Sheikh wa Mkoa wa Manyara: Mwenyezi Mungu amlinde Rais Samia, anatupigania

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Sheikh wa Mkoa wa Manyara amkaribisha Rais Samia mkoani humo kwa kueleza furaha waliyonayo Rais Samia kuwa Mkoani hapo na kutoa rai kwa wananchi kumuunga mkono katika yote kwani amefanya mengi kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani

"Tunayo furaha kubwa sana Rais Samia kuja Manyara, tunamuomba Mwenyezi amhifadhi na ampe afya njema ili azidi kutupigania" alisema Sheikh Mohamed H. Kadidi

Sambamba na hilo, Sheikh wa Mkoa wa Manyara amempongeza Rais Samia kwa kwa kuishi ndoto za Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na uzalendo wake kwa Taifa letu
 
Uzi umewekwa kwenye siasa. Wakati viongozi wanasema viongozi wa dini wanachanganya dini na siasa .
Ukisifiwa sio siasa ila ukiuliza unaleta siasa.

Bangonza kichwa sana
 
Sheikh wa Mkoa wa Manyara amkaribisha Rais Samia mkoani humo kwa kueleza furaha waliyonayo Rais Samia kuwa Mkoani hapo na kutoa rai kwa wananchi kumuunga mkono katika yote kwani amefanya mengi kwa kipindi kifupi alichokaa madarakan...
Wakitoka hapo wanapewa bahasha ya kaki
 
Tunakoelekea kuna siku tutasikia kiongozi wa dini amesema "tunamshukuru mheshimiwa kwa kupendelea kuvaa ushungi ambao ni mfano bora kwa vijana kuacha kuvaa mawigi"
 
Pia alimshukuru Rais Samia kwa kuwaonesha Kibla ilipo na hata sasa kila waswalipo huelekea huko
 
Huyu shekhe ni mnafiki sana. Samia anatupigania kwa kipi wakati ameuza bandari yetu kwa waarabu?
 
Back
Top Bottom