Shehe: Profesa Janabi anataka kutuua, atatuvunjia ndoa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,861
18,285
Shehe mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja amesikika akisema kwamba, kwa ulaji ule wa Profesa Janabi, ukiwa muislamu mwenye wake wanne unaweza kushindwa kumlisha mkeo "chakula cha chini" na hatimaye ndoa zikavunjika.

Amesema haya akiwa na maana kuwa ukibahatika kuoa mwali machachari anayependa kuona mume akishinda kifuani kwake kwa saa 24, utakosa pumzi ya kumhudumia kisawasawa na matokeo yake ndoa itakata roho mapema sana. Sitaki kusema mengi, hebu msikilize wewe mwenyewe hapa chini.

MAONI YANGU
Namuunga mkono huyu shehe tena nampongeza sana kwa ujasiri wa kuweka hili jambo bayana kwani watu wengine wanazo hoja kama yeye lakini wanaogopa kutoka hadharani na kusema kwa kumuogopa Profesa Janabi. Watu jasiri kama hawa ndio wanatakiwa katika nchi hii ili nchi iapate maendeleo haraka.

Nawasilisha.
 
Hakuna watu wa hovyo kama watu wanaojificha kwenye magwanda ya udini. Yako mambo ya kuongea hadharani na yako mambo sio, unaongea mambo ya kikubwa humo msikitini kuna watoto wengi tu wanakuja kuswali. Nini tunawafundisha. Hii imekuwa fashion siku tena nasema viongozi wa dini zote wamekuwa wanaongea mambo yasiokuwa na staha kwenye misikiti na makanisani. Unaweza kuwa uko kanisani na mkeo, watoto zako sijui wajukuu anatokea muhibiri anaongelea mambo ya ngono. Na misikitini hivyo hivyo.
 
Uzuri viongozi wa dini hawamuogopi mtu yeyote mkuu.
 
Hakuna watu wa hovyo kama watu wanaojificha kwenye magwanda ya udini. Yako mambo ya kuongea hadharani na yako mambo sio, unaongea mambo ya kikubwa humo msikitini kuna watoto wengi tu wanakuja kuswali. Nini tunawafundisha. Hii imekuwa fashion siku tena nasema viongozi wa dini zote wamekuwa wanaongea mambo yasiokuwa na staha kwenye misikiti na makanisani. Unaweza kuwa uko kanisani na mkeo, watoto zako sijui wajukuu anatokea muhibiri anaongelea mambo ya ngono. Na misikitini hivyo hivyo.
Ndio maana Kagame amewapiga pin mashehe na wachungaji wa mchingo kwa kuwawekea utaratibu maalumu wa kufanya shughuli zao. Ikiwa mtu akishindwa, huondolewa na kufutiwa leseni mara moja.
 
Back
Top Bottom