Andrew Nyerere
JF-Expert Member
- Nov 10, 2008
- 3,007
- 2,429
Andrew alikuwa anahangaika sana na kazi ya kurekebisha matatizo yaliyokuwa yanatokea mara kwa mara kutokana na kutoelewana na kutokubaliana kati ya wafuasi wa Yohana na wafuasi wapya wa Yesu. Matatizo makubwa yalitokea kila baada ya siku chache,lakini Andrew,kwa kushirikiana na wenzake mitume,alifanikiwa kuwafanya wanaogombana wafikie muafaka fulani,hata kama wa muda tu.Yesu alikataa kushiriki katika hivi vikao,wala hakutoa ushauri jinsi ya kutanzua. Hata mara moja hakutoa mapendekezo kwa mitume jinsi ya kuyatanzua haya matatizo magumu.Andrew alipokuja kwa Yesu,na haya matatizo,alisema kila mara,''Si jambo la busara kwa mwenyeji kushiriki katika matatizo ya familia ya wageni wake;mzazi mwenye hekima hachukui upande katika magomvi madogo madogo ya watoto wake mwenyewe.''
Walipokuwa Amathus,Thomas alimuuliza Yesu,''Ni nani huyu Mungu wa ufalme?''Yesu akajibu,''Mungu ni Baba yako ,na dini-injili yangu-siyo kitu chochote zaidi ya kuamini na kutambua ukweli kwamba wewe ni mtoto wake.Na mimi nipo hapa katika mwili kuyaweka wazi haya mawazo katika maisha yangu na mafundisho yangu.''
Pia walipokuwa Amathus walijadili kuhusu umoja wa kiroho. James Zebedee aliuliza,''Bwana,tunawezaje kuwa na mtazamo mmoja ili tuweze kuishi kwa muafaka zaidi? '' Yesu aliposikia hili swali alisisimka sana rohoni mwake,kiasi kwamba alijibu,''James,James,lini nimewafundisha kwamba wote mnapaswa kuwa na mtazamo mmoja?Nimekuja duniani kutangaza uhuru wa roho ili watu wote wawe na uwezo wa kuishi maisha ya uhuru na kipekee[originality]mbele ya Mungu.Sitaki muafaka wa kijamii na undugu wa amani ununuliwe kwa kutoa sadaka[sacrifice of ]nafsi ambayo ni uhuru na roho ya kipekee[spiritual originality]. Ninachotaka kutoka kwenu ,wafuasi wangu,ni umoja wa kiroho-na ili muwe na furaha kwa kujitoa kwa pamoja na kwa moyo wote kufanya utashi wa Baba yangu mbinguni. Siyo lazima wote muone,au muhisi au mfikiri sawa sawa,ili kufanana kiroho.
''Umoja wa kiroho unatokana na kuelewa kwamba kila mmoja anakaliwa ndani yake,na anatawaliwa zaidi na zaidi,na zawadi ya roho ya Baba wa mbinguni.Muafaka wenu utokane na kuelewa kwamba matumaini ya roho ya kila mmoja wenu yanafanana katika chanzo chake,maumbile yake,na hatima yake[origin,nature and destiny].
Kwa njia hii mnaweza kuwa na umoja uliokamilika wa nia ya kiroho na ufahamu wa kiroho,baada ya kuelewa kwamba katika kila mmoja wenu ipo roho kutoka Paradiso;na mnaweza kuwa na huu umoja wa kiroho ingawa,mnatofautiana; katika kufikiri kwenu,hisia zenu na tabia za kijamii.Nafsi zenu zinaweza kuwa tofauti,lakini katika asili zenu za kiroho na matunda yenu ya kiroho,ya ibada takatifu na upendo wa kindugu, mnaweza kuwa wamoja kiasi kwamba wote wanaotazama maisha yenu kwa hakika wataona asili ya kiroho na umoja wa kiroho;wataelewa kwamba mlikuwa na mimi,na mmejifunza,tena mmejifunza vyema,jinsi ya kufanya utashi wa Baba wa mbinguni,mnaweza kuwa na umoja katika utumishi hata mnapofanya huo utumishi kwa njia zenu;uwezo wenu wa kipekee wa akili,mwili na roho.
