Siasa VS Uchumi: Sakata la Bandari zetu

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
7,786
15,732
Ni dhahiri wa shahiri kuwa watanzania wengi hawana uelewa wa mambo mengi, na kwamba wako tayari kuchukua upande mmoja pindi itokeapo hoja yoyote ya nchi, haijalishi ina maslahi au haina maslahi kwa Taifa letu.

Suala la Bandari, limekuwa hyped sana kwa siku 2 hizi, upande mmoja ukisema Bandari inauzwa, na upande mwingine wanapinga kuwa hakuna makubaliano hayo.

Watu wengi hapa wamejigawa kichama yaani CHADEMA VS CCM na sio kujenga hoja kwa mustakabali wa nchi na kuujua ukweli wenyewe wa mkataba, sambamba na faida na hasara zake.

CHADEMA wameichukua hii hoja kisiasa zaidi, na wakiamini watagain kwenye siasa, wakati CCM wameichukua hii hoja kiuchumi zaidi na hawana uhakika wa kugain kisiasa.

Matamko karibu yote yanalenga zaidi kujikuza kisiasa zaidi ya kiuchumi.

Kwa watu wanaotazama Uchumi zaidi, tunaona ni Bora shughuli za uendeshaji wa Bandari ziwe kwa kampuni binafsi huku Serikali ikihusika na ukusanyaji wa mapato tu, na uendeshaji wa gati za mafuta nk.

Tumekuwa tukilalamika hapa, Bandari haina ufanisi, ukiagiza gari hadi kulipata ni shida, makontena yanakaa hadi mwezi pale Bandarini, lkn wizi uliokithiri kwa wafanyakazi wasio waaminifu, hali hii imepelekea Bandari kuwa na ufanisi mdogo zaidi licha ya uwekezaji mkubwa unaofanywa.

Kwanini naona watu wanachanganya SIASA na UCHUMI? Wengi wanaotoa matamko hawana elimu yoyote ya uchumi wala fedha, wala biashara. Wengi ni waliosomea ualimu wa Kiswahili, wanasheria, wasiosoma kabisa nk.

Tunapojenga hoja za Kuwekeza katika Bandari zetu, tuelekeze nguvu kwenye namna ya kuboresha ufanisi wa hizi Bandari, nini kifanyike, wapi parekebishwe na wapi paachwe kama ilivyokuwa.

Ni hatari kwa nchi kutegemea watu kama Yericko Nyerere, Ex Meya, Malisa, Mbowe nk kuwa eti ndio wanauchungu na nchi hii kuliko watu wengine wowote. Ni lazima tutenganishe Siasa na Uchumi. Tujenge hoja kwa muktadha wa kiuchumi na sio Siasa. Bandari nyingi Duniani zinaendeshwa kwa mfumo huu, wa kwamba Operesheni hufanywa na Private sector na umiliki ni wa Government, yapo makampuni makubwa sana hufanya kazi hizi mfano, Bollore, PSA, nk.

Shida ni nini?
1. Hapa kuna kundi la watu wao ishu sio Bandari kupewa wageni kufanya kazi la hasha, hawa hawataki tu uwekezaji wa WAARABU, kundi hili hata uliambie nini wao wataweka hoja za Uarabu na si Kiuchumi zaidi. Kundi hili wako tayari Bandari wapewe wazungu. Kundi hili limejaa zaidi UDINI.

2. Kuna kundi wao ni CHADEMA, yaano hakuna kitu, au program ya Serikali itawekwa na wao wakakubaliana nayo, upotoshaji hapa ndio umelala zaidi. Matamko, hashtag nk, kundi hili halijawahi kupongeza kwa lolote na kwamba wao ndio wanaweza kuongoza nchi hii, ingawa wameshaprove kufeli hata ndani ya chama tu.

3. Hapa kuna kundi, linataka kujenga hoja, ila kwakuwa hawajasoma au kufatilia mkataba wenyewe basi wapo kujichagulia upande wanaoona wao unafaa.

