Siku nilipokutana na Salim Himidi Tanga

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,271
SIKU NILIPOKUTANA NA SALIM HIMIDI

Hii makala ni taazia niliyomwandikia rafiki na ndugu yangu Salim Himidi alipofariki Paris.
Mtu aliyenijulisha kwa Salim Himidi ni Mohamed Mshangama.

Nimeipata picha ya siku hii Maktaba na ni zaidi ya miaka 25 sasa imepita.
Nimeona niweke taazia ya rafiki yangu hapa na hii picha tuliyopiga sisi watatu Panori Hotel Tanga.

Nimeona pia niweke hapa picha ya kitabu nilichoandika cha maisha ya Sal Davis.

Watu hawa wawili waliojuana ujanani Zanzibar kisha kupoteana kwa takriban nusu karne nilijaaliwa kuwakutanisha Dar es Salaam siku moja.

SALIM HIMIDI (1945 – 2020)
JAHAZI LILILOZAMA NA SHEHENA YAKE YOTE YA VITO VYA THAMANI KUBWA

Nimemfahamu Salim Himidi kiasi cha miaka 20 iliyopita kupitia kwa rafiki na ndugu yangu Mohamed Mshangama.

Wakati huo nilikuwa nikiisha Tanga.
Mshangama na Salim walisoma darasa moja King George VI Zanzibar katika miaka ya 1950.

Kuna kauli hupenda kuitumia lakini huku nikichukua tahadhari kubwa kuchelea kueleweka vibaya.

Binafsi sikupata kuwajua Wazanzibari hadi nilipofika Uingereza na kukutana na Wazanzibari ambao wengi wao waliondoka Zanzibar kutafuta elimu na maisha ughaibuni baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Udogoni nimekuwa nikiwaona Wazanzibari rafiki ya baba yangu wakija nyumbani na nimekua nikiwaona na kuwajua Wazanzibari wengine wenye majina makubwa na nafasi katika serikali ya Tanzania nikiwa na akili zangu.

Wazanzibari hawa ni tofauti sana na Wazanzibari niliokuja kuwajua na kufahamiananao kwa karibu nikiwa nje ya Tanzania.

Hawa hawakuwa watu wa kuvuma wengi hawakuwa wakijulikana lakini nilivutiwa na uwezo wa akili zao.

Kutoka kwao nilipigwa usoni na dharuba iliyonishtusha sana ya uwezo wao mfano wa mtu ambae maisha yake yote maji aliyoyaona ni ya kijito kidogo kijijini alikozaliwa kisha ghafla anaiona bahari kwa mara ya kwanza.

Nakumbuka kama jana vile usiku mmoja nilipomwalika Salim Himidi na mwenyeji wake Mshangama Panori kwa chakula cha jioni ili nami nipate fursa ya kumkirimu mgeni na kuzungumzanae.

Hii Panori ni hoteli iliyokuwa ikisifika sana mjini kwa chakula chake hasa, ‘’Sea Food,’’ na haitokushangaza kwa mahali hapa kuwa hivyo kwani mwenyewe alikuwa mzee wa Kishelisheli.

Sikuwa namjua Salim vyema kabla ya siku hii tumekaa tunaangaliana.

Yeye kumbe kwa kiasi fulani alikuwa kasoma makala zangu zilizokuwa zikichapwa na jarida Africa Events kwa hiyo akinifahamu kwa kiasi.

Mazungumzo yakaanza mithali ya wanamasumbwi wawili katika duru yao ya kwanza.

Salim hakuwa mtu wa kawaida aliweza katika muda mfupi katika mazungumzo akakutolea mifano ya matukio ya sasa kutoka vyanzo vingi akamwingia William Shakespeare, ‘’Richard the Third,’’ na kibyongo chake aliyeua kwa kutafuta ufalme, akakupeleka hadi kwa roho mbaya Stalin na uovu wake usio mithilika.

Hapo inawezekana mnazungumza historia ya Zanzibar mbako yeye alipata elimu yake ya awali.

Hapa Salim atakuwa anafanya uchambuzi wa historia ya Zanzibar akikufananishia na yale yote yaliyotokea baada ya mapinduzi kwa kuwachambua viongozi wake.

