Ndugu wana JF,sherehe ya jana mmejifunza kitu gani?
Mosi,nimejifunza kupasua yale matofali membamba ya kuchoma kwa kutumia ngumi kama wale askari walivyoonyesha pale uwanjani,
Pili, nimejifunza na kugundua kuwa jeshi letu linatumia vibaya nguvu waliyonayo dhidi ya raia hususani baada ya kuona lile igizo la waandamanaji kukamatishwa mbwa waliloigiza askari wale mbele ya umma.
Tatu, nimejifunza kuwa rais anaweza kukagua gwaride la jeshi lake akiwa na bodyguards wake wawili ambao sio wanajeshi tena waliovalia style ya 'men in black'.