Shinyanga: Lugha yasababisha Mahakama kuamuru kesi ya aliyehukumiwa kunyongwa isikilizwe tena

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Mahakama ya Rufani Kanda ya Shinyanga, imeamuru kesi ya mauaji inayomkabili, Juma Ndodi, aliyehukumiwa kunyongwa, ianze kusikilizwa upya kwa sababu hoja za awali na maelezo ya mashahidi yalisomwa kwa Lugha ya Kiswahili wakati yeye anaelewa Kisukuma.

Uamuzi huo ulitolewa juzi mbele ya jopo la majaji watatu, Jaji Augustine Mwarija, Ignas Kitusi na Agnes Mgeyekwa waliosikiliza rufani iliyowasilishwa na Ndodi akipinga hatia na adhabu ya kunyongwa hadi kufa aliyopewa na Mahakama Kuu.

Jopo hilo katika uamuzi wao, walikubaliana na hoja za mawakili wa pande zote mbili kuwa mrufani alikuwa na haki kuelewa shtaka na aina ya ushahidi atakaokutana nao wakati wa usikilizwaji kesi.

"Mrufani hakuwa anaelewa lugha iliyotumiwa na mahaka-ma, hakuna ubishi kwamba alinvimwa haki yake na hivyo hawawezi kusema kuwa mlolongo wa usomwaii wa maele-zo ya mashahidi ulifanvika kwa usahihi," lilisema jopo.

Mahakama ilibainisha kwamba, mahakama ya chini haikutoa mkalimani kwa mrufani hali ambayo imemnyima haki va kujua aina ya shtaka linalomkabili na ushahidi ambao upande wa mashtaka unatarajia kuutumia kwa maana hiyo mlolongo huo ulikuwa na dosari. "Kwa dosari zilizojitokeza tunabatilisha mlolongo wa usomwaji wa maelezo ya mashahidi wa mahakama ya chini na Mahakama Kuu, tunafuta hatia na hukumu ya Mahakama Kuu.

"Kwa minajili ya maslahi ya haki, Mahakama inaamuru kesi hivo isikilizwe upya kuanzia hatua ya kusomwa maelezo ya mashahidi na awepo mkalimani, mrufani abaki mahabusu," lilisema jopo hilo.

Katika kesi hiyo, ilidaiwa Februari 27, 2015, Kijji cha Buyange Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga alimuua
Modester Kilijiwa.

Alisomewa shtaka lake katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama Machi 12, 2015, bila kuwapo mkalimani na Februari 3, 2016 kesi hivo ilianza kusikilizwa Mahakama Kuu Shinyanga bila mkalimani huku yeye akiwa anaelewa lugha ya Kisu-**** pekee.
 
Alisomewa shtaka lake katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama Machi 12, 2015, bila kuwapo mkalimani na Februari 3, 2016 kesi hivo ilianza kusikilizwa Mahakama Kuu Shinyanga bila mkalimani huku yeye akiwa anaelewa lugha ya Kisu-**** pekee
Itakuwa taabu sana kama Jf wataweka systematic ban ya maneno kama walivyofanya kwa neno fu***k.

Kiswahili n kigumu mno kuwekea mfumo.

Anyway ungeandika tu neno lote maana kitu kuwa tusi inategemea na nia ya mtukanaji
 
Wasukuma wengine wanaamini kila mtu anajua Kisukuma :D :D

Nina jamaa yangu msukuma yeye alipovuna mpunga akanieleza anatafuta visa ya kwenda dubai hivo ataenda migiresheni kama kesho, nikawa namweleza hapo migiresheni akatafute passport, halafu visa ataitafuta ubalozini hasa kama nchi ina vigezo ya visa kabla ya kufika au baada ya kufika, akaanza ubishi kua Rafiki yao Doto madukwa mwaka jana alienda dubai eti aliwaambia alikata tigeti ya basi akatumia siku tatu hadi nne kufika dubai, nikasema sawa muulize doto atakufahamisha hiyo dubai ya kwenda kwa basi,
Pamoja na yote wasukuma ni watu wenye upendo sana na wakarimu mno lakini kubwa ni wachapakazi wakubwa sana ,
 
Mahakama ya Rufani Kanda ya Shinyanga, imeamuru kesi ya mauaji inayomkabili, Juma Ndodi, aliyehukumiwa kunyongwa, ianze kusikilizwa upya kwa sababu hoja za awali na maelezo ya mashahidi yalisomwa kwa Lugha ya Kiswahili wakati yeye anaelewa Kisukuma.

Kuu Shinyanga bila mkalimani huku yeye akiwa anaelewa lugha ya Kisu-**** pekee.
Kama anajua Kisukumaaa tu alijuaje kuwa kahukumiwa Kunyongwa ?
 
Back
Top Bottom