Kwangu mimi hapo hapo nikatambua kuwa mbele yangu nina mtu aliyeelimika sawasawa na mwenye kuijua historia ya dunia.

Salim juu ya kukutwisha mzigo mzito kama huu hapo hapo kama vile mtu aliyetambua kuwa umeelemewa atamzungumza James Dean na senema chache alizocheza kabla ya kufariki kwa ajli ya gari akiwa kijana mbichi.

Bila shaka Salim alikuwa anatambua kuwa kuna historia kila zinapozungumzwa hukumbusha machungu na si kwa mzungumzaji peke yake bali hata kwa yule anaesikiliza.

Nilikuwa nastarehe nikimsikiliza Salim pale anapochambua siasa za Zanzibar na viongozi wake kisha mmojawapo akampa nembo akamwita, ‘’Stanilist.’’

Lakini haya ya ‘’Stanilist,’’ ndani ya Zanzibar tuliyazungumza miaka mingi baadae nilipokwenda Paris na nikawa na fursa kubwa ya kukaanae na kumsikiliza.

Nababaika sijui nianze wapi nimalizie wapi.

Leo nikiangalia nyuma na kurejesha mazungumzo mengi niliyopata kuzungumza na Salim tukiwa Tanga, Dar es Salaam kila alipokuja na nilipomtembelea Paris najiuliza kwa nini alikuwa kama vile anasoma kutoka kwenye kitabu cha misiba na majonzi ya maisha akianza na mapinduzi ya Zanzibar, Comoro na akimtaja Richard the Third na Stalin ambazo zote ni historia zilizopambika kwa damu.

Salim niliyekuwanae Tanga na Dar es Salaam ni tofauti na Salim niliyekuwanae Paris alikohamia.

Akiwa nyumbani Tanzania Salim nilikuwa namuona kwa jicho lingine akizungumza na kucheka kwa furaha ndugu zake.

Salim niliyemuona Paris nilimuona kwa jicho lingine.

Nilimuona Salim kama mfungwa ugenini, Salim Himidi mwanadiplomasia, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje aliyehama kwao kuja kuishi kwa wale wale ambae yeye akiwa kijana baada ya kurudi Comoro mwaka wa 1968 aliwaundia Wafaransa chama cha siasa cha kishoshalisti Socialist Party of Comoro (PASOCO) kiungane na Liberation Movement of Comoro (MOLINACO) kudai uhuru wa Comoro.

Mwaka huu wa 1968 mjini Paris kulikuwa na maandamano yasiyo na kikomo ya wanafunzi wakipinga serikali.

Moto uliokuwa unawaka katika kifua cha Salim wakati huu akiwa mwanafunzi ulizidi kukolezwa na yale yaliyokuwa yakitokea Paris.

Leo nikimkumbuka Salim kwa mazingira yale niliyomuona akiishi Paris sasa akiwa mtu mzima akielekea uzeeni haikunijia tabu kutambua kuwa alikuwa amegubikwa na wimbi zito la upweke na kukumbuka sana nyumbani Zanzibar na Comoro.

Salim alikuwa hapendi tule kwenye migahawa yenye vyakula vya Kizungu na siku zote akinipeleka migahawa ya Kihindi na kuna mgahawa mmoja akiupenda sana.

Mwenye mgahawa huu alikuwa Mzanzibari ambae baba yake alikimbilia Ufaransa baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1964 na baada ya baba yake kufariki mwanae akawa anauendesha.

Hapo tutaagiza chai, chapati, sambusa na kababu pamoja na chatney yake. Ukitukuta hapo tunakunywa chai na ukatupia jicho sahani zetu wala huwezi kujua kama tuko katikati ya jiji la Paris, utadhani labda tuko ‘’Passing Show,’’ Malindi, au mgahawa wowote Stone Town, Zanzibar.

Tutakunywa chai huku tukisikiliza muziki wa Kihindi wa Lata Mangeshkar, Asha Bhosle, Mohamed Rafi na Mukesh uliokuwa ukipigwa kwa sauti ya chini sana.

Nilijua Salim akiwa hapa alikuwa anarejea udogoni Zanzibar akiiwaza Zanzibar ambayo haitaweza kurudi tena.

