Sheria mpya ya uwekezaji Zanzibar ni bora Afrika

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema sheria mpya ya uwekezaji ya mwaka 2023 itakuwa bora Afrika ambayo ataisaini hivi karibuni baada ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi Mwezi Novemba Mwaka jana.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipoweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Hoteli ya nyota tano ya Zanzibar Crown Mazizini, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 07 Januari, 2024.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza wawekezaji wa hoteli hiyo kwa kuwekeza dola za kimarekani Milioni 30 kwa mradi wa hoteli ambapo utatoa fursa ya ajira ya Wazanzibari zaidi ya 200.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa lengo la Serikali ifikapo mwaka 2025 kupokea watalii milioni moja ambapo sasa Zanzibar inapokea watalii laki tano na elfu sitini kwa mwaka.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amesema Zanzibar inaongoza kupokea ndege nyingi Tanzania kwa sasa ukilinganisha na viwanja vya ndege vya Kilimanjaro na Dar es Salaam .

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza wawekezaji hao kwa uamuzi wa ujenzi wa soko la kisasa la wavuvi na Msikiti pembezoni mwa hoteli hiyo.
IMG-20240107-WA0048.jpg
View attachment 2864543
IMG-20240107-WA0050.jpg
IMG-20240107-WA0051.jpg
IMG-20240107-WA0052.jpg
IMG-20240107-WA0047.jpg
IMG-20240107-WA0046.jpg
IMG-20240107-WA0045.jpg
IMG-20240107-WA0043.jpg
IMG-20240107-WA0044.jpg
IMG-20240107-WA0042.jpg
IMG-20240107-WA0041.jpg
IMG-20240107-WA0040.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom