Shemeji yangu huyu ananitega!

SnowBall nafikiri we are too old kwa mambo kama haya
May be tuko sayari tofauti
Maana sijaona ambacho kimemfanya mpaka amuone shemeji yake anamtega
kupigiwa magoti
na huyo mke ambaye anamuacha mdofo wake kuingia kwenye chumba chao na kutandika kitanda ni wa wapi na anaacha hata kumuandalia mumewe chai na chakula anampa hilo jukumu mdogo wake

Hapa kuna mambo mawili katika tabia za mleta bandiko. 1) Tamaa kwa wanawake bila mipaka, sidhani anaona mpaka wowote kati ya mkewe a shemejiye. Anachofikiri ni "trophies" na anadhani shemejiye ni another trophy to win!! katika bandiko lake, hakuna sehemu inaonesha ametegwaje. 2. Kukosa uongozi katika nyumba yake mwenyewe. Kila jambo lina mipaka. Shemeji kukupelekea maji bafuni si jambo baya lakini katika jamii inayotuzuguka, limekabidhiwa sana kwa wake. Ukijua mke hayuko, kuepusha balaa - jipelekee mwenyewe. Vitu kama miswaki anaweza kufanya mwenyewe. Kutandika kitanda si sawa!!! Na huyu bwana anavoshangilia jambo hili anaonesha uelewa mdogo wa majukumu na mgawanyo wake. Ikiwa yeye mwenyewe hawezi kutandika kitanda, akiache hivo mpaka mke atapokuja jioni. Sidhani mke atamlaumu mdogowe kwa kutokitandika.

Damn!!!
 
Nadhani wewe ni mrafi sana! Una mawazo ya kingono ngono na mwisho wa siku uta mbaka shemeji yako na utaumbuka. Huyo anakuheshimu sana na anayafanya hayo kwa mapenzi mema tu. Acha ugube gube wewe.
 
we bata kweli mtu anakuheshimu unasema anakutega asipokuheshimu unasema anakiburi wee vipi
 
Hivi unaogea bafu gani vile hadi unapelekewa mswaki? By the way, kama we ni mfanyabiashara na hujaweza hata kuwa na nyumba yenye masterbedroom then concentrate na biashara kwanza! Ukiwa na room ambayo ni self contained hizo biashara zakubebewa mswaki hazitakuwepo na utamuona shemejio sawa na dada zako tu!
 
Tamaa tu inakusumbua huna lolote! Wanaume wengine bwana mkiheshimiwa mnatamani, msipoheshimiwa maneno, mwataka nini haswa?
Na huyo shemeji shule anaenda saa ngapi? Usiku? Huo muda wa kukuhudumia asubuhi anatoa wapi?
 
Mh, mbona kama manyoya mengi dude?! hajaliwa kweli huyuuuuuuuuuuu
kama anatoka kanda ya ziwa, hiyo migoti ni mila na desturi tu mtu wangu haisignify upendo mapenzi wala heshima, ni utamaduni tu wa kupiga magoti unapoongea au kumkaribisha hasa mwanaume. kwao hata kama anegkuwa ni mdogo kiumri, lakini so long as ni mwanaume goti mtindo mmoja
teh teh teh!! kula tu dude siyo haramu sana ingawa ni kosa
 
kama kwetu kule kasikazini nijambo la kawaida sana kwa mwanamke kupiga magoti naweza kusema ni asili yetu kufanya hivyo kwa kila jambo hasa kuwafanyia wakubwa wako
 
Mimi naishi na mke wangu na tumejaaliwa kupata watoto wawili. Shemeji yangu baada yakumaliza shule, kaja kuishi nasi nyumbani kwangu, nimemtafutia chuo na anasoma nakurudi nyumbani, lakini maisha yake yamenifanya nizidishe upendo kwake. Kwakuwa mke wangu nimfanyakazi huwa sanyingine anaondoka mapema nakuniacha mimi, mimi ni mfanyabiashara na huwa nasafiri maramojamoja mikoani hivyo nirudipo nyumbani toka mikoani nabaada ya kusambaza biashara zangu, muda mwingi huwa nachelewa kutoka nyumbani na saanyingine nakuwepo tu nyumbani kwaajili yakupumzika jioni ndo huwa natoka. Sasa shemeji yangu huwa ananisalimia kwakupiga magoti mpaka chini na kama hiyo haitoshi hunipelekea sabuni na mswaki aliouwekea dawa ya mswaki, kama hiyo haitoshi hurudi tena nakuniita kwa sauti ya upole, shemeji nenda kaoge tena akiwa amepiga magoti! Baada yakutoka kuoga nikiingia chumbani nakuta kitanda kimetandikwa kwa umaridadi na ameniandalia nguo ambazo nitavaa iwapo kama nitatoka, nakuta chai imeshatengwa mezani nakaribishwa kwakupigiwa magoti. Nanawishwa mikono kwa maji ya moto, chakula kinaombewa halafu nakaribishwa kwa sauti nzuri, yaani mmh! shemeji huyu tabia yake inanifanya nampenda zaidi ya sana kwakweli. Mbaya zaidi ni mrembo navutiwa nae hadi napitiliza, kwani ananionyesha upendo ambao hata mke wangu huwa hanionyeshi na sijawahi kuupata. Nampenda sana shemeji yangu, ila tu najilinda nisifanye dhambi ya kumtamani naku do nae!