Ni hivi wadau, hii nchi yetu sote, hakuna kiongozi mwenye lengo la Kuongoza nchi masikini Duniani. Nchi hii ina wanasheria wengi sana, Majaji wengi sana, wanaojua mikataba wengi sana nk, haiwezekani Mkataba uletwe hauna maelezo ya kueleweka.

Watu wengi wako na kipengele cga ukomo wa mkataba, wengine wanasema hauna mwisho ma wengine Miaka 100, mradi kuvuga hoja tu.

Sio kila mkataba una time frame jamani, kuna mikataba inamalizika pindi kazi ikiisha. Mfano kazi ya uongezaji wa Kina, itafanyika Milele?, Ujenzi wa Gati unafanyika milele? Sijaona kipengele chochote cha Miaka 100 wala waliposema watafanya milele na hakuna kuvunjwa. Kama mtapitia Article 23 basi mtajaribu kuona utaratibu gani wa kufanya ikitokea kuna shida.

Binafsi naona ni hatua nzuri kwa Serikali kiachia shughuli za Bandari ziendeshwe na Private sector ili kuleta ushindani dhidi ya Mombasa.

Tutenganishe SIASA na UCHUMI.
 
Umesema hoja nzuri tu, japo na wewe ukiwa na pressure ya kisiasa.

Maswali Yangu ni.
-Je vipi mkataba na Sheria zake umejikita kutetea rasilimali za nchi yetu?

- Mkataba umeeleza kuwa hauna ukomo mpaka pale mahakama ya ushuruhishi itakapoamua ukome Kwa kuangalia hoja za pande zote mbili hasa pale kutakapotokea mgogoro je iko sawa?

-Je vipi na matakwa mengine ya mkataba haya athari za kiuchumi, kijamii kiutamaduni au kimazingira?

Kumbuka tunaitafuta Tanzania ya vizazi vijavyo
 
IMG-20230608-WA0013.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema hoja nzuri tu, japo na wewe ukiwa na pressure ya kisiasa.
Maswali Yangu ni.
-Je vipi mkataba na Sheria zake umejikita kutetea rasilimali za nchi yetu?
-Mkataba umeeleza kuwa hauna ukomo mpaka pale mahakama ya ushuruhishi itakapoamua ukome Kwa kuangalia hoja za pande zote mbili hasa pale kutakapotokea mgogoro je iko sawa?
-Je vipi na matakwa mengine ya mkataba haya athari za kiuchumi, kijamii kiutamaduni au kimazingira?
Kumbuka tunaitafuta Tanzania ya vizazi vijavyo
Mkataba umejikita katika kuongeza ifanisi na hali ya uchumi wa nchi yetu.

Mkataba unalinda mali za taifa, kiuchumi, Tamaduni nk. Ieleweke kuwa mkataba sio wa mauziano ya Bandari, bali tenda ya Kufanya shughuli za bandari kama kupakua na kupakia mizigo.

Uwekezaji mkubwa lazima uwe na vipengele vingi vya kulinda mwekezaji na Serikali, kampuni iwekeze Tril 20 afu unataka kuvunja mkataba unapajisikia tu bila utaratibu mkuu.

Dangote kule Mtwara uwekezaji wake ni Tril kibao, na hana limit ya muda kutokana na uwekezaji wake.
 
Watetezi wa mambo ya ovyo wamejazwa Kila Kona. Ni aibu na fedheha kwa taifa.
 
Ni dhahiri wa shahiri kuwa watanzania wengi hawana uelewa wa mambo mengi, na kwamba wako tayari kuchukua upande mmoja pindi itokeapo hoja yoyote ya nchi, haijalishi ina maslahi au haina maslahi kwa Taifa letu.

Suala la Bandari, limekuwa hyped sana kwa siku 2 hizi, upande mmoja ukisema Bandari inauzwa, na upande mwingine wanapinga kuwa hakuna makubaliano hayo.

Watu wengi hapa wamejigawa kichama yaani CHADEMA VS CCM na sio kujenga hoja kwa mustakabali wa nchi na kuujua ukweli wenyewe wa mkataba, sambamba na faida na hasara zake.

CHADEMA wameichukua hii hoja kisiasa zaidi, na wakiamini watagain kwenye siasa, wakati CCM wameichukua hii hoja kiuchumi zaidi na hawana uhakika wa kugain kisiasa.

