Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Mimi sio mwanasheria na pia naomba kujua sheria inachukua mkondo gani endapo mtu anawaita watu na mbele ya makamera jamii au ulimwengu wote wakamsikia akidai atajiua? hii ni mujibu wa sheria zetu hapa kwetu Tanzania! mfano mojawapo ni huu hapo jana TBC1 kutuonyesha live bila chenga bwana Abdalah Zombe kuuambia uma wa watanzania kua chama cha chadema kikichukua madaraka basi atajitoa kafara kwakujinyonga Je kama basi indendapo chama hiki cha demokrasia na maendeleo endapo kitapata ridhaa ya kuongoza nchi huyu bwana atachukuliwa hatua gani kwa mujibu wa sheria? Naomba kuwasilisha