Salim akinihadithia utoto wake nyumbani Zanzibar na vipi filamu za Kihindi na nyimbo zake zilivyokuwa zikisikilizwa kila nyumba na vipi wacheza senama wa Kihindi kama Raj Kapoor, Dev Anand, Dilip Kumar, Nargis, Madhubala walivyokuwa maarufu visiwani.

Salim ghafla atakutoa hapo na kukutia katika historia ya muziki wa jazz na blues kutoka New Orleans na New York.

In Shaa Allah nitarudi hapa kwenye sura nyingine ya Salim katika muziki wakati wa udogo wake.

Salim anapozungumza mapinduzi alikuwa anakizungumza kitu anachokifahamu kwani kazaliwa Zanzibar katika nchi iliyofanya mapinduzi na yeye akiwa kijana mdogo ameyashuhudia mapinduzi na akaishi ndani ya mapinduzi.

Alipomaliza masomo shule ya Kingi George VI Salim aliondoka Zanzibar na kwenda nchi ya asili yake Comoro na kutokea Comoro akaenda Ufaransa na Uingereza kuendelea na masomo ya juu.

Safari hii ambayo Salim aliifanya hadi Ulaya ‘’kwa miguu,’’ ni kisa tosha cha Steven Spielberg kutengeneza senema.

Salim aliwenda Ulaya kwa kuvuka mpaka mmoja hadi mwingine mpaka akafika Cairo.
Kutokea Cairo akavuka Bahari ya Mediterranean kuingia Ulaya.

Alipomaliza masomo yake Ufaransa Salim alirudi Comoro iliyokuwa katika harakati za kudai uhuru wake kutoka kwa Ufaransa.

Salim alikuwa anapo yazungumza mapinduzi hakuwa anayazungumza kama nadharia, alikuwa anayazungumza mapinduzi katika uhalisia wake kwa kuishi ndani yake kwanza Zanzibar kisha Comoro.

Salim alikuwa na fahari kujinasabisha na pande zote mbili. Mnapoandikiana baruapepe au yeye kuchangia kwenye mjadala mitandaoni, humalizia kwa maneno haya, "Wako Mzanzibari wa Comoro na Mcomoro wa Zanzibar.’’

Salim alikuwa akisema, ‘’Comoro nimezaliwa tu nimeondoka na wazee wangu kwenda Unguja, nina umri wa miezi 20, ni Zanzibar ilionilea hadi nikafika nilipo.’’

Picha za Salim Himidi akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Comoro zinatosha kueleza historia ya maisha yake lakini ukimsikiliza Salim mwenyewe anapozungumza na hazungumzii maisha yake bali siasa za Comoro, dunia na historia yake utatamani aandike kitabu ili ulimwengu unufaike na elimu ile.

Huu ndiyo ulikuwa ugomvi wangu na Salim kila tukikutana na mimi kumkumbusha kuhusu kuandika kumbukumbu zake.

Salim siku zote akinijibu kwa mkato, ‘’Sheikh Mohamed nitaandika ondoa huo wasiwasi wako.’’

Lakini nikiangalia ile ‘’body language,’’ napata ‘’signals,’’’ zinazoniambia kuwa Salim anaanua ngoma juani nami sijapenda jibu hilo nashikilia na sasa naingia katika kumbughudhi namshikilia, namng’ang’ania kuhusu kuandika maana inakuwa mara ya mwisho miaka kadhaa tumekutana na nimemuuliza kuhusu kumbukumbu zake na jibu si kuwa naandika niko sura kadhaa bali jibu siku zote ni lile lile, ‘’Nitaandika.’’

Ikawa sasa najua Salim haandiki na sababu yake sijui na haniambii.

Siku moja nikaamka nimeghadhibika nikaamua kuandika kitu kuhusu rafiki yangu Salim Himidi ingawa nilijua nitakayoandika ni sawa na tone la maji ndani bahari katika maisha yake lakini nilisema nikiandika hamaki zangu za kumkasirikia rafiki yangu zitapungua na yeye akisoma atasema, ‘’Unaona Mohamed keshanianzia vurugu zake za kumbukumbu zangu huyu mtu mshari sana.’’

