Siasa za majitaka, Hivi Tanzania ni Kisiwa cha kilichojitenga pekee duniani!

Kasimba G

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,428
2,609
Kwa wafuatiliaji wa siasa ulimwenguni watakuwa pamoja na mimi kuwa siasa za majitaka wakati wa uchaguzi haziepukiki, kinadhalia inawezekana lakini kwa utekelezaji ni haiwezekani kabisa. Uchaguzi wa Marekani walisema Obama na Osama wana undugu kiasi cha kuteka hisia za wamerekani wahafidhina wengi na kumponda Obama kuwa hafai. Siasa za majitaka zilisema Obama sio raia wa Marekani zikapelekea Obama kujibu kwa kuonyesha cheti chake cha kuzaliwa n.k,

Urusi hapa juzi siasa za majitaka zilichukua kasi na kusababisha Putin kutokujiamini, bila ukachero Putin asingegombea. Siasa za majitaka huwa zinaaambatana na mambo ya hovyo machache ambayo mgombea aliishawahi fanya au anayofanya pamoja na mambo mengi ya uongo ya uchafuzi.

Naona watu wengi hata humu jamvini wanachangia kuwa siasa za majitaka zisipewe nafasi hapa kwetu Tanzania, je sisi ni kisiwa kilichojitenga na cha waelevu saana kiasi cha kuwa na utamaduni unaoenda tofauti kabisa na utamaduni duniani kwa sasa?

Kwa mtazamo wangu siasa za uchaguzi ni mkusanyiko wa siasa nyingi, majitaka , kuelezea sera, uzushi, ukweli n.k.

Nawasilisha.
 
Siasa za majitaka ni JADI ya CCM. Walifundishwa mbinu hizi na KGB (enzi hizo) kule Bulgaria, Yugoslavia na Poland. We unadhani hiyo kozi aliyoenda Mrema kusomea kule Poland ilikuwa ya nini?
 
Wasalam nNg wana JF,

Habarini za muda huu, kwa kweli nafikiria sana na kuwazua kuhusu siasa za Ndg yetu, mdogo wetu Ndg Mwigulu Nchemba, hakika nadhani siasa imeingiliwa na mtu ambaye sio sahihi kuwa mahali hapo, kwanini kila anapokuwa katika kampeni zake zote anasababisha mauaji huyu mtu?

Arumeru, Igunga, Ndago, Arusha, u wapi uadilifu wake, anyway malipo yake ni hapahapa duniani, kama ni kweli kwa namna moja anahusika kumwaga damu ya watu basi hukumu yake ipo, yetu macho, ila kwa kweli naiona roho ya ibilisi inguoni mwako, endelea kuvaa kofia yako yenye alama nyekundu katika paji la uso wako, wape na wengine hizo kofia, naona kwa Martha Mlata kavaa hizo kofia?
 
Mwigulu Tanzania ina watu zaidi ya Milioni 45 sote tunaangalia jinsi ulivyoamua kuiharibu.
 
Amekuwa akisema ccm lazima itashinda kwa damu au kwa nyama sijui anamanisha nini.
 
mwigulu nchemba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mwigulu nchemba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mwigulu nchemba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mwigulu nchemba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mwigulu nchemba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mwigulu shetani gani uliyenaye anayeangamiza ROHO za WATZ....HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KUWATUMIKIA MABWANA 2 KWA WAKATI MMOJA...SHETANI NA MUNGU...
 
hakika naomba watu wa iramba magharibi kuweni makini na huyu mtu hakika ana mambo ya kishirikina ktk kulazmisha kutawala ,waliomchagua sio washez,hawakumjua vizuri kumbe ni m.bwa mwitu,hakika kijana mbaya huyu,laana zimfikie kule aliko,Ombea adui yako aishi siku nyingi ili mtakapofanikiwa ajionee kwa macho,
 
Mwigulu nchemba hajui siasa za kiushindani! Waliofanya kosa ni ccm kwa kumpa kichaa rungu, tukio la arusha mwigulu anahahusika 100%, kama tungekuwa na vyombo vya usalama imara kwa mustakabali wa watanzania wote, huyu ndugu angekuwa lupango, mwigulu anahusika na mauaji kama ya Ndago, iringa, arumeru na hata igunga. Watanzania huyu mtu ni janga kwa taifa letu!
 
We wanna thanks u you father for making politicians be able to lie with the straight face while the nation crying. By lucky dube rasta man prayer
 
Back
Top Bottom