Shehena kubwa ya almasi yazuiwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Shehena kubwa ya almasi yazuiwa

Ni ya mgodi wa Williamson, Shinyanga

Kisa ni hali tete ya kuuzwa kwa mgodi

Mwandishi Wetu Machi 25, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

SHEHENA ya almasi inayotajwa kuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 4.5 (zaidi ya Sh bilioni 4.5) iliyopo katika Mgodi wa Almasi wa Wiliamson, uliopo eneo la Maganzo, mkoani Shinyanga, imezuiwa kuuzwa.

Hatua ya kuzuiwa kwa shehena hiyo kuuzwa inatokana na hali tete iliyopo baada ya kuuzwa kwa mgodi huo uliokuwa chini ya kampuni ya kimataifa ya Willcroft, iliyokuwa na ubia na Serikali, kupitia kampuni yake ya De Beers.

Kamishna wa Madini nchini, Dk. Peter Kafumu, amethibitisha kuhusu kuzuiwa kwa kwa shehena hiyo ya almasi na kusema kwamba uamuzi huo umetokana na mchakato wa kuhamisha umiliki wa mgodi huo baada ya shughuli za kampuni ya Wilcroft kupitia De Beers kuuzwa kwa kampuni ya Petra Diamonds.

Alisema kutokana na hatua hiyo, Serikali imezuia kwa muda uuzwaji wa almasi katika mgodi huo ili kupisha mchakato mpya wa maelewano baada ya shughuli za mgodi huo kuuzwa.

Dk. Kafumu pia alikiri kuzuiwa kwa karati 45,000 za almasi zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.5. Thamani hiyo imetokana na bei ya soko kuwa dola za Marekani milioni 100 kwa kila karati moja.

"Kinachofanyika sasa ni kuendelea kwa mchakato wa maelewano baada ya mabadiliko ya mbia kati ya Serikali na mwekezaji. Kama unavyojua serikali ina hisa asilimia 25 na mbia asilimia 75," anasema Dk. Kafumu.

Katika uendeshaji wa mgodi huo, Serikali ilikuwa na hisa asilimia 25 wakati kampuni hiyo kwa kutumia kampuni ya De Beers, ikiwa na hisa asilimia 75.

Kwa sasa shughuli za mgodi huo zimeuzwa kwa kampuni ya Petra Diamonds kutoka Willcroft, kwa dola za Marekani milioni 10, katika uuzaji ambao unatajwa kutoipatia nchi mapato yaliyostahili, yakiwamo ya ushuru (Stamp Duty).

"Kimsingi migodi yote iliyofanya mabadiliko (kuuziana), Serikali imekuwa haipati fedha yoyote, kumbuka mgodi wa North Mara wa kampuni ya Placer Dome ya Canada kutoka kwa kampuni ya Afrika Mashariki ya Australia, na baadaye mgodi huo kuwa mikononi mwa Barrick ya Canada," kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Inaelezwa kuwa katika mgodi wa Williamson, licha ya Serikali kuwa na hisa asilimia 25, tangu mwaka 1994, imekuwa haina mwakilishi wake kwa upande wa uendeshaji hadi Mei, mwaka jana, na badala yake uwakilishi wa Serikali ulikuwa katika ngazi ya bodi ya wakurugenzi tu.

Habari zaidi zinaeleza kuwa katika kipindi hicho mgodi huo kupitia De Beers, umekuwa ukikopa fedha zilizofikia Dola za Marekani milioni 100 (zaidi ya sh bilioni 100), na kubwa zaidi imekuwa ikikopa fedha hizo kutoka kampuni ya Willcroft, ambayo ndiyo mama wa De Beers.

Mkopo umekuwa ukichukuliwa kwa awamu kwa madai kuwa mgodi umekuwa ukijiendesha kwa hasara, jambo ambalo ni vigumu kwa Serikali kuthibitisha kutokana na kutokuwa na mwakilishi wake katika uendeshaji.

"Kwa miaka kadhaa, De Beers wamekuwa wakidai kujiendesha kwa hasara, lakini wamekuwa wakiendelea kukopa. Mkopo sasa umefikia Dola za Marekani milioni 100. Inashangaza kuendelea kukopa huku ukilalamika kupata hasara.

"Mbali na De Beers kukopa kutoka katika kampuni yake mama ya Willcroft, pia iliweka masharti kwamba ni lazima almasi yote iuzwe katika kampuni yake nyingine ya DTC, hali ambayo watalaamu wanamini ni kuweka ukiritimba usio wa lazima.

"Kwa hiyo, De Beers ilikuwa ikieleza kuwa inapata hasara lakini ilikuwa ikikopa kutoka katika kampuni yake mama ya Willcroft lakini pia ilikuwa ikilazimisha almasi ziuzwe katika kampuni yake nyingine ya DTC. Wakati wote huu tangu mwaka 1994 hadi mwaka jana, Serikali haikuwa na mwakilishi katika shughuli za uendeshaji," kinadokeza chanzo chetu cha habari.
 
its time to recall the minister and leaders who were in power 1994-2005 ,to answer our questions kwanini uzembe mkubwa kiasi hiki ulifanyika,na isitoshe serikali inabidi iongeze percentage of ownership,25% ni ndogo saana ,kwani hiyo almasi iliyopo tu inathamani ya dola 4.5million kampuni ya Debeers inauzwa kwa dola 10million,hapo inaonyesha wazi kuna wizi mtupu kuibia serikali yetu.
 