Ikawa kama vile Allah kanifungulia mlango. Makala nikaipa kichwa cha habari, ‘’Down Memory Lane.’’
Makala hii naamini wengi waliipenda.

Nikafuatia na makala mengine, ‘’Salim Himidi akiadhimishwa na gazeti la Raia Mwema,’’ baada ya makala hizi kuchapwa na kusomwa na wasomaji wengi marafiki zake wakaanza sasa kunitumia picha zake na habari zake nyingi.

Ilikuwa kama vile walikuwa wananitaka mimi niandike historia ya Salim Himidi.

Lakini kuandika historia ya mtu kama Salim Himidi inataka makamo ya kila kitu kuanzia umri hadi uwezo wa akili.

Nikapokea picha ya Salim Himidi na Nelson Mandela, Salim Himidi na Salim Ahmed Salim, Salim Himidi na Raisi wa Senegal Leopold Sedar Senghor, Salim Himidi na Rais Sassou Nguesso wa Congo Brazaville, Salim Himidi anatoa hotuba Umoja wa Mataifa, Salim Himidi na Seif Shariff Hamad katika gari ya wazi Comoro.

Nililetewa picha nyingi akiwa katika matukio mengi kama Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Pamoja na picha hizi pia nikatumiwa mengi ambayo Salim Himidi alifanya katika kuitumikia nchi yake kuanzia kupigania uhuru wa Comoro na misukosuko kutoka serikali ya Ufaransa na wakati mwingine misukosuko ya vibaraka wa ndani.

Salim Himidi ni jahazi lililobeba vito vya thamani linapotia linaposafiri baharini na linapotia nanga bandarini linahitaji nahodha aliye na ujuzi wa kutosha sana na ulinzi mkali usio na shaka.

Mara ya mwisho kuonana na Salim Himidi ilikuwa mwaka wa 2017 na ikasadifu kuwa Sal Davis alikuwapo Dar es Salaam.

Salim kama mimi akiusudu sana muziki wa somo yake Salim Abdallah Salim maarufu kwa jina la Sal Davis. Nikamchukua Salim barzani kwetu ambako kila jioni anapokuwa Dar es Salaam Sal Davis huja pale.

Ilikuwa imepita miaka 54 toka Salim amuone Sal Davis Zanzibar mwaka wa 1963 siku hizo Sal Davis wakati huo yuko juu katika muziki wake alipofanya onyesho Ukumbi wa Sayyid Khalifa.

Umri wao wote wawili wakati ule ilikuwa si zaidi ya miaka 23 hivi.

Ujana ni wazimu.

Ukumbi ulijaa pomoni hakuna kijana aliyebakia nyumbani siku ile.

Wakongwe hawa wawili mmoja ‘’Cabaret Star,’’ na mwingine ‘’Diplomat,’’ kila mmoja akiwa ameacha alama katika fani yake walisalimiana.

Nimekaa pembeni nikiwaangalia.

Salim akamkumbusha lile onyesho la mwaka wa 1963 kisha akamwambia Sal Davis, ‘’Baada ya show ulitoka nje kundi kubwa likikuzonga ukaingia kwenye gari llilokuwa likiuza, ‘’ice cream,’’ pale nje ya ukumbi.

Ulichukua microphone iliyokuwa ndani ya ile gari ukaimba nyimbo moja ya Perry Como nasi tukikusikiliza kutoka vile vipaza sauti vilivyokuwa kwenye kipaa cha ile gari.’’

Sal Davis alikaa kimya kwa muda kisha akasema, ‘’Salim una kumbukumbu kali sana ni miaka mingi imepita.’’

Hakika kati ya watu hawa wawili mengi baina yao katika dunia zao yalikuwa yamepita.

Si rahisi kumwandika Salim Himidi ukammaliza na ndiyo maana kila nilipokutana na rafiki yangu nilikuwa namwimbia mwimbo mmoja tu nikiuurudia mara zote kuwa aandike kumbukumbu zake.

Bahati mbaya sana kwetu Salim kaondoka bila ya kutuachia elimu na uzoefu mkubwa wa siasa za ulimwengu na Afrika uliokuwa kichwani kwake.

