Sharobaro kasaidia wengi

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,176
305
Jamaa mmoja aliibiwa simu kwenye daladala, ila kutokana na utozi wake (usharobaro) akaona aibu kumwambia jirani yake aibeep ili ajue inalilia wapi.

Basi akamwambia dereva wa dala dala "hebu zima redio ya mkulima hiyo isiyochuja mziki, kisha kondakta apige namba yangu (huku akimtajia kondakta namba yake) ili usikie mziki uloenda shule.

Kondakta alipopiga ile namba, simu ikalia mlio wa nokia (tililiu tililiu) toka kwenye mfuko wa teja mmoja alekuwa karibu na mlango, basi yule sharobaro akatia "Mwizi wangu man, nipe hiyo blackberry nikupe samsung galaxy S3 man"
 
Mlio wa nokia?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom