Shikamoo "Muajemi"; Umeguswa, Umenuka!

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,921
15,613
Iran imeandika historia mpya Ulimwenguni kwa kufanya shambulizi la kipekee ambalo halijawahi kushuhudiwa toka dunia iumbwe.

Shambulizi lile litaendelea kutumika ktk mafunzo ya vyuo vya kijeshi vya nchi za Ulimwengu wa kwanza.

Kwa hakika safari hii Iran imetoa salamu za kipekee si kwa Israel tu bali kwa Marekani, Uingereza, Ufaransa na vifaranga vyao vyotee.

Salamu hizo zimezifika vema nchi zote za mashariki ya kati ambazo kamwe hakuna atakaejaribu kufanya ujinga wowote (kutoa anga au ardhi kwa adui) wa kuomba kupelekewa bando la moto wa droni na makombora 300 kwa mpigo.

Pamoja na mkwara mzito wa Biden kuwa Iran akiishambulia Israel, Biden nae atajibu mashambulizi...lakini wanaume wametimiza ahadi ya kushambulia tena shambulio la kihistoria ambalo halijawahi shuhudiwa popote kwenye Ulimwengu huu. Biden kausoma mchezo, kamkanya kijana wake BN kuwa asijibu chochote, kama haikutosha nae Biden katia mpira kwapani!

Btw: Usitegemee kusikia tena Israel karusha jiwe kwenye ardhi (ubalozi) ya Muajemi...hata kwa bahati mbaya
 
IMG_20240414_213609.jpg

😄😀😄
 
Nasikia alifanya kwanza shambulio la kimtandao, ukanda wote ukawa unaona namba namba tu, hadi safari za ndege zikasitishwa
Mkuu ni noma na nusu, imagine umekaa area D pale royal ya Dodoma unatizama juu unaona anga limetapakaa silaha za kivita, ila unaambiwa tulia hazikuhusu hizo zinaelekea Msumbiji, wewe unakunhwa beer msumbiji wanakimbizana na hicho kinachowakimbiza komepita juu yako pasipo madhala tena toka nchi ya mbali zaidi zaidi....nimependa hii....🤪 🤪 🤪
 
Kusema kweli shambulizi hili litakuwa ni moja ya module kwenye course za kijeshi za nchi nyingi tu, na emphasis ya Wakufunzi hao wa kijeshi itakuwa ni "Ni failure ya hali ya juu kurusha missiles takribani 300 kwa adui yako na zote zikasambaratishwa angani kabla hazijafikia targets, ni ujinga wa hali ya juu, na ni jambo la kuonea aibu badala ya kujisifu".
 
Ila kwa kweli Irani jana kaonesha kitu amaizing, hajaomba kutumia nchi za jirani kufanya kazi yake, hizo nchi zilishuhudia tu anga inapitishwa silaha kuelekea nchi nyingine. Package ya kitu 300 sio mchezo
Je yamefanikiwa kuleta madhara au damage imekuwa ndogo kuliko matarajio?
 
Kusema kweli shambulizi hili litakuwa ni moja ya module kwenye course za kijeshi za nchi nyingi tu, na emphasis ya Wakufunzi hao wa kijeshi itakuwa "Ni failure ya hali ya juu kurusha missiles takribani 300 kwa adui yako na zote zikasambaratishwa angani kabla hazijafikia targets, ni ujinga wa hali ya juu, na ni jambo la kuonea aibu badala ya kujisifu".



Taratib videos zinaanza fichuka
 
Back
Top Bottom