Shule ya Kiteto Kuitwa J. Kikwete Ni sawa?

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Nimeona Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara
aliwaambia wananchi wa Kiteto waite Shule ya Sekondari ya Laalakir iliyojengwa kwa msaada wa Wachina iitwe Shule ya Sekondari ya JK.

Sioni haja ya kuita shule kwa majina ya marais. Itakuwaje kama kila Wilaya itaipa shule
jina la Rais. Si tatkuwa na shule zenye majina yanayofanana ni bora majina ya asili ama
majina ya watu muhimu katika jamii ile yatumike.
 
Kwani asingeipa hiyo shule jina lake yeye mwenyewe! Kila wakati wanafikiria kumpendeza bwana mkubwa na kuimba sifa zake feki!
 
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizo na viongozi WANAFIKI waliopitiliza. Sababu ni kwamba hata wao wenyewe hawaamini kwamba wanasifa za kupewa nafasi walizonazo kwakua ajuaye sifa za kiongozi ni bwana mkubwa anayewateua. Kuna wanaofikiri wamepewa uongozi kwa kuwa "wanamchekesha sana bwana mkubwa" kuna wale wanaofikiria wamepewa nafasi kwa sababu ni "wazuri wa sura" na mengineyo. Hivi kiongozi wa namna hii ataachaje kufanya mambo ya Kinafiki kama hayo ya kutoa majina ya aliyemteua kwenye majengo na madaraja?
 
....huu ni ukosefu wa fikra....nakumbuka kuna kipindi mkoa fulani waliamua kuipataia majina mitaa......jina la Benjami Mkapa lilijitokeza karibu kila kata kama sio kitongoji............next move.....Halmashauri waliagiza kufuta majina mapya yote. Hii naiona katika Elimu....kuna majina yanajirudia mpaka mtu unakosa muelekeo. mfano matumizi ya jina la baba wa Taifa, Mkapa, Sumaye na Mwenge kuna shule zaidi ya 1. Natumai watarekebisha hili, vinginevyo historia hapo baadae itashindwa kuandikika au udanganyifu utakuwa rahisi kufanyika kupitia majina haya.
 
ni sawa lakini watatoka vilaza wa kufa mtu hapo
si unaona tanzania tulikofikia
na maneno yanaumba wewe wahache waiteite tu majina
 
nimeona mkuu wa mkoa wa singida ambaye pia ni kaimu mkuu wa mkoa wa manyara
aliwaambia wananchi wa kiteto waite shule ya sekondari ya laalakir iliyojengwa kwa msaada wa wachina iitwe shule ya sekondari ya jk.

Sioni haja ya kuita shule kwa majina ya marais. Itakuwaje kama kila wilaya itaipa shule
jina la rais. Si tatkuwa na shule zenye majina yanayofanana ni bora majina ya asili ama
majina ya watu muhimu katika jamii ile yatumike.
watu muhimu katika jamii kikwete ni miongoni mwao. Wewe unaishi nchi gani vile. Au unachunga min'gombe huko porini?
 
Back
Top Bottom