''Umoja wenu wa kiroho una maana mbili;kwanza,wote mna lengo la pamoja la kutaka kutumikia,wote mnataka kufanya utashi wa Baba aliye mbinguni. Pili,wote mna wazo moja kuhusu lengo la kuishi,mnataka kumtafuta Baba mbinguni ili muweze kuthibitisha kwa mbingu[Universe]kwamba mmekuwa kama yeye.''
Walipokuwa Amathus,Simon Zelote,akamleta Mshirazi mmoja,Teherma,kufundishwa na Yesu.
Baadaye Simon na Yesu walipokuwa peke yao,Simon akamuuliza Yesu,''Bwana,kwa nini mimi nilishindwa kumshawishi? Kwa nini alinipinga,lakini alikusikiliza wewe?''Yesu akajibu,''Simon,Simon,mara ngapi nimekueleza uache kutoa kutoka katika mioyo ya watu wanaotafuta wokovu. Mara ngapi nimekuambia ufanye tu kazi ya kuweka vitu ndani ya roho zenye njaa. Waongoze watu kwenye ufalme,na kweli zilizo hai za ufalme zitaondoa makosa yote makubwa. Ukimwambia mtu kwamba Mungu ni Baba yake,itakuwa rahisi kumwambia kwamba yeye ni mtoto wa Mungu. Na ukifanya hivyo utakuwa umeleta taa ya wokovu kwa mtu aliyekuwa amekaa katika giza.Simon,Mwana wa Mtu alikuja anaishamblia sheria ya Mose na Manabii na kutangaza maisha mazuri na mapya?Hapana.Sikuja kuondoa kile mlichopewa na wahenga isipokuwa kuwaonyesha njia iliyokamilika ambayo baba zenu waliiona kwa kiasi tu. Kwa hiyo,nenda,Simon,kuufundisha na kuuhubiri ufalme,na ukimweka mtu kwa usalama na kwa uhakika ndani ya ufalme,,huo,ndio wakati,kama huyo atakuja na maswali,kumpa maagizo ya jinsi ya kupata maendeleo ya roho,hatua kwa hatua,katika ufalme.''
Simon alishangazwa na haya maneno,lakini alifanya kama Yesu alivyoagiza,na,Teherma,yule Mshirazi,akahesabika miongoni mwa wale walioingia katika ufalme.
Usiku ule,Yesu aliongea na mitume kuhusu maisha mapya katika ufalme.Pamoja na maneno mengine alisema,''Unapoingia katika ufalme,unazaliwa upya. Huwezi kufundisha mambo ya kina ya kiroho kwa wale ambao wamezaliwa katika mwili;hakikisha kwanza watu wanazaliwa katika roho kabla ya kuanza kuwafundisha mambo ya juu ya kiroho. Usijaribu kuwaonyesha watu maajabu ya Hekalu kabla hujawaingiza katika Hekalu. Watambulishe watu kwa Mungu na kama watoto wa Mungu kabla ya kuanza kuwafundisha kwamba Mungu ni Baba yao na wao ni watoto wake.Usigombane na watu. Huu sio ufalme wako,wewe ni balozi tu,wewe fundisha tu;'Huu ni ufalme wa mbinguni-Mungu ni Baba yako na wewe ni mtoto wake na hii habari nzuri,ukiiamini kwa moyo wote,ndio wokovu wako wa milele.''
Mitume walipata maendeleo sana walipokuwa Amathus. Lakini hawakupendezwa jinsi ambavyo Yesu hakutoa mapendekezo juu ya jinsi ya kuwashughulikia wafuasi wa Yohana. Hata katika jambo muhimu la ubatizo,Yesu hakusema lolote zaidi tu alisema,''Yohana aliwabatiza kwa maji,lakini ukiingia katika ufalme wa Mungu utabatizwa kwa Roho.''