Lakini mimi angalau nina ya kueleza kwa yale machache ambayo nilijaaliwa kuyaokota kutoka kwake tukiwa Tanga, Barzani Dar es Salaam na tukiwa Paris tukizungumza katika mgahawa wetu wa yule Muhindi kutoka Zanzibar au tukitembea taratibu Champse Elysees.

Hakika Salim Himidi kwa kutotuachia kumbukumbu zake amekuwa mfano wa jahazi lililozama na shehena yake yote ya vito vya thamani kubwa kupotea.

Allah mpokee nduyu yetu Salim Himidi kwa salama na amani, msamehe na amtie mahali pema peponi.

Amin.

PICHA: Kulia Salim Himidi, Mwandishi na Mohamed Mshangama
Kitabu cha Sal Davis
Salim Himidi akihutubia Umoja wa Mataifa

1694277788299.png

1694277950583.png

1694278001934.png
 
Hakika alikua mutu makini.sema changamoto hakuandika kumuhusu YY mwenye.
 
Sijasoma Uzi, lakini naombeni kubahatisha
Hakuna stori za waislam kuonewa sana humu?
 
Sijasoma Uzi, lakini naombeni kubahatisha
Hakuna stori za waislam kuonewa sana humu?
Historia hii ya uhuru wa Tanganyika na yale ambayo yalifutwa tatizo hili lilimalizwa na kitabu cha Abdul Sykes baada ya kuchapwa 1998.

Kitabu hiki ndicho kilichowafahamisha wanafunzi wa historia ya TANU kuwa ni lazima watambue kuwa fikra ya kuasisi African Association Kleist Sykes aliipata kutoka kwa Dr. Kwegyir Aggrey 1924.

Hili halikuwa likisemwa.

Kleist Sykes ndiye aliyeandika historia ya African Association na kututajia kuwa President alikuwa Cecil Matola na alifariki 1934 na nafasi yake ikachukuliwa na Mzee bin Sudi.

Kleist na Mzee bin Sudi wakiwa viongozi wa AA wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 ili kuepusha mambo ya Waislam kwenda serikalini kupitia AA.

Hili walikuwa pia wengi hawalijui.

Katueleza Kleist katika mswada wake wa kitabu huo hapo chini:

(AD Sykes Seminar Paper: "The Life of Kleist Sykes," Ref. No. JAN/HIST/143/15, East Africana, University of Dar-es-Salaam 1968).

Haya ninayokueleza yote yamo humo.

Hakuna rais wa kwanza wa TAA bali Rais wa kwanza wa AA 1929 Cecil Matola.

Dr. Kyaruzi kawa Rais wa TAA 1950 hapo AA ishabadili jina toka 1948 na kuwa TAA na Katibu alikuwa Abdul Sykes.

Wakati jina linabadilishwa Rais alikuwa Thomas Plantan na Secretary Clement Mohamed Mtamila.

Haya hawakuwa wanayajua.

Kitabu cha Abdul Sykes kimeeleza historia hii na vipi Dr. Kyaruzi alichaguliwa.

Kuhusu Rais wa TANU kitabu cha Abdul Sykes kilishamaliza tatizo hili sasa huu mwaka wa 25 yaani robo karne na Abdul Sykes na Ally Sykes wamepewa Medali ya Mwenge wa Uhuru 2011 kwa mchango wao katika kuunda TANU.

Historia hii ipo katika Cambridge Journal of African History (1988/89) na katika Dictionary of African Biography (2011).

Hii ndiyo historia ya Julius Nyerere hivi sasa.
 
Historia hii ya uhuru wa Tanganyika na yale ambayo yalifutwa tatizo hili lilimalizwa na kitabu cha Abdul Sykes baada ya kuchapwa 1998.

Kitabu hiki ndicho kilichowafahamisha wanafunzi wa historia ya TANU kuwa ni lazima watambue kuwa fikra ya kuasisi African Association Kleist Sykes aliipata kutoka kwa Dr. Kwegyir Aggrey 1924.

Hili halikuwa likisemwa.

Kleist Sykes ndiye aliyeandika historia ya African Association na kututajia kuwa President alikuwa Cecil Matola na alifariki 1934 na nafasi yake ikachukuliwa na Mzee bin Sudi.

