Siku moja na Sir Andy Chande

Leo ndio siri imefichuka, ni wazi Dr Dau amewabeba sana ndugu zake katika imaani hasa huyu Mzee Mohammed Said, karani ambaye alikuwa na access ya kuingia hadi board meeting.
Hahahahahahhahahahhhhh
 
Kwa kifupi those days bandari ilikuwa ni mali ya Mzee Janguo na kabla wapemba hawajatuharibia kujilipuwa tulikuwa tukienda UK kama unavyokwenda South Africa tu kwa sasa bila kuomba viza ubalozini, sasa kama manoti unayo ni kwa nini weekend usilikwee BA to Heathrow London? Mambo yamebadirika sana.
lile lenye ghorofa tulikuwa tunaliita kichwa cha d*ck
 
Muhamakilo,
Unajua inawezekana kuwa mimi ndiyo mtu wa kwanza kuandika
maisha ya Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wakati wa utafiti na baada ya kutoka kitabu kile cha Abdul Sykes
watu wengi sana walinijia kwa mazungumzo ya kawaida tu na
baadhi ya watu hawa walikuwa na Mwalimu Nyerere kwa karibu
sana.

Wote wanasema Mwalimu Nyerere alikuwa na uadilifu wa hali ya juu
katika sauala fedha na hii toka enzi za TANU 1954.

Utajiri haukumshughulisha.
Haya Maalim...
 
Hivi wewe na wale si Mange kasema? Mna tofauti gani? Umesahau Kambona kwamba ni mwanasiasa?

Umesahau fix tuliyopigwa eti Kambona kashinda bahati nasibu ya dunia anarudi Tanzania na Land cruiser 300? Hivi unadhani ni kwa nini watu wengi walijiunga na Tadea?

Wabongo ni poor IQ hata kuutafuta ukweli ni shida Kambona amerudi Tanzania hana lolote na tumshukuru Mzee Mwinyi uchaguzi wa mwaka 1995 ruzuku kwa wagombea wa vyama vyote ngazi zote na mawakala wote pesa zilitolewa na serikali ya Mwinyi.

Ukiniuliza leo nitamkumbuka Mwinyi kwa lipi hakika kwa hili hata mimi kwa mara ya kwanza na ya mwisho nilikula pesa ya serikali burebure kabisa.

Uchaguzi ule ndio ulisababisha kuzaliwa vyama holela na wagombea holela wakidhani pesa za bure kama zile za mwaka 1995 zitarudi tena.

Mtu anachukuwa fomu kwenye chama kama cha Dovutwa kugombea ubunge serikali inampa ruzuku cash money millioni 5 mtu anatokomea hakuna cha kufanya kampeni wala nini.

Utaratibu ule ungeendelezwa hadi leo ingekuwa tuna vyama 1000 mpaka sasa.
Eti Mange Kimambi daah...haya mkuu pamoja.
 
Ikawa sasa nimemfahamu Chande kutoka kwa mwanachama mwenzake wa hiyo ‘’club,’’ yao. Siku moja nikamuuliza mzee wangu, ‘’Hii ‘’club,’’ yenu ni ‘’club,’’ gani?’’ Akanitazama usoni huku kakunja uso akaniuliza, ‘’Wewe unaitakia nini?’’

Sikuuliza tena hilo swali lakini iko siku akanitajia.,...........

" Ndugu Mohamed hapa umeniacha....hiyo siku alikutajia hiyo " club" ni club chenye kujishughulisha na nini....! ukizingatia sheria zake kuwa ni kali... please dadavua kidogo hofu ituondoke kuwa hicho ni chama kams kile cha devil woshiper...... tukisikiaga huko kuna sheria kali kali sana.....
 
Narudia tena, hakuna , hakuna! aliyewahi kuthibitisha pesa za Kawawa, Nyerere au Amir Jamal nje ya nchi.

Kumsikia Kambona akisema hakufanyi kuwa ukweli
Nani alitegemea Kambona ataongea jambo zuri kuhusu Nyerere kwa ugomvi wao?

Hadi anafariki, hakuna aliyewahi kuthibitisha madai akiwemo Kambona mwenyewe

Vijana wa leo wanasikia tu na kuamini, walioishi zama hizo wanajua ukweli

Kuna Anour Kassum,alikuwa waziri na moja ya wizara alizodumu ni Madini na Nishati. Leo kama angekuwa sawa na 'fisi' tulio nao, tusingekuta hata mchanga wa kujaza katroli. Nani alikuwa na ufahamu wakati huo?

Tuwape heshima waliotumikia Taifa tukalikuta lilipo, tuache hadithi za kuzusha tu

JokaKuu
Kambona ndie aliwaambukiza uongo na uzushi wapinzani
Tuliambiwa gesi inatoka mtwara inakwenda bagamoyo hivyo wakazi wa mtwara waasi,operesheni iliongozwa na JJ mnyika
 
Nakumbuka sana zamani tuliaminishwa Saab Scania ni investment ya Nyerere pia.

I don't buy this nonsense.
Mkuu yaani Taifa letu linasikitisha sana.

Watu hawana muda wa kutafuta ukweli au kufikiria zaidi, wana muda wa kupiga majungu na kuendeleza uongo.

Leo akisema Mtu Matola anamiliki Serena Hotel wapo watakaoamini,'tuliambiwa'

Huyo anayezungumzia Nyerere, Kawawa, Jamal kuficha mapesa hana mstari hata mmoja wa kutetea hoja yake. Anachojua 'Kambona alisema'.

Hata kama Kambona angesema Kawawa alikuwa Jambazi kabla ya siasa, ataamini tu

Akihadithiwa Nyerere aliwahi kupeleka posa ya Malkia, ataamini. Kaambiwa na fulani

Akiambiwa Amir Jamal alikuwa waziri mkuu wa India kabla ya kuja Tz, ataamini
 
Kwa kifupi those days bandari ilikuwa ni mali ya Mzee Janguo na kabla wapemba hawajatuharibia kujilipuwa tulikuwa tukienda UK kama unavyokwenda South Africa tu kwa sasa bila kuomba viza ubalozini, sasa kama manoti unayo ni kwa nini weekend usilikwee BA to Heathrow London? Mambo yamebadirika sana.
waliharibu vipi hao mpaka ikahitajika visa kwenda kwa Malkia?
 
Back
Top Bottom