Matamko karibu yote yanalenga zaidi kujikuza kisiasa zaidi ya kiuchumi.

Kwa watu wanaotazama Uchumi zaidi, tunaona ni Bora shughuli za uendeshaji wa Bandari ziwe kwa kampuni binafsi huku Serikali ikihusika na ukusanyaji wa mapato tu, na uendeshaji wa gati za mafuta nk.

Tumekuwa tukilalamika hapa, Bandari haina ufanisi, ukiagiza gari hadi kulipata ni shida, makontena yanakaa hadi mwezi pale Bandarini, lkn wizi uliokithiri kwa wafanyakazi wasio waaminifu, hali hii imepelekea Bandari kuwa na ufanisi mdogo zaidi licha ya uwekezaji mkubwa unaofanywa.

Kwanini naona watu wanachanganya SIASA na UCHUMI? Wengi wanaotoa matamko hawana elimu yoyote ya uchumi wala fedha, wala biashara. Wengi ni waliosomea ualimu wa Kiswahili, wanasheria, wasiosoma kabisa nk.

Tunapojenga hoja za Kuwekeza katika Bandari zetu, tuelekeze nguvu kwenye namna ya kuboresha ufanisi wa hizi Bandari, nini kifanyike, wapi parekebishwe na wapi paachwe kama ilivyokuwa.

Ni hatari kwa nchi kutegemea watu kama Yericko Nyerere, Ex Meya, Malisa, Mbowe nk kuwa eti ndio wanauchungu na nchi hii kuliko watu wengine wowote. Ni lazima tutenganishe Siasa na Uchumi. Tujenge hoja kwa muktadha wa kiuchumi na sio Siasa. Bandari nyingi Duniani zinaendeshwa kwa mfumo huu, wa kwamba Operesheni hufanywa na Private sector na umiliki ni wa Government, yapo makampuni makubwa sana hufanya kazi hizi mfano, Bollore, PSA, nk.

Shida ni nini?
1. Hapa kuna kundi la watu wao ishu sio Bandari kupewa wageni kufanya kazi la hasha, hawa hawataki tu uwekezaji wa WAARABU, kundi hili hata uliambie nini wao wataweka hoja za Uarabu na si Kiuchumi zaidi. Kundi hili wako tayari Bandari wapewe wazungu. Kundi hili limejaa zaidi UDINI.

2. Kuna kundi wao ni CHADEMA, yaano hakuna kitu, au program ya Serikali itawekwa na wao wakakubaliana nayo, upotoshaji hapa ndio umelala zaidi. Matamko, hashtag nk, kundi hili halijawahi kupongeza kwa lolote na kwamba wao ndio wanaweza kuongoza nchi hii, ingawa wameshaprove kufeli hata ndani ya chama tu.

3. Hapa kuna kundi, linataka kujenga hoja, ila kwakuwa hawajasoma au kufatilia mkataba wenyewe basi wapo kujichagulia upande wanaoona wao unafaa.

Ni hivi wadau, hii nchi yetu sote, hakuna kiongozi mwenye lengo la Kuongoza nchi masikini Duniani. Nchi hii ina wanasheria wengi sana, Majaji wengi sana, wanaojua mikataba wengi sana nk, haiwezekani Mkataba uletwe hauna maelezo ya kueleweka.

Watu wengi wako na kipengele cga ukomo wa mkataba, wengine wanasema hauna mwisho ma wengine Miaka 100, mradi kuvuga hoja tu.

Sio kila mkataba una time frame jamani, kuna mikataba inamalizika pindi kazi ikiisha. Mfano kazi ya uongezaji wa Kina, itafanyika Milele?, Ujenzi wa Gati unafanyika milele? Sijaona kipengele chochote cha Miaka 100 wala waliposema watafanya milele na hakuna kuvunjwa. Kama mtapitia Article 23 basi mtajaribu kuona utaratibu gani wa kufanya ikitokea kuna shida.

Binafsi naona ni hatua nzuri kwa Serikali kiachia shughuli za Bandari ziendeshwe na Private sector ili kuleta ushindani dhidi ya Mombasa.

