Sie tunywe tu mbinguni si tutapewa miili mipya

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,373
Wasalam,

B81A04DF-D48B-46BA-B37D-8D64B8839A62.jpeg



Sisi vijana tumekuwa na kauli nyingi sana za kishujaa na za kupeana matumaini kwenye maswala mazima ya starehe kama kumwagilia moyo na kuburudika nafsi na kusahau ili tuweze kufanya mambo yetu tofauti fofauti na kuweza kufikia malengo yetu tunaitaji afya pia,
Nimetanguliza kichwa hiki hiyo ni moja ya kauli pendwa sana za sisi vijana kwenye swala zima la kuponda raha au kuupa mwili faraja (Addiction)

Hiyo picha hapo ni ya Jamaa mmoja kutoka huko calfornia Marekani aitwaye Austin Ambaye alipoteza sehemu kati ya sehemu za fuvu lake baada ya kukithirisha unywaji wa vinywaji aina ya Energy drinks.

Austin alianza unywaji wa energy drinks kwa wingi ili apate muda mwingi sana wakufanya kazi kutokana na masaa aliyotakiwa kufanya kazi dhamira ikiwa ni kuupatia mwili nishati ili kukabiliana na uchovu.
Kwa bahati mbaya sana mfumo huu ulipelekea Addiction na akawa anachukua kwa kiwango kikubwa mno, na mwishowe katika athari za kiafya ikapelekea brain haemorrhage baada ya pressure kuongezeka kwenye mirija ya damu iliyopo karibu na ubongo, kutokana na tatizo hilo ambalo pengine lingegharimu maisha ya Austin.

Wataalamu na timu ya madaktari ilifanya toxicology screening ili kung'amua tatizo, madaktari walitambua matumizi ya energy drinks yaliyokithirishwa ndio sababu kubwa iliyopelekea tatizo .

AF08B9C7-2242-44F1-8C8F-14FF9B70889C.jpeg


Kufuatia uchunguzi huo, Austin alifanyiwa pasuaji tofaouti tofauti za ubongo ambazo pia zilizosababisha kupata side Effects kadhaa kama Kuvimba kwa ubongo, kupata strokes , seizures na shida nyingine tofauti tofauti, na mwishowe wataalamu wakafanya pasuaji kuondoa sehemu ya fuvu lake la mbele(Frontal Skull). Ili kupunguza pressure kwenye ubongo

Scenario hii hutumika sana kuwakumbusha vijana kuhusu kutumia vinywaji kama energy na vinavyofanana na hivyo kwa kiwango maalumu ili kupunguza athari za kiafya kama hizo

D8A29B6A-CC04-4823-8DCA-8619CD95AD6E.jpeg

Ukienda hospital leo hii hasa hasa wagonjwa wanaosumbuliwa magonjwa sugu kama pressure na Kisukari maisha yao yapo chini ya lifestyle modification, mara nyingi ni kuhusu chakula, kula vyakula au vinywaji venye mpangilio maalumu kutoka kwa daktari, mazoezi na matibabu mengine.

Mara nyingi vijana tunapena kauli za ushujaa zinazoambatana na utani ili tu kumotivate na kuhamsha hisia inayochochea uvunjifu fulani wa kanuni ya afya kwa namna moja ama nyingine mfano.

Kukithirisha kunywa vinywaji kama energy ambavyo vina contents nyingi kama , caffeine ambayo mara nyingi ikichukuliwa kwa wingi basi huchochea kupata shida kwa mtumiaji kama pressure ,pia vinywaji hivo huwa na kemikali nyinginezo ambazo kikawaida hazitakiwi kuwa nyingi katika mwili wa mwanadamu.


Leo hii vijana sie tumekuwa mstari wa mbele kwenye uvunjifu wa kanuni hizi na kupeana kauli fulani , za kishujaa na kujifariji mfano
Utaskia we kunywa tu kila mtu atakufa mbinguni tutapewa miili mipya.

Yote haya tunayafanya kwakuwa bado hatujatetereka wala kudhoofu hali
Ikifikia point tunashindwa kuinuka na tupo hoi kitandani hatujiwezi ndipo tunapokumbuka umuhimu wa mtaji huu uitwao Afya

5F10427D-6143-498C-B8A5-0D9133B94093.jpeg


NB: Hajakatazwa mtu kuponda raha zake , Lakini Jali AFYA yako afya ni MTAJI.



DaVinci XV
 
Back
Top Bottom