Siasa na Vitimbi vya Kombe la Dunia Lilipotua Bongo!!

Coca cola watapenda sana hii picha....
11_09_nztzc7.jpg

-- Is it "Coca Cola FIFA World Cup Finals" as it is in "Barclays Premier League?!"

-- Or, Coca Cola happened to sponsor this event in Tz and along the way coerced our President to put on their branded merchandise for a high profile marketing stunt?

-- Or, was our Honourable Mr. President paid by Coca Cola, as commonly practised in marketing campaigns?

-- Or, is it the case that, Mr. President inadvertently and nonchalantly happened to be in Coca Cola branded outfit that day?!

-- The question is, wouldn't it have been a stately gesture for our President to show support of the tournament in a rather more traditional attire, or something geared toward marketing of Tanzania than how this appears?

-- What would you market as a president at such event given the opportunity?!
 
Tuna kazi kubwa ya kuhakikisha na sisi hatuendelei kuwa watazamaji wa timu za nje.Utakuta asilimia kubwa ya watanzaia wanashabikia vilabu vya Uingereza lakini ukimuuliza hata rais wa TFF hamjui,wakati huohuo anafahamu kikoso chote cha chelsea mpaka mmiliki wake, hii ni aibu kubwa kwa sisi Waafrika kutawaliwa kwa kila nyanja na wazungu.Ipo haja kubwa ya kubadilika na watu kuanza kulipenda soka la kwao.
 
Mr. Kibaki incoercible?!

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=5zGvl8HmoEo[/ame]
 
Sir are you sure? can you bring the evidence down here?

Kama huna ushahidi jamani si vyema kusema mambo ambayo ya aribu image yetu tena ya kiongozi mstaafu wa juu wa nchi.

Lets talk with evidence and its good to realistic in our conversation as a sign of proffessionalism and maturity

Nakumbuka kama Bw Mrema alishtoa ushahidi kuhusiana na pande la dhahabu lililosemekana alipewa Mkapa! Nakumbuka serikali ilihaha sana kwenye hiyo ishu kujaribu kumsafisha mheshimiwa Nkapa!
 
Thursday Nov 19, 2009

11_09_nztzc7.jpg

President Jakaya Kikwte

Huyu jamaa anatakiwa atatue matatizo kebe kebe nchini leo anaenda kuvishwa trucksuit ya wadhamini kwenda kunyanyua kombe linalopita.........

Halafu tunasema tunaviongozi makini, yeah its time he sacked his advisors or promote that January, perhaps he can advise him whats tosh for a president. This being one
 
Sera nzuri za CCM kombe la Dunia latua nchini. Asante mwenyekiti wa CCM na Raisi Kikwete
 
Jamani sasa lawama hizi zimezidi,mnataka asi-socialize kwa vile yeye ni rais? kwani mmeambiwa hana hisia,haruhusiwi kufurahi au kushiriki michezo?.Mwacheni apumue jamani kidogo na yeye.ajifungie tu kila wakati na madocs ya IPTL na dowani si atachanganyikiwa?,mwishowe akianguka mnasema tulikushauri upumzike hukusikia,yani hamna jema.Mbona nyie mnaenda bar kila siku na huko mpirani ndio kabisa.Acheni hizo.
 
Kombe hili kwa Wabongo ni Mwasesere na kamwe haliwezi hata kunyanyua soka letu la kibabaishaji.

Wakenya wao, baada ya timu yao kushindwa kufuzu kombe la Dunia -- tayari wameanza mkakati wa kufaidika -- kwanza wameitisha Breakfast wiki hii -- na kualika wawakilishi wa mataifa 16 kati ya 32 yanayoshiriki katika kombe hilo -- kwenye kikao -- wakiwataka waitumie kenya kwa mazoezi na malazi, wakidai kutoka Nairobi hadi J'burg ni saa 4 kwa ndege na wana shirika la ndege imara ikiwa ni pamoja na Boeing 777.

Sisi naona hapa tunasheherekea mwanasesere na kuzuzuka wote wakiwemo viongozi wetu -- kalagabaho
 
Nasikia mamaa alipoona mmewe kalishika kombe la Dunia nae akapeleka mkono lakini wakuu wakamvuta mkono (kama alivyofanyiwa Raila kule Kenya)...

Hivi hakuarifiwa mapema kuwa linaguswa na mmewe tu?
 
Amezidi kuwa kimbelembele. This could make her come to her senses
 
Nasikia mamaa alipoona mmewe kalishika kombe la Dunia nae akapeleka mkono lakini wakuu wakamvuta mkono (kama alivyofanyiwa Raila kule Kenya)...

Hivi hakuarifiwa mapema kuwa linaguswa na mmewe tu?
wakulaumiwa ni protocol Officers wa Ikulu, kwani wao ndio wanatakiwa kuwaeleza Wakuu, nini cha kufanya na nini si cha kufanya, hasa hasa kama wanasoma magazeti, baada ya tukio la Raila walitakiwa kuanza kujiuliza, kulikoni?

Pili barua ya hao watembezaji kombe la Dunia Inasemaje?