Tutenganishe SIASA na UCHUMI.

"Ni hivi wadau, hii nchi yetu sote, hakuna kiongozi mwenye lengo la Kuongoza nchi masikini Duniani. Nchi hii ina wanasheria wengi sana, Majaji wengi sana, wanaojua mikataba wengi sana nk, haiwezekani Mkataba uletwe hauna maelezo ya kueleweka"

Mfano Chenge na Biswalo, hao ndo vinara wa ubora
 
Wanasiasa hucheza karata... Kuzuga kwingi !!
Kuna makampuni mengi ya kimataifa yenye ujuzi wa kuendesha bandari. Je sheria ya manunuzi ya ishindani imefuatwa?
Hao wabunge 10 waliotembezwa Dubai ni kweli walihongwa magari v8 na dollar 50,000? Hili ikibainikà kuwa kweli mkataba haufai na wabunge hao wavuliwe ubunge.
 
Nchi inataka kufanya maboresho ya bandari bungeni imefuata nini. Watu watoe maoni ya nini naona siasa kuliko uhalisia dp wapewe kazi tuone kontena zikipakiwa kwa wakati na milolongo ipunguwe sio ukipakia contena gari inachukua masaa ma4 kutoka getini. Watumie mfumo wa t.r.h ukipakia dakika 5 mzigo uko nnje
 
Ni dhahiri wa shahiri kuwa watanzania wengi hawana uelewa wa mambo mengi, na kwamba wako tayari kuchukua upande mmoja pindi itokeapo hoja yoyote ya nchi, haijalishi ina maslahi au haina maslahi kwa Taifa letu.

Suala la Bandari, limekuwa hyped sana kwa siku 2 hizi, upande mmoja ukisema Bandari inauzwa, na upande mwingine wanapinga kuwa hakuna makubaliano hayo.

Watu wengi hapa wamejigawa kichama yaani CHADEMA VS CCM na sio kujenga hoja kwa mustakabali wa nchi na kuujua ukweli wenyewe wa mkataba, sambamba na faida na hasara zake.

CHADEMA wameichukua hii hoja kisiasa zaidi, na wakiamini watagain kwenye siasa, wakati CCM wameichukua hii hoja kiuchumi zaidi na hawana uhakika wa kugain kisiasa.

Matamko karibu yote yanalenga zaidi kujikuza kisiasa zaidi ya kiuchumi.

Kwa watu wanaotazama Uchumi zaidi, tunaona ni Bora shughuli za uendeshaji wa Bandari ziwe kwa kampuni binafsi huku Serikali ikihusika na ukusanyaji wa mapato tu, na uendeshaji wa gati za mafuta nk.

Tumekuwa tukilalamika hapa, Bandari haina ufanisi, ukiagiza gari hadi kulipata ni shida, makontena yanakaa hadi mwezi pale Bandarini, lkn wizi uliokithiri kwa wafanyakazi wasio waaminifu, hali hii imepelekea Bandari kuwa na ufanisi mdogo zaidi licha ya uwekezaji mkubwa unaofanywa.

Kwanini naona watu wanachanganya SIASA na UCHUMI? Wengi wanaotoa matamko hawana elimu yoyote ya uchumi wala fedha, wala biashara. Wengi ni waliosomea ualimu wa Kiswahili, wanasheria, wasiosoma kabisa nk.

Tunapojenga hoja za Kuwekeza katika Bandari zetu, tuelekeze nguvu kwenye namna ya kuboresha ufanisi wa hizi Bandari, nini kifanyike, wapi parekebishwe na wapi paachwe kama ilivyokuwa.

Ni hatari kwa nchi kutegemea watu kama Yericko Nyerere, Ex Meya, Malisa, Mbowe nk kuwa eti ndio wanauchungu na nchi hii kuliko watu wengine wowote. Ni lazima tutenganishe Siasa na Uchumi. Tujenge hoja kwa muktadha wa kiuchumi na sio Siasa. Bandari nyingi Duniani zinaendeshwa kwa mfumo huu, wa kwamba Operesheni hufanywa na Private sector na umiliki ni wa Government, yapo makampuni makubwa sana hufanya kazi hizi mfano, Bollore, PSA, nk.