Kleist na Mzee bin Sudi wakiwa viongozi wa AA wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 ili kuepusha mambo ya Waislam kwenda serikalini kupitia AA.

Hili walikuwa pia wengi hawalijui.

Katueleza Kleist katika mswada wake wa kitabu huo hapo chini:

(AD Sykes Seminar Paper: "The Life of Kleist Sykes," Ref. No. JAN/HIST/143/15, East Africana, University of Dar-es-Salaam 1968).

Haya ninayokueleza yote yamo humo.

Hakuna rais wa kwanza wa TAA bali Rais wa kwanza wa AA 1929 Cecil Matola.

Dr. Kyaruzi kawa Rais wa TAA 1950 hapo AA ishabadili jina toka 1948 na kuwa TAA na Katibu alikuwa Abdul Sykes.

Wakati jina linabadilishwa Rais alikuwa Thomas Plantan na Secretary Clement Mohamed Mtamila.

Haya hawakuwa wanayajua.

Kitabu cha Abdul Sykes kimeeleza historia hii na vipi Dr. Kyaruzi alichaguliwa.

Kuhusu Rais wa TANU kitabu cha Abdul Sykes kilishamaliza tatizo hili sasa huu mwaka wa 25 yaani robo karne na Abdul Sykes na Ally Sykes wamepewa Medali ya Mwenge wa Uhuru 2011 kwa mchango wao katika kuunda TANU.

Historia hii ipo katika Cambridge Journal of African History (1988/89) na katika Dictionary of African Biography (2011).

Hii ndiyo historia ya Julius Nyerere hivi sasa.
Kweli,waislam wanaonewa sana duniani
 
Kweli,waislam wanaonewa sana duniani
MAELEZO MAFUPI KUHUSU PICHA SHAMBANI KWA CHAUREMBO MTONI 1956

Kuna kijana kawatukana waliokuwa katika picha ile ukimtoa Julius Nyerere na John Rupia.

Hakika kakosa adabu.

Lakini dharau hii kwake imekuja kwa kuwa hakusomeshwa historia ya watu hawa.

Nimeamua kumweleza kwa kifupi historia ya baadhi ya hawa wazalendo:

"Kijana jizuie na maneno yasiyopendeza.

Hao baadhi yao ni babu na baba zetu na watu walio na heshima kubwa katika historia ya Tanganyika.

1. Dossa Aziz alikuwa rafiki wa Mwalimu Nyerere na mfadhili wa TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

2. Mwalimu Thomas Plantan mtoto wa Chief Mohosh, Mzulu kutoka Shangaan na Imhambane.

Thomas Plantan alikuwa Rais wa AA/TAA hadi 1950 alipopinduliwa na vijana.

3. Sheikh Haidar Mwinyimvua Mjumbe Halmashauri Kuu ya TANU na mmoja wanachama wa mwanzo wa TANU 1954.

4. Omar Londo mwanachama shupavu wa TANU 1954 na amepewa mtaa kwa heshima ya mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

5. Abdulwahid Sykes baba yake, Kleist Abdallah Sykes ndiye aliyeasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 na ndiye aliyeandika historia ya African Association.

Mswada alioandika ni Seminar Paper imehifadhiwa East Africana Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.

Abdul Sykes ndiye aliyempokea Mwalimu Nyerere Dar-es-Salaam na kati ya waasisi 17 wa TANU kadi yake ya TANU ni No. 3.

6. Mwinjuma Mwinyikambi Mjumbe Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe 120.

7. Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU 1954 - 1958.

8. Rajabu Diwani kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU 1954.

9. Muhsin Mende kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU.

10. Sheikh Mohamed Mattar akijulikana zaidi kama Maalim Mattar mwalimu shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika akisomesha Qur'an.

11. Ali Mwinyi Halwa maarufu Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika ).

Alifuatana na Abdul Sykes kwenda Nansio, Ukerewe kuonana na Hamza Mwapachu kujadili kumwingiza Julius Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA 1953 kisha iundwe TANU 1954.

12. Said Chaurembo Mjumbe wa TAA Political Subcommittee 1950.

Wengine kama Julius Nyerere na John Rupia kwa makusudi nimewaacha kwani wanafahamika vyema."
 
Back
Top Bottom