BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 2,712
- 6,515
Kule Moshi kuna shule moja ni ya kanisa sitaitaja jina ni zile shule zina mashariti lukuki ikiwemo kwamba kumuona mtoto ni hadi Visiting day.
Sasa kuna Jamaa alikuwa na mtoto anasoma kwenye hio shule jamaa yeye anaishi Dar ila ni mtu wa safari nje ya nchi sana kiasi kwamba anapishanaga na mtoto wake anaye soma Moshi.
Mtoto akiwa likizo Baba hayupo na Baba akirudi mtoto walisha fungua, hivyo ilikuwa ni anaweza kata mwaka hajaoanana na mtoto wake kwa sababu ya safari na kupishana.
Siku moja akawa na safari Arusha, sasa akaona hii pia ni nafasi pekee ya kumuona mtoto wake make hawajaonana mwaka.
Alivyofika shuleni alikutana na kizingiti cha mlinzi akimwambia huwezi onana na mtoto hadi siku ya Visiting Day, jamaa kakomaa kwamba ni lazima aonene na mtoto wake kwa sababu hajaonana naye mwaka mzima na hakuna namna anaweza ondoka bila kumuona.
Uongozi ukashikilia msimamo kwamba jamaa hawezi kamwe kumuona mtoto na huo ndio msimamo wa shule na hauwezi badilishwa kamwe.
Jamaa kaona isiwe tabu akauliza mnanidai? Yaani kuna ada yoyote nadaiwa? Uongozi ukasema hapana hudaiwi.
Okay nipeni mtoto wangu na kila kilicho chake niondoke naye, Uongozi ukadhania ni utani kumbe ndio jamaa anamanisha, sasa msimo ulibadilika kutoka kumuona na sasa ni anaondoka naye mazima, ilibidi kweli mtoto atolewe na jamaa akasepa naye na kwenda kumtafutia shule nyingine isio kuwa na ujinga kama huo.
Jamaa msimamo wake ilikuwa yule ni mtotot wake hajaonana naye mwaka na hakuna namna amaweza ondoka Moshi bila kumuona.
Ila ukiangalia jamaa alikuwa sahihi yeye ndie mwenye mtoto, ndie anaye lipa ada haiwezekani hujaonana na mtoto. Wako miaka bado ufike getini uambiwe hairuhusiwi kumuona.