Shida ni nini?
1. Hapa kuna kundi la watu wao ishu sio Bandari kupewa wageni kufanya kazi la hasha, hawa hawataki tu uwekezaji wa WAARABU, kundi hili hata uliambie nini wao wataweka hoja za Uarabu na si Kiuchumi zaidi. Kundi hili wako tayari Bandari wapewe wazungu. Kundi hili limejaa zaidi UDINI.

2. Kuna kundi wao ni CHADEMA, yaano hakuna kitu, au program ya Serikali itawekwa na wao wakakubaliana nayo, upotoshaji hapa ndio umelala zaidi. Matamko, hashtag nk, kundi hili halijawahi kupongeza kwa lolote na kwamba wao ndio wanaweza kuongoza nchi hii, ingawa wameshaprove kufeli hata ndani ya chama tu.

3. Hapa kuna kundi, linataka kujenga hoja, ila kwakuwa hawajasoma au kufatilia mkataba wenyewe basi wapo kujichagulia upande wanaoona wao unafaa.

Ni hivi wadau, hii nchi yetu sote, hakuna kiongozi mwenye lengo la Kuongoza nchi masikini Duniani. Nchi hii ina wanasheria wengi sana, Majaji wengi sana, wanaojua mikataba wengi sana nk, haiwezekani Mkataba uletwe hauna maelezo ya kueleweka.

Watu wengi wako na kipengele cga ukomo wa mkataba, wengine wanasema hauna mwisho ma wengine Miaka 100, mradi kuvuga hoja tu.

Sio kila mkataba una time frame jamani, kuna mikataba inamalizika pindi kazi ikiisha. Mfano kazi ya uongezaji wa Kina, itafanyika Milele?, Ujenzi wa Gati unafanyika milele? Sijaona kipengele chochote cha Miaka 100 wala waliposema watafanya milele na hakuna kuvunjwa. Kama mtapitia Article 23 basi mtajaribu kuona utaratibu gani wa kufanya ikitokea kuna shida.

Binafsi naona ni hatua nzuri kwa Serikali kiachia shughuli za Bandari ziendeshwe na Private sector ili kuleta ushindani dhidi ya Mombasa.

Tutenganishe SIASA na UCHUMI.
Najua utatukanwa, lakini umeonfea UKWELI MTUPU.

Tuvilaza mno; watu wameikimbilia hii hoja ya bandari fasta kuelezea chuki zao za kidini walizonazo dhidi ya mtawala wetu na hao waarabu pamoja na kujaribu kujifufua kwa chama Chao kilichokufa.

Ningepata nafasi ya kumshauri mama, ningemwambia asisikilize kelele za chura; ye aendelee na mipango yake mpaka matokeo yatapoonekana watanyamaza wenyewe tu.
 
Kwanza mtoa mada ufahamu Watanzania kuhoji kuhusu jambo hili, ni haki yetu. Maana hii nchi siyo mali ya ccm au Chadema. Hii nchi ni mali ya Watanzania wote.

Halafu Watanzania tunahoji kuhusu huo mkataba, ni kwa sababu huko nyuma serikali imeshawahi kufanya madudu mengi kupitia mikataba ya kimangungo, na iliyokuja kuiletea hasara kubwa nchi baada ya kugundulika ni ya hovyo! Na hivyo kuamua kuivunja.

Kwa hiyo tunataka uwazi. Na hatufungwi kuhoji kisa tu tumesomea ualimu, ni wanasheria tusiojua uchumi, nk. Kama mngekuwa nyinyi mnaoujua huo uchumi mna tija ya maana kwenye nchi hii, msingeingia mikataba mingi ya kimangungu, huku mkitanguliza maslahi ya matumbo yenu.

Watanzania tunataka kujua ukomo wa huo mkataba. Na ni kwa nini huo mkataba ushinikize migogoro yote kusuluhishwa Afrika ya Kusini, na kwa sheria za Uingereza! Na isiwe Tanzania, na kwa sheria za kwetu.
 
Back
Top Bottom