Ndugu yangu hakuna chochote kigeni hapo!kitu kinachokusumbua ni "TAMAA" mara nyingi ukizoea chakula cha aina fulani mwishowe hukinai na kutaka kuonja kingine.ila jua hakuna cha zaidi hata hicho pia utakinai.Ridhika na uliye naye huyo unayemmezea mate hana cha zaidi na matokeo yake ni kukuweka matatani na majuto hapo baadae na kuyumbisha ndoa yako pindi mke anapogundua.
 
Hebu minya hiyo dushele akili zirudi kichwani,maana nahisi ziko njiani kuelekea kwenye dushelele

Mimi naishi na mke wangu na tumejaaliwa kupata watoto wawili. Shemeji yangu baada yakumaliza shule, kaja kuishi nasi nyumbani kwangu, nimemtafutia chuo na anasoma nakurudi nyumbani, lakini maisha yake yamenifanya nizidishe upendo kwake. Kwakuwa mke wangu nimfanyakazi huwa sanyingine anaondoka mapema nakuniacha mimi, mimi ni mfanyabiashara na huwa nasafiri maramojamoja mikoani hivyo nirudipo nyumbani toka mikoani nabaada ya kusambaza biashara zangu, muda mwingi huwa nachelewa kutoka nyumbani na saanyingine nakuwepo tu nyumbani kwaajili yakupumzika jioni ndo huwa natoka. Sasa shemeji yangu huwa ananisalimia kwakupiga magoti mpaka chini na kama hiyo haitoshi hunipelekea sabuni na mswaki aliouwekea dawa ya mswaki, kama hiyo haitoshi hurudi tena nakuniita kwa sauti ya upole, shemeji nenda kaoge tena akiwa amepiga magoti! Baada yakutoka kuoga nikiingia chumbani nakuta kitanda kimetandikwa kwa umaridadi na ameniandalia nguo ambazo nitavaa iwapo kama nitatoka, nakuta chai imeshatengwa mezani nakaribishwa kwakupigiwa magoti. Nanawishwa mikono kwa maji ya moto, chakula kinaombewa halafu nakaribishwa kwa sauti nzuri, yaani mmh! shemeji huyu tabia yake inanifanya nampenda zaidi ya sana kwakweli. Mbaya zaidi ni mrembo navutiwa nae hadi napitiliza, kwani ananionyesha upendo ambao hata mke wangu huwa hanionyeshi na sijawahi kuupata. Nampenda sana shemeji yangu, ila tu najilinda nisifanye dhambi ya kumtamani naku do nae!
 
Aisee hongera kwa kupata shemeji mzuri, mwenye heshima na mkarimu kiasi hicho. Lakini kipi cha ajabu hapo...kukupigia magoti? kuna makabila jinsia ya kike kuchuchumaa mbele ya mwananume ni tamaduni, nadhani ni vyama nawe ukaendelea kumpatia heshima yake kama shemeji na wala usifikirie vinginevyo kwani kwa kumuwazia vinginevyo unampa nafasi ibilisi akupelekee kudo.
Nadhani ni jukumu lake kukuheshimu kama shem na wewe umheshimu kama shem vile vile. Ila hii ya kutandikiwa kitanda na maji ya kuoga lol! Vyema akaacha haraka sna kwani naiona hatari iliyoko mbeleni.

Ndo hayo tu...Mungu ailinde na kuibariki ndoa yako!

Barikiwa sna.
 
unapaswa umfukuze mara moja kama unataka ndoa yako iendelee. Kwa jambo hili usiwe na huruma hata chembe. Muonyeshe mkeo hatari ya kuishi na mdogo wake.
 
Mie sina tatizo na mambo mengine kama 'kupigiwa magoti', 'kuwekewa sabuni bafuni' na kadhalika. Tatizo KUBWA nilionalo ni VIPI shemejio aingie CHUMBA CHAKO na kukutayarishia nguo za kuvaa weweeeeeee?
 
Back
Top Bottom