enzo."

Kila mtu hakika ana dini yake.

Tofauti katika historia ni wafuasi wa dini ipi na viongozi wao waliojitolea kupambana na ukoloni?
 
Wataalam wetu wa kiswahili ni maarufu zaidi nje kuliko ndani kwa sababu huku kila mtu anajua kiswahili, vivo hivyo kwa wataalam wa mila na historia zetu
 
Huu Mnara ulikuwa hapo Georgia kabla haujalipuliwa na gaidi la kizungu lenye ubaguzi halikupenda lugha ya kiafrika kutukuzwa hapo. Upande mmoja wa mnara ulikuwa umeandikwa kwa Kiswahili kama inavyoonekana.

1688817177734.png
 
Enzo....
Katika kitabu cha Mario Puzo "The Godfather" kuna mtu anaitwa, "Enzo."

Kila mtu hakika ana dini yake.

Tofauti katika historia ni wafuasi wa dini ipi na viongozi wao waliojitolea kupambana na ukoloni?
Hakuna shaka yoyote, wafuasi wa dini ya Kiislamu waliongoza mapambano ya kupigania uhuru kwa kiasi kikubwa kuliko wakristo (Mimi ni mkristo) hili lipo wazi na halijifichi. Vita kubwa dhidi ya mkoloni Ujerumani kwa kiasi kikubwa viliendeshwa na Waislamu.

Mkoloni hasa Mwingereza alitumia mbinu ya tuwagawe kisha tuwatawale, mfumo huu kwa kiasi fulani uliwabeba zaidi wakristo na kuwakandamiza waislamu ambao waliamua kupambana nao. Hili lipo wazi ukitumia ubongo wako vizuri na siyo mhemko,papara, chuki, hasira n.k.

Natumaini nimekujibu vyema!!!!!!!!!!

1: Hizi harakati za kudai uhuru zina athari kubwa kwako mpaka kusahulishwa kimakusudi hapa nchini????

2: Wewe na Ahmed Rajab mnajulikana sana huko duniani na mnapewa sifa na heshima lukuki, mbona hapa ni kinyume chake????
 
Back
Top Bottom