Sherehe ya harusi yavunjika baada ya kugundulika bwana harusi ameoa na ana watoto saba

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
‘Hivi ni vijimambo’ unaweza ukaita hivyo, baada ya sintofahamu kutanda katikati ya sherehe ya harusi kutokana na vurugu iliyosababishwa na taarifa iliyomfikia bi harusi kuwa anayefunga nae ndoa ana familia yenye watoto saba.

Sherehe hiyo iliyokuwa ikifanyika siku ya Jumapili katika jimbo la Edo kusini mwa Nigeria iligeuka shubiri ambapo vilio vilitawala upande wa bibi harusi anayesemekana hakufanya uchunguzi kamili kumgundua mwenza wake huyo kabla ya kujitosa kufunga nae pingu za maisha.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha eneo la tukio kuvurugika baada ya viti, maua na mapambo yakiwa yametupwa kila mahali huku waalikwa wakiwa wamesimama kwa mshangao wakiashiria hakuna tena kinachoendelea.

TAZAMA VIDEO CHINI HAPA

 
.
IMG-20230317-WA0006.jpg
 
Back
Top Bottom