Haya ni matatizo ya kupeana kazi bila muhusika kuwa aidha na wito au taaluma iliyo tukuka katika mambo ya Protokali (protocol)
 
Amezidi kuwa kimbelembele. This could make her come to her senses
Mkuu,

Mama hana kosa, amekumbwa na fedheha hii ya kuvutwa mkono sababu ya wanaohusika na protokali kutompa mwongozo mapema, Raila nadhani alifanya makusudi (kama ukiangalia vema video).
 
Hehehe, mnawalaumu watu wa protokali, vipi kama mama alikuwa mbishi na hakuwasikiliza?
 
Hehehe, mnawalaumu watu wa protokali, vipi kama mama alikuwa mbishi na hakuwasikiliza?

Mkuu mama hana tatizo, ni watu wa protocol!!! suala la protocol halina mjadala kama hutaki unapotezewa!!
 
Kikwete:Tusipobadilika tutakuwa watazamaji milele
kombekikwete.jpg
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na kombe la dunia katika uwanja wa Taifa, baada ya kulipokea kombe hilo mjini Dar es salaam Alhamisi.
broken-heart.jpg
Na Dorice Maliyaga

RAIS Jakaya Kikwete jana alilipokea Kombe la Dunia la fifa na Coca-Cola kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku kuwalaumu wadau wa soka kwa kukwamisha maendeleo ya mchezo hapa nchi.

Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea kombe hili Rais Kikwete alisema kuwasili kwa taji hilo ni jambo la kihistoria, imeleta changamoto kubwa kwenye maendeleo ya michezo hapa nchini.

"Kutwaa Kombe la Dunia ni ndoto ya kila mchezaji na kufika kwa taji hili Tanzania ni bahati ya pekee kwa kutimiza malengo yetu ya soka," alisema.

“Itatuchukua miaka elfu moja kabla yaTanzania kufuzu kwa kombe la Dunia kama tusipobadilika kwenye mfumo wetu wa soka,” alisisitiza rais.

Rais alishutumu shirikisho la soka la Tanzania 'TFF' kwa kushindwa kubaini vigezo vinavyosababisha kuzototesha mchezo huo hapa nchini.

"TFF iachane na tabia ya kutilia mkazo suala la mapato na ushabiki kwenye kupanga ratiba zake kama kweli wanataka kuendeleza soka."
Alisema; ''Kama TFF itaachana na mambo hayo na kutilia suala la ukuzaji wa soka ya vijana kwa kuhakikisha klabu zote zinakuwa na timu za vijana.''

Rais alilipigia vita suala la adhabu zinazotolewa na kamati zake TFF kwani kwa kiasi kubwa zinachangia kuua vipaji vya wachezaji.

"Ni jambo la kushangaza kuona TFF inawafungia wachezaji miezi sita au mitatu si sawa kawaida mchezaji angetakiwa kufungiwa michezo mitatu kama anafanya kosa kubwa."

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa ziara ya kombe hilo kwenye uwanja wa Taifa jijini jana, Kikwete alisema kamwe Tanzania haitoweza kusonga mbele kisoka kama viongozi na wadau wote wa soka wasipokubali kubadilika.

Alisema ni lazima kufanywe jitahada za makusudi ya kujenga shule za soka kwa vijana na kuachana na tabia ya kusajili wachezaji hao wazee ambao watacheza kwa msimu amoja na mwingine huachwa kutokana na umri wake.

''Watafutwe walimu wengi wa michezo kwenye mashule, vijijini mitaani na sehemu zote ili kuwapa nafasi na kuutambulisha mchezo huo kwa wingi.''

Alisema ujio wa kombe hilo ni deni kwa Taifa kuhakikisha wanaongeza bidii na kuacha kuwa watazamaji kila siku.

Hata hivyo Kikwete alizitaka klabu kuachana na tabia ya kuwa na malumbano ya kila kukicha kwani ni moja ya sababu ya kudidimiza soka kwa kuwa zenyewe ndiyo mizizi ya fitina.

Alisema ili kuuendeleza mchezo huo lazima kupata walimu wenye uzoefu na hodari wa mpira na kuwaepuka wachambuzi wa soka uchwala ambao wao kazi yao kila siku kusubili makosa ilikukosoa.

"Tuwasikia wakisema kocha hafai kwanini asingemtumia mchezaji furani wakati hawana wanalojua."

Rais alisifu uteuzi wa vijana kwenye timu taifa ya Tanzania kwani unasaidia kuibua vipaji vipya ambao wataweza kusaidia nchi siku za usoni.

Kombe hilo liliwasili nchini majira ya saa 10:30 jioni na kupokelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendela kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa.

Kombe hilo lilopo kwenye safari ya kuelekea Afrika Kusini ilikuwa hapa nchini kwa siku mbili, leo walitakuwa visiwani Zanzibar na kesho Jumamosi ilitakuwa uwanja wa Taifa na kushudia na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa soka hapa nchini. Watu waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege walibaki wakiduwa wasijue nini kinaendelea baada ya ndege kuwasili, na kushitukia tayari limeshangia kwenye magari maalumu yalioandaliwa na msafara kuanza ukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Helkopta.
 
Back
Top Bottom