Shehena kubwa ya almasi yazuiwa

Ni ya mgodi wa Williamson, Shinyanga

Kisa ni hali tete ya kuuzwa kwa mgodi

Mwandishi Wetu Machi 25, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

SHEHENA ya almasi inayotajwa kuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 4.5 (zaidi ya Sh bilioni 4.5) iliyopo katika Mgodi wa Almasi wa Wiliamson, uliopo eneo la Maganzo, mkoani Shinyanga, imezuiwa kuuzwa.

Hatua ya kuzuiwa kwa shehena hiyo kuuzwa inatokana na hali tete iliyopo baada ya kuuzwa kwa mgodi huo uliokuwa chini ya kampuni ya kimataifa ya Willcroft, iliyokuwa na ubia na Serikali, kupitia kampuni yake ya De Beers.

Kamishna wa Madini nchini, Dk. Peter Kafumu, amethibitisha kuhusu kuzuiwa kwa kwa shehena hiyo ya almasi na kusema kwamba uamuzi huo umetokana na mchakato wa kuhamisha umiliki wa mgodi huo baada ya shughuli za kampuni ya Wilcroft kupitia De Beers kuuzwa kwa kampuni ya Petra Diamonds.

Alisema kutokana na hatua hiyo, Serikali imezuia kwa muda uuzwaji wa almasi katika mgodi huo ili kupisha mchakato mpya wa maelewano baada ya shughuli za mgodi huo kuuzwa.

Dk. Kafumu pia alikiri kuzuiwa kwa karati 45,000 za almasi zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.5. Thamani hiyo imetokana na bei ya soko kuwa dola za Marekani milioni 100 kwa kila karati moja.

“Kinachofanyika sasa ni kuendelea kwa mchakato wa maelewano baada ya mabadiliko ya mbia kati ya Serikali na mwekezaji. Kama unavyojua serikali ina hisa asilimia 25 na mbia asilimia 75,” anasema Dk. Kafumu.

Katika uendeshaji wa mgodi huo, Serikali ilikuwa na hisa asilimia 25 wakati kampuni hiyo kwa kutumia kampuni ya De Beers, ikiwa na hisa asilimia 75.

Kwa sasa shughuli za mgodi huo zimeuzwa kwa kampuni ya Petra Diamonds kutoka Willcroft, kwa dola za Marekani milioni 10, katika uuzaji ambao unatajwa kutoipatia nchi mapato yaliyostahili, yakiwamo ya ushuru (Stamp Duty).

“Kimsingi migodi yote iliyofanya mabadiliko (kuuziana), Serikali imekuwa haipati fedha yoyote, kumbuka mgodi wa North Mara wa kampuni ya Placer Dome ya Canada kutoka kwa kampuni ya Afrika Mashariki ya Australia, na baadaye mgodi huo kuwa mikononi mwa Barrick ya Canada,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Inaelezwa kuwa katika mgodi wa Williamson, licha ya Serikali kuwa na hisa asilimia 25, tangu mwaka 1994, imekuwa haina mwakilishi wake kwa upande wa uendeshaji hadi Mei, mwaka jana, na badala yake uwakilishi wa Serikali ulikuwa katika ngazi ya bodi ya wakurugenzi tu.

Habari zaidi zinaeleza kuwa katika kipindi hicho mgodi huo kupitia De Beers, umekuwa ukikopa fedha zilizofikia Dola za Marekani milioni 100 (zaidi ya sh bilioni 100), na kubwa zaidi imekuwa ikikopa fedha hizo kutoka kampuni ya Willcroft, ambayo ndiyo mama wa De Beers.

Mkopo umekuwa ukichukuliwa kwa awamu kwa madai kuwa mgodi umekuwa ukijiendesha kwa hasara, jambo ambalo ni vigumu kwa Serikali kuthibitisha kutokana na kutokuwa na mwakilishi wake katika uendeshaji.

“Kwa miaka kadhaa, De Beers wamekuwa wakidai kujiendesha kwa hasara, lakini wamekuwa wakiendelea kukopa. Mkopo sasa umefikia Dola za Marekani milioni 100. Inashangaza kuendelea kukopa huku ukilalamika kupata hasara.

“Mbali na De Beers kukopa kutoka katika kampuni yake mama ya Willcroft, pia iliweka masharti kwamba ni lazima almasi yote iuzwe katika kampuni yake nyingine ya DTC, hali ambayo watalaamu wanamini ni kuweka ukiritimba usio wa lazima.

“Kwa hiyo, De Beers ilikuwa ikieleza kuwa inapata hasara lakini ilikuwa ikikopa kutoka katika kampuni yake mama ya Willcroft lakini pia ilikuwa ikilazimisha almasi ziuzwe katika kampuni yake nyingine ya DTC. Wakati wote huu tangu mwaka 1994 hadi mwaka jana, Serikali haikuwa na mwakilishi katika shughuli za uendeshaji,” kinadokeza chanzo chetu cha habari.

Nimesoma vizuri au macho yamenidanganya? Umeuzwa Kwa dola millioni 10? Wakowapi kina vijisenti na RA kama serikali haina hizo za kununulia hisa zilizobakia.

Kwa hili hata vijisenti na RA tunaweza kuwafumbia macho hasa tulivyokwishajuwa kuwa si dhambi kwa Vigogo wa Serikali/Bunge kumiliki MAHISA.
 
Back
Top Bottom